Mhubiri 11 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Mhubiri 11:1-10

Mkate Juu Ya Maji

111:1 Kum 15:10; 24:19; Hos 10:12; Mt 10:42; Isa 32:20; Mit 19:17Tupa mkate wako juu ya maji,

kwa maana baada ya siku nyingi

utaupata tena.

211:2 Mik 5:5; Efe 5:16; Za 112:9Wape sehemu watu saba, naam hata wanane,

kwa maana hujui ni baa gani

litakalokuwa juu ya nchi.

3Kama mawingu yamejaa maji,

hunyesha mvua juu ya nchi.

Kama mti ukianguka kuelekea kusini

au kuelekea kaskazini,

mahali ulipoangukia,

hapo ndipo utakapolala.

4Yeyote atazamaye upepo hatapanda,

yeyote aangaliaye mawingu hatavuna.

511:5 Za 139:14-16; Yn 3:8-10Kama vile usivyofahamu njia ya upepo,

au jinsi mwili uumbwavyo

ndani ya tumbo la mama,

vivyo hivyo huwezi kufahamu kazi ya Mungu,

Muumba wa vitu vyote.

611:6 Mhu 9:10Panda mbegu yako asubuhi,

nako jioni usiruhusu mikono yako ilegee,

kwa maana hujui ni ipi itakayofanikiwa,

kwamba ni hii au ni ile,

au kwamba zote zitafanikiwa sawasawa.

Mkumbuke Muumba Wako Ukiwa Bado Kijana

711:7 Mhu 7:11Nuru ni tamu,

tena inafurahisha macho kuona jua.

8Hata kama mtu ataishi miaka mingi kiasi gani,

na aifurahie yote.

Lakini na akumbuke siku za giza,

kwa maana zitakuwa nyingi.

Kila kitu kitakachokuja ni ubatili.

911:9 Ay 19:29; Kum 29:19; Mdo 14:16; Rum 14:10; Mhu 2:24; 3:17Furahi ewe kijana, wakati ungali kijana,

moyo wako na ukupe furaha

katika siku za ujana wako.

Fuata njia za moyo wako

na chochote macho yako yaonayo,

lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote

Mungu atakuleta hukumuni.

1011:10 2Kor 7:1; Za 94:19; Mhu 2:24Kwa hiyo basi, ondoa wasiwasi moyoni mwako

na utupilie mbali masumbufu ya mwili wako,

kwa kuwa ujana na nguvu ni ubatili.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

传道书 11:1-10

1当把你的粮食运到海外,

因为日久必有收获。

2当把你的投资分成七份,甚至八份,

因为你不知道日后会有什么灾难临到世上。

3云中满了水,就会下雨。

树不论倒向南或倒向北,

倒在哪里就躺在哪里。

4你若总指望风轻云淡的日子,

必无法撒种,无法收割。

5正如你不知道风的路线,不知道骨骼在母胎中如何形成,你也无法了解创造万物之上帝的作为。 6你早晚都要撒种,因为你不知道什么时候撒的会茁壮生长,或许早晚撒的长的一样好。 7光真美好,能够看见阳光真好! 8人一生不论活多久,都要活得快乐,但不要忘记死后有许多黑暗的日子。将来的一切都是虚空。 9年轻人啊,在年轻时要快乐,要在青春岁月里使自己的心欢畅。心里想做什么就去做,眼睛想看什么就去看。然而,要切记:上帝必照你所行的一切审判你。 10所以,你要抛开心中的烦恼和肉体的痛苦,因为青春年华转瞬即逝。