Mika 6 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mika 6:1-16

Shauri La Bwana Dhidi Ya Israeli

16:1 Za 50:1; Eze 6:2Sikiliza asemalo Bwana:

“Simama, tetea shauri lako mbele ya milima;

vilima na visikie lile unalotaka kusema.

26:2 Kum 32:1; Hos 12:2; Isa 3:13; Za 50:7; Yer 9:7Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya Bwana,

sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia.

Kwa kuwa Bwana ana shauri dhidi ya watu wake;

anatoa mashtaka dhidi ya Israeli.

36:3 Za 50:7; Isa 5:3, 4; Yer 2:31; 2:5“Watu wangu, nimewatendea nini?

Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu.

46:4 Kum 7:8; Kut 3:10; 6:6; 4:16; 15:20; Hes 33:1; Za 77:20Nimewatoa kutoka Misri na kuwakomboa

kutoka nchi ya utumwa.

Nilimtuma Mose awaongoze,

pia Aroni na Miriamu.

56:5 Hes 22:2-6Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu

alivyofanya shauri

na kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu.

Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu mpaka Gilgali,

ili mfahamu matendo ya haki ya Bwana.”

66:6 Yn 6:28; Za 15:1; 40:6-8; 95:2; 51:16-17Nimjie Bwana na kitu gani na kusujudu

mbele za Mungu aliyetukuka?

Je, nije mbele zake na sadaka za kuteketezwa,

nije na ndama za mwaka mmoja?

76:7 Isa 1:11; 40:16; Law 18:21; Za 50:8-10; 2Fal 3:27; 16:3; Amo 5:22; Hos 5:6Je, Bwana atafurahishwa na kondoo dume elfu,

au mito elfu kumi ya mafuta?

Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu,

mtoto wangu mwenyewe

kwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu?

86:8 Isa 1:17; Yer 22:3; 23:23; 2Fal 22:19; Isa 57:15; Mwa 5:22; 1Sam 15:22; Kum 10:12-13; Zek 7:9-10; Mt 9:13; Mk 12:33; Lk 11:42Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu.

Bwana anataka nini kwako?

Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema,

na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.

Hatia Na Adhabu Ya Israeli

96:9 Mwa 17:1; Isa 11:4Sikiliza! Bwana anauita mji:

kulicha jina lako ni hekima:

“Tii hiyo fimbo na yeye aliyeiamuru.

106:10 Eze 45:9-10; Amo 3:10; 8:4-6Je, bado nisahau, ee nyumba ya uovu,

hazina yako uliyopata kwa udanganyifu

na vipimo vilivyopunguka,

ambavyo vimelaaniwa?

116:11 Law 19:36; Hos 12:7; Amu 3:10; Kum 25:13Je, naweza kuhukumu kuwa

mtu mwenye mizani ya udanganyifu hana hatia,

aliye na mfuko wa mawe ya kupimia ya uongo?

126:12 Isa 1:23; 3:8; Za 35:20; 116:11; Yer 9:5Matajiri wake ni wajeuri;

watu wake ni waongo

na ndimi zao zinazungumza

kwa udanganyifu.

13Kwa hiyo, nimeanza kukuharibu,

kuwaangamiza kwa sababu ya dhambi zenu.

146:14 Isa 9:20; 30:6; Hos 4:10Mtakula lakini hamtashiba;

matumbo yenu bado yatakuwa matupu.

Mtaweka akiba lakini hamtaokoa chochote,

kwa sababu mtakachoweka akiba

nitatoa kwa upanga.

156:15 Kum 28:36-38; Yer 12:13; Ay 24:11; Amo 5:11; Sef 1:13Mtapanda lakini hamtavuna;

mtakamua zeituni lakini

hamtatumia mafuta yake.

Mtakamua zabibu

lakini hamtakunywa hiyo divai.

166:16 1Fal 16:25, 29-33; Yer 7:24; 25:9; 51:51; Mik 2:6Mmezishika sheria za Omri

na matendo yote ya nyumba ya Ahabu,

tena umefuata desturi zao.

Kwa hiyo nitakutoa kwa maangamizi

na watu wako kuwa dhihaka;

mtachukua dharau za mataifa.”