Mhubiri 9 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Mhubiri 9:1-18

Hatima Ya Wote

19:1 Mhu 8:14; 10:14; Kum 33:3; Ay 12:10Kwa hiyo niliyatafakari yote haya nikafikia uamuzi kwamba waadilifu na wenye hekima na yale wanayoyafanya yako mikononi mwa Mungu, lakini hakuna mtu ajuaye kama anangojewa na upendo au chuki. 29:2 Ay 9:22; Mhu 2:14; 6:6Wote wanayo hatima inayofanana, mwadilifu na mwovu, mwema na mbaya, aliye safi na aliye najisi, wale wanaotoa dhabihu na wale wasiotoa.

Kama ilivyo kwa mtu mwema,

ndivyo ilivyo kwa mtu mwenye dhambi;

kama ilivyo kwa wale wanaoapa,

ndivyo ilivyo kwa wale wasioapa.

39:3 Mhu 2:14; Yer 11:8; 17:9; Ay 21:26; 9:22; Yer 13:10; 16:12Huu ni ubaya ulio katika kila kitu kinachotendeka chini ya jua: Mwisho unaofanana huwapata wote. Zaidi ya hayo, mioyo ya watu, imejaa ubaya na kuna wazimu mioyoni mwao wangali hai, hatimaye huungana na waliokufa. 4Yeyote aliye miongoni mwa walio hai analo tumaini, hata mbwa hai ni bora kuliko simba aliyekufa!

59:5 Ay 14:21; Mhu 2:16; Za 9:6; Isa 26:14; 63:16Kwa maana walio hai wanajua kwamba watakufa,

lakini wafu hawajui chochote,

hawana tuzo zaidi,

hata kumbukumbu yao imesahaulika.

69:6 Ay 21:21Upendo wao, chuki yao na wivu wao

vimetoweka tangu kitambo,

kamwe hawatakuwa tena na sehemu

katika lolote linalotendeka chini ya jua.

79:7 Mhu 2:24; 8:15; Hes 6:20Nenda, kula chakula chako kwa furaha, unywe divai yako kwa moyo wa shangwe, kwa maana sasa Mungu anakubali unachofanya. 89:8 Za 23:5; Ufu 3:4Daima uvae nguo nyeupe na daima upake kichwa chako mafuta. 99:9 Mit 5:18; Ay 31:2Furahia maisha na mke wako, umpendaye, siku zote za maisha ya ubatili uliyopewa na Mungu chini ya jua, siku zote za ubatili. Kwa maana hili ndilo fungu lako katika maisha na katika kazi yako ya taabu chini ya jua. 109:10 Isa 38:18; 1Sam 10:7; Rum 12:11; Za 6:5; Mhu 2:24; 11:6; Hes 16:33Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakokwenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.

119:11 Amo 2:14-15; Yer 9:23; Kum 8:18; Ay 32:13; Isa 47:10; Mhu 2:14Nimeona kitu kingine tena chini ya jua:

Si wenye mbio washindao mashindano

au wenye nguvu washindao vita,

wala si wenye hekima wapatao chakula

au wenye akili nyingi wapatao mali,

wala wenye elimu wapatao upendeleo,

lakini fursa huwapata wote.

129:12 Mit 29:6; Za 73:22; Mhu 8:7; 2:14Zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ajuaye wakati saa yake itakapokuja:

Kama vile samaki wavuliwavyo katika wavu mkatili,

au ndege wanaswavyo kwenye mtego,

vivyo hivyo wanadamu hunaswa na nyakati mbaya

zinazowaangukia bila kutazamia.

Hekima Ni Bora Kuliko Upumbavu

139:13 2Sam 20:16-22Pia niliona chini ya jua mfano huu wa hekima ambao ulinivutia sana: 14Palikuwa na mji mdogo uliokuwa na watu wachache ndani yake. Mfalme mwenye nguvu akainuka dhidi yake, akauzunguka akaweka jeshi kubwa dhidi yake. 159:15 Mwa 40:14; Mhu 1:11; 2:16Katika mji huo kulikuwepo mtu mmoja maskini lakini mwenye hekima, naye akauokoa ule mji kwa hekima yake. Lakini hakuna aliyemkumbuka yule maskini. 169:16 Mhu 7:19; Mit 21:22; Es 6:3Kwa hiyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu.” Lakini hekima ya maskini imedharauliwa, wala hakuna anayesikiliza maneno yake.

179:17 2Sam 20:17; Dan 5:10Maneno ya utulivu ya mwenye hekima

husikiwa kuliko makelele ya mtawala wa wapumbavu.

189:18 Mhu 2:13; Rum 6:12, 16-23Hekima ni bora kuliko silaha za vita,

lakini mwenye dhambi mmoja

huharibu mema mengi.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

传道书 9:1-18

1我仔细思想、探究这一切事,就知道义人、智者及他们的行事为人都由上帝掌管,人无法知道前面等待自己的是爱还是恨。 2义人和恶人、好人和坏人、洁净的和污秽的、献祭的和不献祭的、行善的和犯罪的、敢于起誓的和不敢起誓的人,命运都一样。 3在日光之下有一件可悲的事,就是人的命运都一样。况且,人内心都充满邪恶,活着的时候行事狂妄,之后都步入死亡。 4有生命就有希望,一条活狗总比一头死狮子强。 5因为活着的人还知道自己终有一死,但死了的人什么都不知道,再也得不到任何赏赐,他们被忘得一干二净。 6他们的爱、恨和嫉妒早已不复存在,他们再也无法参与日光之下的任何事。

7去欢欢喜喜、快快乐乐地吃喝吧!因为上帝已经悦纳你所做的。 8你的衣服要经常保持洁白,头上也不要缺少膏油。 9在你虚空的人生中,就是在上帝所赐、日光之下虚空的岁月里,你要与爱妻快乐度日,因为这是你一生在日光之下的劳碌中所当得的。 10凡你的手能做的,都要尽力去做,因为在你要去的阴间没有工作,没有计划,也没有知识和智慧。 11我又发现,日光之下,跑得快的未必能得奖,强大的未必能得胜,智者未必得温饱,聪明人未必得财富,博学者未必受爱戴,因为时机和境遇左右众人。 12再者,人无法知道何时大难临头。祸患突然临到时,人根本无法摆脱,就像鱼落入险恶的网中,又像鸟儿陷入网罗。

13我看见日光之下有一种智慧,对我来说意义深远。 14有一个势力强大的君王来攻击一个人口不多的小城,他建造营垒围困这城。 15这城里有一个贫穷的智者,他用智慧拯救了这城,事后却无人记念他。 16我认为智慧胜过武力,然而那位穷人的智慧却被轻视,他所说的话也无人理会。 17听智者的细语,胜过听官长在愚人中的喊叫。 18智慧胜过兵器,但一个罪人却能破坏许多善事。