Mhubiri 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mhubiri 10:1-20

110:1 Mit 13:16; 18:2Kama vile nzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato,

ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima.

2Moyo wa mwenye hekima huelekea kuume,

lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto.

3Hata anapotembea barabarani,

mpumbavu hukosa ufahamu

na kudhihirisha kwa kila mmoja

jinsi alivyo mpumbavu.

410:4 Mit 16:14; 25:15; Mhu 8:3Kama hasira ya mtawala ikiwaka dhidi yako,

usiache mahali pako,

utulivu huweza kuzuia makosa mengi.

5Kuna ubaya niliouona chini ya jua,

aina ya kosa litokalo kwa mtawala:

610:6 Mit 29:2Wapumbavu kuwekwa kwenye nafasi nyingi za juu,

wakati matajiri hushika nafasi za chini.

710:7 Mit 19:10Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi,

wakati wakuu wakitembea

kwa miguu kama watumwa.

810:8 Es 2:23; Amo 5:19; Mit 26:27; Za 57:6; 9:16Yeye achimbaye shimo

aweza kutumbukia ndani yake,

yeyote abomoaye ukuta

anaweza kuumwa na nyoka.

910:9 Mit 26:27Yeyote apasuaye mawe

inawezekana yakamuumiza,

yeyote apasuaye magogo

inawezekana yakamuumiza.

10Kama shoka ni butu

na halikunolewa,

nguvu nyingi zinahitajika,

lakini ustadi utaleta mafanikio.

1110:11 Yer 8:17; Za 58:5; Isa 3:3Kama nyoka akiuma kabla ya kufanyiwa uaguzi,

mwaguzi hatahitajika tena.

1210:12 Mit 10:14, 32; 14:3; 15:2; 18:7Maneno yatokayo kinywani mwa mtu mwenye hekima

yana neema,

bali mpumbavu huangamizwa

na midomo yake mwenyewe.

13Mwanzoni maneno yake ni upumbavu,

mwishoni ni wazimu mbaya,

1410:14 Yak 4:14; Mit 15:2; Mhu 8:7; 5:3; 9:1naye mpumbavu huzidisha maneno.

Hakuna yeyote ajuaye linalokuja,

ni nani awezaye kueleza ni jambo gani

litakalotokea baada yake?

15Kazi ya mpumbavu humchosha mwenyewe,

hajui njia iendayo mjini.

1610:16 Isa 3:4-12Ole wako, ee nchi ambayo mfalme wako alikuwa mtumwa

na ambayo wakuu wako hufanya karamu asubuhi.

1710:17 Mit 31:4; Kum 14:26; 1Sam 25:36Heri wewe, ee nchi ambayo mfalme wako ni wa uzao wenye kuheshimika

na ambayo wakuu wako hula chakula kwa wakati unaofaa:

ili kupata nguvu na si kwa ajili ya ulevi.

1810:18 Mit 20:4; 24:30-34Kama mtu ni mvivu paa la nyumba huinama,

kutokana na mikono milegevu, nyumba huvuja.

1910:19 Mwa 14:18; Amu 9:13Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko,

nao mvinyo hufurahisha maisha,

lakini fedha ni jawabu la mambo yote.

2010:20 Kut 22:28Usimshutumu mfalme hata ikiwa ni katika mawazo yako,

au kumlaani tajiri katika chumba chako cha kulala,

kwa sababu ndege wa angani wanaweza kuchukua maneno yako,

naye ndege anayeruka anaweza kutoa taarifa ya yale uliyosema.