Mithali 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 10:1-32

Mithali Za Solomoni

110:1 1Fal 4:32; Mit 1:1; 15:20; 17:21; 19:13; 23:22; 27:11; 29:3Mithali za Solomoni:

Mwana mwenye hekima

huleta furaha kwa baba yake,

lakini mwana mpumbavu

huleta huzuni kwa mama yake.

210:2 Dan 4:27; Mit 13:11; 21:6; 12:28; Lk 12:29Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai,

lakini uadilifu huokoa kutoka mautini.

310:3 Za 10:14; Mt 6:25-34Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa,

lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu.

410:4 Mit 24:30-34; 13:4Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini

lakini mikono yenye bidii huleta utajiri.

510:5 Mit 24:30-34Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi

ni mwana mwenye hekima,

lakini yeye alalaye wakati wa mavuno

ni mwana mwenye kuaibisha.

610:6 Es 7:8; Mit 13:3; Mhu 10:12Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki,

lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.

710:7 Mhu 8:10; Ay 18:17; Za 109:13Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka,

lakini jina la mwovu litaoza.

810:8 Ay 33:33; Mt 7:24-27Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo,

lakini mpumbavu apayukaye huangamia.

910:9 Za 23:4; 25:21; Isa 33:15; Mit 28:18Mtu mwadilifu hutembea salama,

lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.

1010:10 Za 35:19Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni,

naye mpumbavu apayukaye huangamia.

1110:11 Za 37:30; Mit 3:18Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima,

lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.

1210:12 Mit 17:9; 1Kor 13:4-7; 1Pet 4:8Chuki huchochea faraka,

lakini upendo husitiri mabaya yote.

1310:13 Za 37:30; Mit 15:7; Kum 25:2; Lk 4:22Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua,

lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu.

1410:14 Za 59:12; Mt 12:37Wenye hekima huhifadhi maarifa,

bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi.

1510:15 Mit 18:11; Ay 31:24; 1Tim 6:17Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome,

bali ufukara ni maangamizi ya maskini.

1610:16 Kum 30:15; Mit 11:18-19; 15:6; Rum 6:23Ujira wa wenye haki huwaletea uzima,

lakini mapato ya waovu huwaletea adhabu.

1710:17 Mit 6:23; 15:5Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima,

lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.

1810:18 Za 31:18Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo,

na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu.

1910:19 Yak 1:19; Mhu 5:3; Za 39:1Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani,

lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara.

20Ulimi wa mwenye haki ni fedha iliyo bora,

bali moyo wa mwovu una thamani ndogo.

2110:21 Isa 5:13; Yer 5:4Midomo ya mwenye haki hulisha wengi,

lakini wapumbavu hufa kwa kukosa ufahamu.

2210:22 Mwa 12:2; 13:2; Za 37:22; Kum 8:17-18Baraka ya Bwana hutajirisha,

wala haichanganyi huzuni.

2310:23 Mit 2:14Mpumbavu hufurahia tabia mbaya,

lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima.

2410:24 Isa 66:4; Mt 5:6; Ay 15:21Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata;

kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa.

2510:25 Za 20:8; Mt 7:24-27Tufani inapopita, waovu hutoweka,

lakini wenye haki husimama imara milele.

2610:26 Isa 65:5; Mit 13:17; 25:13; 26:6Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho,

ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma.

2710:27 Kum 11:9; Mit 22:4; Mhu 7:17; Ay 15:32Kumcha Bwana huongeza urefu wa maisha,

lakini miaka ya mwovu inafupishwa.

2810:28 Es 7:10; Ay 8:13; Za 16:9Tarajio la mwenye haki ni furaha,

bali matumaini ya mwovu huwa si kitu.

2910:29 Za 10:12; Mit 21:15; Hos 14:9Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki,

lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya.

3010:30 Za 37:28-29; Mit 2:20-22Kamwe wenye haki hawataondolewa,

bali waovu hawatasalia katika nchi.

3110:31 Mit 10:13; 15:2; 31:26; Za 52:4Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima,

bali ulimi wa upotovu utakatwa.

3210:32 Mhu 10:12; Za 59:7Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa,

bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.