Mhubiri 7 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mhubiri 7:1-29

Hekima

17:1 Ufu 14:13; Wim 1:3; Mit 22:1; Ay 10:18Afadhali sifa nzuri kuliko manukato safi,

nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa.

27:2 Za 90:12; Mit 11:19; Mhu 2:14Afadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba

kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu,

kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu,

imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao.

37:3 2Kor 7:10; Mit 14:13Huzuni ni afadhali kuliko kicheko,

kwa sababu uso wenye huzuni wafaa kwa moyo.

47:4 Mhu 2:1; Yer 16:8Moyo wa wenye hekima uko katika nyumba ya msiba,

lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya anasa.

57:5 Za 141:5; Mit 13:18; 15:31-32Afadhali kusikia karipio la mtu mwenye hekima,

kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.

67:6 Za 58:9; Mhu 2:2; Mit 14:13Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria,

ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu.

Hili nalo pia ni ubatili.

77:7 Kut 18:21; 23:8; Kum 16:19Dhuluma humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu,

nayo rushwa huuharibu moyo.

87:8 Mit 14:29; Gal 5:22Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo wake,

uvumilivu ni bora kuliko kiburi.

97:9 Mit 16:32; 14:17, 29; Mt 5:22Usiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako,

kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.

10Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?”

Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo.

117:11 Mit 8:10-11; Mhu 2:13; 11:7Hekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema

na huwafaidia wale walionalo jua.

12Hekima ni ulinzi kama fedha ilivyo ulinzi,

lakini faida ya maarifa ni hii:

kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo.

137:13 Isa 14:27; Mhu 2:24; 1:15Tafakari kile Mungu alichokitenda:

Nani awezaye kunyoosha

kile ambacho yeye amekipinda?

147:14 Ay 1:21; Mhu 2:24Nyakati zikiwa nzuri, ufurahi,

lakini nyakati zikiwa mbaya, tafakari:

Mungu amefanya hiyo moja,

naam, sanjari7:14 Sanjari hapa maana yake mwandamano wa vitu, wanyama au watu. na hiyo nyingine.

Kwa hiyo, mwanadamu hawezi kugundua

kitu chochote kuhusu maisha yake ya baadaye.

157:15 Mhu 8:14; Yer 12:1; Ay 21:7; 7:7Katika maisha haya yangu ya ubatili nimeshaona haya mawili:

mtu mwadilifu akiangamia katika uadilifu wake,

naye mtu mwovu akiishi maisha marefu katika uovu wake.

16Usiwe mwenye haki kupita kiasi,

wala usiwe na hekima kupita kiasi:

kwa nini kujiangamiza mwenyewe?

177:17 Ay 15:32; Za 55:23Usiwe mwovu kupita kiasi,

wala usiwe mpumbavu:

kwa nini kufa kabla ya wakati wako?

187:18 Mhu 3:14Ni vyema kushika hilo moja

na wala usiache hilo jingine likupite.

Mtu amchaye Mungu ataepuka huko kupita kiasi.7:18 Au: atafuata hayo yote mawili.

197:19 Mhu 2:13; 9:13-18; Mit 8:14Hekima humfanya yeye aliye nayo kuwa na uwezo zaidi

kuliko watawala kumi katika mji.

207:20 1Fal 8:46; Rum 3:12, 23; Gal 3:22; Za 14:3; Mit 20:9; Ay 4:17Hakuna mtu mwenye haki duniani

ambaye hufanya mambo ya haki

na kamwe asitende dhambi.

217:21 Mit 30:10Usitie maanani kila neno linalosemwa na watu,

la sivyo, waweza kumsikia

mtumishi wako akikulaani:

22kwa kuwa unafahamu moyoni mwako

kwamba wewe mwenyewe mara nyingi

umewalaani wengine.

237:23 Mhu 1:17; Rum 1:22Yote haya niliyajaribu kwa hekima, nikasema,

“Nimeamua kuwa na hekima”:

lakini hii ilikuwa nje ya uwezo wangu.

247:24 Ay 28:12; 11:12; Isa 55:8-9Vyovyote hekima ilivyo,

hekima iko mbali sana na imejificha,

ni nani awezaye kuigundua?

257:25 Ay 28:3; Mhu 1:17Nikageuza fikira zangu ili kuelewa,

kuchunguza na kuitafuta hekima

na kusudi la mambo,

na ili kuelewa ujinga wa uovu,

na wazimu wa upumbavu.

267:26 Kut 10:7; Amu 14:15; Mit 7:23; 22:14; 2:16-19; 5:3-5Nimeona jambo lililo chungu kuliko mauti,

mwanamke ambaye ni mtego,

ambaye moyo wake ni wavu wa kutegea

na mikono yake ni minyororo.

Mtu ampendezaye Mungu atamkwepa,

bali mwenye dhambi atanaswa naye.

27Mhubiri anasema, “Tazama, hili ndilo nililogundua:

“Nimegundua kitu kimoja baada ya kingine nilipokuwa katika kusudi la mambo:

287:28 1Fal 11:3ningali natafiti

lakini sipati:

nilimpata mwanaume mmoja mnyofu miongoni mwa elfu,

lakini hakuna mwanamke mmoja mnyofu miongoni mwao.

29Hili ndilo peke yake nililolipata:

Mungu amemuumba mwanadamu mnyofu,

lakini mwanadamu amebuni mambo mengi.”