Mika 2 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mika 2:1-13

Mipango Ya Mwanadamu Na Ya Mungu

12:1 Isa 29:20; 32:7; Es 3:8, 9; Za 36:4; 7:11-14; Hos 7:6; Mwa 31:29Ole kwa wale wapangao uovu,

kwa wale wafanyao shauri la hila vitandani mwao!

Kunapopambazuka wanalitimiza

kwa sababu uko katika uwezo wao kutekeleza.

22:2 Isa 1:23; 5:8; Mit 30:14; Yer 22:17; 1Sam 8:14; Eze 46:18Wanatamani mashamba na kuyakamata,

pia nyumba na kuzichukua.

Wanamlaghai mwanaume nyumba yake,

mwanadamu mwenzake urithi wake.

32:3 Yer 18:11; 8:3; Amo 3:1-2; Isa 2:12Kwa hiyo, Bwana asema:

“Ninapanga maangamizi dhidi ya watu hawa,

ambayo hamwezi kujiokoa wenyewe.

Hamtatembea tena kwa majivuno,

kwa kuwa utakuwa ni wakati wa maafa.

42:4 Law 26:31; Yer 4:13; 6:12Siku hiyo watu watawadhihaki,

watawafanyia mzaha

kwa wimbo huu wa maombolezo:

‘Tumeangamizwa kabisa;

mali ya watu wangu imegawanywa.

Ameninyangʼanya!

Ametoa mashamba yetu kwa wasaliti.’ ”

52:5 Kum 32:8, 9, 13; Yos 18:4; Hes 34:13Kwa hiyo hutakuwa na yeyote katika kusanyiko la Bwana

wa kugawanya mashamba kwa kura.

Manabii Wa Uongo

62:6 Za 44:13; Yer 19:8; 18:16; 25:18; 29:18; Mik 6:16; Amo 2:12Manabii wao husema, “Usitabiri.

Usitabiri kuhusu vitu hivi;

aibu haitatupata.”

72:7 Za 119:65; 15:2; 84:11Je, ingesemwa, ee nyumba ya Yakobo:

“Je, Roho wa Bwana amekasirika?

Je, yeye hufanya vitu kama hivyo?”

“Je, maneno yangu hayamfanyii mema

yeye ambaye njia zake ni nyofu?

8Siku hizi watu wangu wameinuka

kama adui.

Unawavua joho la kitajiri wale wanaopita

pasipo kujali,

kama watu warudio kutoka vitani.

92:9 Yer 10:20Unawahamisha wanawake wa watu wangu

kutoka kwenye nyumba zao za kupendeza.

Unaondoa baraka yangu

kwa watoto wao milele.

102:10 Kum 12:9; Law 18:25-29; Za 106:38-39; Mao 4:15Inuka, nenda zako!

Kwa maana hapa sio mahali pako pa kupumzikia,

kwa sababu pametiwa unajisi,

pameharibiwa, wala hapatengenezeki tena.

112:11 2Nya 36:16; Yer 5:31; Law 10:9; Isa 30:10Ikiwa mwongo na mdanganyifu atakuja na kusema,

‘Nitawatabiria divai na pombe kwa wingi,’

angekuwa ndiye nabii

anayekubalika na watu hawa!

Ahadi Ya Ukombozi

122:12 Mik 4:6, 7; 5:7; 7:18; Isa 11:11; Sef 3:19; Neh 1:9“Hakika nitawakusanya ninyi nyote, ee Yakobo,

Hakika nitawaleta pamoja mabaki ya Israeli.

Nitawaleta pamoja kama kondoo ndani ya zizi,

kama kundi kwenye malisho yake,

mahali hapa patakuwa na msongamano wa watu.

132:13 Isa 52:12; 60:11Yeye afunguaye njia atawatangulia;

watapita kwenye lango na kutoka nje.

Mfalme wao atawatangulia,

Bwana atakuwa kiongozi.”