Mithali 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 13:1-25

Mema Ya Muda Mfupi Na Yale Ya Kudumu

113:1 1Sam 2:25; Mit 10:1; 12:1; 15:5Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye,

bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.

213:2 Mit 12:14Kutoka tunda la midomo yake mtu hufurahia mambo mema,

bali wasio waaminifu wanatamani sana jeuri.

313:3 Za 12:2; Yak 3:2; Mit 10:6; Ay 1:22Yeye alindaye midomo yake hulinda nafsi yake,

bali yeye asemaye kwa haraka ataangamia.

413:4 Mit 21:25-26Mvivu hutamani sana na hapati kitu,

bali nafsi ya mwenye bidii

hutoshelezwa kikamilifu.

513:5 Kol 3:9; Rum 12:9Mwenye haki huchukia uongo,

bali waovu huleta aibu na fedheha.

613:6 Mit 11:3-5; Yer 44:5Haki humlinda mtu mwadilifu,

bali uovu humwangusha mwenye dhambi.

713:7 2Kor 6:10Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote;

mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.

813:8 Mit 15:16Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake,

bali mtu maskini hasikii kitisho.

913:9 Ay 18:5; Mit 4:18-19Nuru ya mwenye haki hungʼaa sana,

bali taa ya mwovu itazimwa.

1013:10 Amu 19:30; Mit 9:9Kiburi huzalisha magomvi tu,

bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.

1113:11 Mit 10:2; 9:9; 20:21Fedha isiyo ya halali hupungua,

bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka.

1213:12 Mit 10:11Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua,

bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima.

1313:13 Hes 15:31; Kut 9:20; Mit 16:20; 2Nya 36:16Yeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi,

bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo.

1413:14 Mit 10:11; 14:27Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima,

ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.

15Ufahamu mzuri hupata upendeleo,

bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu.

1613:16 Es 5:11; Mit 12:23Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa,

bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake.

1713:17 Mit 10:26; 25:13Mjumbe mwovu huanguka kwenye taabu,

bali mjumbe mwaminifu huleta uponyaji.

1813:18 Mit 15:31-32; Za 141:5Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu,

bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa.

1913:19 Mit 10:11Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi,

bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya.

2013:20 2Nya 10:8Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima,

bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara.

2113:21 Za 32:10; Mit 19:17; 11:12Balaa humwandama mtenda dhambi,

bali mafanikio ni thawabu kwa mwenye haki.

2213:22 Es 8:2; Mhu 2:26Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi,

bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa

kwa ajili ya wenye haki.

2313:23 Mit 12:11Shamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi,

bali dhuluma hukifutilia mbali.

2413:24 Mit 29:15-17; Efe 6:4Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe,

bali yeye ampendaye

huwa mwangalifu kumwadibisha.

2513:25 Za 34:10; Mit 10:3Mwenye haki hula mpaka akaridhisha moyo wake,

bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa.