Mithali 12 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 12:1-28

Mafundisho Ya Kifamilia Na Ya Kijamii

112:1 Mit 5:11-14; 9:7-9; 13:1, 18; 15:5, 10Yeyote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa,

bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu.

212:2 Ay 33:26; Za 84:11; 2Sam 15:3; Mit 11:20Mtu mwema hupata kibali kutoka kwa Bwana,

bali Bwana humhukumu mwenye hila.

312:3 Mit 10:25Mtu hathibitiki kutokana na uovu,

bali mwenye haki hataondolewa.

412:4 Mit 14:30; 31:23; 1Kor 11:7; Rum 3:11Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe,

bali aaibishaye ni kama uozo

katika mifupa ya mumewe.

5Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki,

bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu.

612:6 Mit 11:9; 14:3Maneno ya waovu huotea kumwaga damu,

bali maneno ya waadilifu huwaokoa.

712:7 Mt 7:24; Za 37:34; Mit 14:11; 15:25Watu waovu huondolewa na kutoweka,

bali nyumba ya mwenye haki husimama imara.

812:8 1Sam 13:13; Mal 2:8-9; Mt 27:4-5Mtu husifiwa kulingana na hekima yake,

bali watu wenye akili zilizopotoka hudharauliwa.

9Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi,

kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula.

1012:10 Kum 25:4; Hes 22:29Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake,

bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili.

1112:11 Mwa 3:19; Efe 4:28Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,

bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.

1212:12 Za 1:3; Lk 8:15Waovu hutamani mateka ya watu wabaya,

bali shina la mwenye haki hustawi.

1312:13 Za 59:12; Mit 10:6; 21:23; 2Pet 2:9Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi,

bali mwenye haki huepuka taabu.

1412:14 Mit 15:23; 14:14; Isa 3:10-11Kutokana na tunda la midomo yake

mtu hujazwa na mambo mema,

hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza.

1512:15 Mit 16:2, 25; Lk 18:11Njia ya mpumbavu huonekana sawa

machoni pake mwenyewe,

bali mtu mwenye hekima husikiliza ushauri.

1612:16 1Sam 25:25; Ay 5:2; Mit 29:11Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara moja,

bali mtu wa busara hupuuza matukano.

1712:17 Za 12:2; Mit 14:5, 25Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika,

bali shahidi wa uongo husema uongo.

1812:18 Za 57:4; Mit 25:18; 15:4Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga,

bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.

1912:19 Zek 1:5, 6Midomo isemayo kweli hudumu milele,

bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.

2012:20 Rum 14:19Upo udanganyifu katika mioyo

ya wale ambao hupanga mabaya,

bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani.

2112:21 Ay 4:7; Za 91:10; Rum 8:28Hakuna dhara linalompata mwenye haki,

bali waovu wana taabu nyingi.

2212:22 1Fal 13:18; Ufu 22:15; Mit 11:20Bwana anachukia sana midomo idanganyayo,

bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.

2312:23 Mit 10:14; Za 38:5; 59:7; Mit 18:2Mtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe,

bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu.

2412:24 Mit 10:4; 1Fal 11:28Mikono yenye bidii itatawala,

bali uvivu huishia katika kazi za utumwa.

2512:25 Mit 15:13; Isa 50:4Moyo wa wasiwasi humlemea mtu,

bali neno la huruma humfurahisha.

2612:26 Za 95:10Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki,

bali njia ya waovu huwapotosha.

27Mtu mvivu haoki mawindo yake,

bali mtu mwenye bidii ana mali za thamani.

2812:28 Kum 30:15; Rum 5:21; Mit 10:2Katika njia ya haki kuna uzima;

katika mapito hayo kuna maisha ya milele.