Utangulizi: Kusudi Na Kiini
11:1 1Fal 4:29-34Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:
2Kwa kupata hekima na nidhamu;
kwa kufahamu maneno ya busara;
31:3 Mit 2:1; 2:1, 9kwa kujipatia nidhamu na busara,
kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;
41:4 Mit 8:5, 12; 2:10-11huwapa busara wajinga,
maarifa na akili kwa vijana;
51:5 Mit 9:9wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,
wenye kupambanua na wapate mwongozo;
61:6 Za 78:2; Mt 13:10-17; Hes 12:8; Amu 14:12kwa kufahamu mithali na mifano,
misemo na vitendawili vya wenye hekima.
71:7 Kut 20:20; Ay 28:28Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa,
lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Onyo Dhidi Ya Ushawishi Wa Marafiki Waovu
81:8 Mit 6:20; 22:17; Kum 21:18Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,
wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
91:9 Mit 3:21-22; 4:1-9Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,
na mkufu wa kuipamba shingo yako.
101:10 Mwa 39:7; Ay 24:15; Kum 13:8; Rum 16:18Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi,
usikubaliane nao.
111:11 Mit 12:6; Yer 5:26; Mik 7:2Kama wakisema, “Twende tufuatane;
tukamvizie mtu na kumwaga damu,
njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;
121:12 Ay 33:18; Mwa 38:25; Za 40:3tuwameze wakiwa hai kama kaburi,1:12 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.
13Tutapata aina zote za vitu vya thamani
na kujaza nyumba zetu kwa nyara.
141:14 Mit 1:19Njoo ushirikiane nasi,
vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”
151:15 Za 119:101; Mwa 49:6; Mit 4:14Mwanangu, usiandamane nao.
Usiweke mguu wako katika njia zao,
161:16 Mit 6:18; Isa 59:7kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,
ni wepesi kumwaga damu.
17Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu
wakati ndege wote wanakuona!
181:18 Za 71:10Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe;
hujivizia tu wenyewe!
191:19 Mit 11:19; 15:27; 2Fal 5:20-27Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila;
huuondoa uhai wa wale wenye mali.
Onyo Dhidi Ya Kukataa Hekima
201:20 Ay 28:12; Mt 7:10-13; 9:1-3, 13-15Hekima huita kwa sauti kuu barabarani,
hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa;
21kwenye makutano ya barabara za mji
zenye makelele mengi hupaza sauti,
kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake:
221:22 Mit 6:32; 7:7; 8:5; 9:4, 16; Za 50:17“Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini?
Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha,
na wapumbavu kuchukia maarifa?
231:23 Yoe 2:28; Yn 7:37Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu,
ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu
na kuwafahamisha maneno yangu.
241:24 Isa 65:12; Zek 7:11Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita
na hakuna yeyote aliyekubali
niliponyoosha mkono wangu,
251:25 Lk 7:30kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote
na hamkukubali karipio langu,
261:26 Za 2:4; Kum 28:63; Mit 10:24mimi nami nitawacheka katika maafa yenu,
nitawadhihaki wakati janga litawapata:
271:27 Za 18:18; Mit 5:12-14wakati janga litawapata kama tufani,
wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli,
wakati dhiki na taabu zitawalemea.
281:28 Isa 1:15; Mik 3:4; Eze 8:18; Hos 5:6“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu;
watanitafuta lakini hawatanipata.
291:29 Ay 21:14; Isa 27:11; Mdo 7:51Kwa kuwa walichukia maarifa,
wala hawakuchagua kumcha Bwana,
301:30 Ay 21:14; Za 81:11kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu,
na kukataa maonyo yangu,
311:31 2Nya 36:16; Yer 14:16watakula matunda ya njia zao,
na watashibishwa matunda ya hila zao.
321:32 Isa 66:4; Yer 2:19Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua,
nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza.
331:33 Hes 24:21; Za 25:12; 112:8Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama,
atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”