Mika 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mika 3:1-12

Viongozi Na Manabii Wakemewa

13:1 Yer 5:5Kisha nikasema,

“Sikilizeni enyi viongozi wa Yakobo,

enyi watawala wa nyumba ya Israeli.

Je, hampaswi kujua hukumu,

23:2 Za 53:4; Eze 22:27ninyi mnaochukia mema

na kupenda maovu;

ninyi mnaowachuna watu wangu ngozi

na kuondoa nyama kwenye mifupa yao;

33:3 Za 14:4; Sef 3:3; Ay 24:14; Eze 11:7; 24:4-5; 34:4ninyi mnaokula nyama ya watu wangu,

mnaowachuna ngozi

na kuvunja mifupa yao vipande vipande;

mnaowakatakata kama nyama

ya kuwekwa kwenye sufuria

na kama nyama

ya kuwekwa kwenye chungu?”

43:4 Kum 1:45; 31:17; 1Sam 8:18; Yer 11:11; Isa 58:4; Mit 1:28; Ay 15:31; Eze 8:18Kisha watamlilia Bwana,

lakini hatawajibu.

Wakati huo atawaficha uso wake

kwa sababu ya uovu waliotenda.

53:5 Isa 3:12; 9:16; 53:6; 56:10; Mt 7:15; Yer 4:10Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kuhusu manabii wanaowapotosha watu wangu,

mtu akiwalisha,

wanatangaza ‘amani’;

kama hakufanya hivyo,

wanaandaa kupigana vita dhidi yake.

63:6 Isa 8:19-22; 29:10; Eze 7:26; 12:24Kwa hiyo usiku utawajieni, msiweze kuwa na maono,

na giza, msiweze kubashiri.

Jua litawachwea manabii hao,

nao mchana utakuwa giza kwao.

73:7 Yer 6:15; Mik 7:16; Isa 44:25; Es 6:12; Za 74:9; Amu 8:11; Law 13:45; Eze 20:3Waonaji wataaibika

na waaguzi watafedheheka.

Wote watafunika nyuso zao

kwa sababu hakuna jibu litokalo kwa Mungu.”

83:8 1Kor 2:1, 4; Isa 58:1; 57:12; 61:2Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu,

nimejazwa Roho wa Bwana,

haki na uweza,

kumtangazia Yakobo kosa lake,

na Israeli dhambi yake.

93:9 Isa 58:1-2; 1:23Sikieni hili, enyi viongozi wa nyumba ya Yakobo,

enyi watawala wa nyumba ya Israeli,

mnaodharau haki

na kupotosha kila lililo sawa;

103:10 Yer 22:13, 17; Isa 59:7; Mik 7:2; Hab 2:12; Nah 3:1; Eze 22:27mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu

na Yerusalemu kwa uovu.

113:11 Kut 23:8; Law 19:15; Mal 2:9; Eze 22:12; Mik 7:3; Yer 6:13; 1Tim 1:11; 1Sam 4:5-6; Eze 13:19; 34:2; Isa 1:23; 10:20; 56:11; Yer 6:13; 7:4; Mao 4:13; Hos 4:8, 18Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa,

na makuhani wake wanafundisha kwa malipo,

nao manabii wake wanatabiri kwa fedha.

Hata hivyo wanamwegemea Bwana na kusema,

“Je, Bwana si yumo miongoni mwetu?

Hakuna maafa yatakayotupata.”

123:12 2Fal 25:9; Isa 6:11; Mik 1:6; Za 79:1; Yer 52:13; 22:6; Mao 5:18; Eze 5:14Kwa hiyo kwa sababu yenu,

Sayuni italimwa kama shamba,

Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto,

na kilima cha Hekalu

kitakuwa kichuguu

kilichofunikwa na vichaka.