Mathayo 7 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mathayo 7:1-29

Kuwahukumu Wengine

(Luka 6:37-38, 41-42)

17:1 1Kor 5:12; Yak 4:11-12“Usihukumu ili usije ukahukumiwa. 27:2 Lk 6:38; Rum 2:1Kwa maana jinsi unavyowahukumu wengine, ndivyo utakavyohukumiwa, na kwa kipimo kile upimiacho, ndicho utakachopimiwa.

37:3 Lk 6:41, 42“Mbona unatazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na wala huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? 4Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Acha nitoe kibanzi kwenye jicho lako,’ wakati kuna boriti kwenye jicho lako mwenyewe? 5Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako.

67:6 Mt 9:7, 8; 23:9; Mdo 13:13, 45, 46; Mt 10:11“Msiwape mbwa vitu vilivyo vitakatifu; wala msitupie nguruwe lulu zenu. Kama mkifanya hivyo, watazikanyagakanyaga na kisha watawageukia na kuwararua vipande vipande.

Omba, Tafuta, Bisha

(Luka 11:9-13)

77:7 1Fal 3:5; Mk 11:24; Yer 29:13-14“Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. 87:8 Mit 8:17; 29:12-13Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango.

9“Au ni nani miongoni mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe? 10Au mwanawe akimwomba samaki atampa nyoka? 117:11 Yak 1:17Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? 127:12 Lk 6:31; Rum 13:8-10; Gal 5:14Kwa hiyo chochote mnachotaka mtendewe na watu, ninyi nanyi watendeeni vivyo hivyo. Kwa kuwa hii ndiyo Sheria na Manabii.

Njia Nyembamba Na Njia Pana

137:13 Lk 13:24; Yn 10:7-9“Ingieni kupitia mlango mwembamba, kwa maana lango ni pana na njia ni pana ielekeayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa kupitia lango hilo. 147:14 Mt 19:24; Mdo 14:22Lakini mlango ni mwembamba na njia ni finyu ielekeayo kwenye uzima, nao ni wachache tu waionao.

Mti Na Tunda Lake

(Luka 6:43-44)

157:15 Yer 23:16; Mk 13:22; Eze 22:27; Mdo 20:29; Isa 1:23“Jihadharini na manabii wa uongo, wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini ndani ni mbwa mwitu wakali. 167:16 Mt 12:33; Lk 6:44Mtawatambua kwa matunda yao. Je, watu huchuma zabibu kwenye miiba, au tini kwenye michongoma? 177:17 Mt 12:33Vivyo hivyo, mti mwema huzaa matunda mazuri, na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 187:18 Lk 6:43Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 197:19 Mt 3:10Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. 20Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.

Mwanafunzi Wa Kweli

(Luka 13:25-27)

217:21 Hos 8:2; Yn 13:13; Yak 1:22; 1Yn 3:18; Rum 2:13“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 227:22 Mt 10:15; Lk 10:20; Mdo 19:13Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo wachafu na kufanya miujiza mingi?’ 237:23 Za 6:8; Lk 13:25-27Ndipo nitakapowaambia wazi, ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’

Msikiaji Na Mtendaji

(Luka 6:47-49)

247:24 Mt 7:21; Yak 1:22-25“Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba. Lakini haikuanguka; kwa sababu msingi wake ulikuwa kwenye mwamba. 26Naye kila anayesikia haya maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 277:27 Eze 13:10, 11Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, nao upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.”

287:28 Mt 19:1; 26:1; Mk 11:18; Yn 7:46Yesu alipomaliza kusema maneno haya, makutano ya watu wakashangazwa sana na mafundisho yake, 297:29 Yn 7:46kwa sababu alifundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wao wa sheria.