Mathayo 28 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Mathayo 28:1-20

Yesu Afufuka

(Marko 16:1-10; Luka 24:1-12; Yohana 20:1-10)

128:1 Mt 27:56Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ya kwanza ya juma, Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikwenda kulitazama kaburi.

228:2 Mt 27:51; Yn 20:12; Mdo 5:9Ghafula, pakawa na tetemeko kubwa la ardhi, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaenda penye kaburi, akalivingirisha lile jiwe na kulikalia. 328:3 Dan 7:9; Yn 20:12Sura ya huyo malaika ilikuwa kama umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. 4Wale walinzi wa kaburi walimwogopa sana, wakatetemeka hata wakawa kama wafu.

528:5 Mt 14:27Yule malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope, kwa maana ninajua kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. 628:6 Mt 16:21Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama vile alivyosema. Njooni mpatazame mahali alipokuwa amelazwa. 728:7 Mt 26:32Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba, ‘Amefufuka kutoka kwa wafu, naye awatangulia kwenda Galilaya. Huko ndiko mtamwona. Sasa nimekwisha kuwaambia.’ ”

8Hivyo wale wanawake wakaondoka pale kaburini wakiwa wamejawa na hofu, bali wakiwa na furaha nyingi. Wakaenda mbio kuwaeleza wanafunzi wake habari hizo. 928:9 Yn 20:14-18Ghafula, Yesu akakutana nao, akasema, “Salamu!” Wale wanawake wakamkaribia, wakaishika miguu yake, wakamwabudu. 1028:10 Rum 8:29; Ebr 2:11-17Ndipo Yesu akawaambia, “Msiogope. Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona.”

Taarifa Ya Walinzi

1128:11 Mt 27:65-66Wakati wale wanawake walikuwa njiani wakienda, baadhi ya wale askari waliokuwa wakilinda kaburi walienda mjini na kuwaeleza viongozi wa makuhani kila kitu kilichokuwa kimetukia. 12Baada ya viongozi wa makuhani kukutana na wazee na kutunga hila, waliwapa wale askari kiasi kikubwa cha fedha 1328:13 Mt 27:64wakiwaambia, “Inawapasa mseme, ‘Wanafunzi wake walikuja wakati wa usiku na kumwiba sisi tulipokuwa tumelala.’ 1428:14 Mt 27:2Kama habari hizi zikimfikia mtawala, sisi tutamwondolea mashaka nanyi hamtapata tatizo lolote.” 15Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha nao wakafanya kama walivyoelekezwa. Habari hii imeenea miongoni mwa Wayahudi mpaka leo.

Yesu Awatuma Wanafunzi Wake

(Marko 16:14-18; Luka 24:36-49; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8)

1628:16 Mt 26:32Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda hadi Galilaya kwenye ule mlima ambao Yesu alikuwa amewaagiza. 17Walipomwona, wakamwabudu; lakini baadhi yao wakaona shaka. 1828:18 Dan 7:13, 14; Efe 1:20-22Yesu akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 1928:19 Isa 49:6; Mdo 14:21Kwa sababu hii, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, 2028:20 Mt 18:20; Yn 14:23nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

马太福音 28:1-20

耶稣复活

1安息日刚过,周日黎明时分,抹大拉玛丽亚和另一位玛丽亚一同到坟墓去察看。

2突然,大地剧烈地震动,主的天使从天而降,把墓口的石头滚开,坐在上面。 3他的容貌如闪电,衣裳洁白如雪。 4看守墓穴的卫兵吓得浑身发抖,像死人一样。

5天使对那两个女人说:“不要怕,我知道你们是在找那位被钉十字架的耶稣。 6祂不在这里,正如祂所说的,祂已经复活了。你们来看,这是安放祂的地方。 7现在你们快去告诉祂的门徒,祂已经从死里复活,要先你们一步去加利利,你们将在那里见到祂。记住,我已经告诉你们了。”

8她们听了又害怕又欣喜,连忙离开坟墓,跑去告诉门徒。 9忽然,耶稣迎面而来,对她们说:“愿你们平安!”她们就上前抱住祂的脚敬拜祂。

10耶稣对她们说:“不要害怕。你们去告诉我的弟兄,叫他们到加利利去,他们将在那里见到我。”

行贿造谣

11她们还在赶路的时候,有些守墓的卫兵已经进城把整件事告诉祭司长。 12祭司长和长老聚集商议,决定用重金买通守墓的卫兵,又吩咐他们: 13“你们就说,‘夜里我们熟睡的时候,耶稣的门徒来把祂的尸体偷走了。’ 14如果这件事传到总督那里,我们会跟他解释,保你们无事。” 15守卫收下钱,便依照吩咐去做。于是,这说法在犹太人中一直流传到今天。

大使命

16十一个门徒赶到加利利,到了耶稣和他们约定的山上, 17看到耶稣就敬拜祂,但有些人仍然心存疑惑。 18耶稣上前对门徒说:

“天上地下所有的权柄都交给我了。 19所以,你们要去使万民做我的门徒,奉父、子、圣灵的名给他们施洗, 20教导他们遵守我吩咐你们的一切。记住,我必常与你们同在,一直到世界的末了。”