Mathayo 27 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mathayo 27:1-66

Yesu Aletwa Mbele Ya Pilato

(Marko 15:1; Luka 23:1-2; Yohana 18:28-32)

127:1 Mk 15:1; Lk 22:66Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri pamoja dhidi ya Yesu ili kumuua. 227:2 Mt 20:19; Mdo 3:13; 1Tim 6:13Wakamfunga, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato, ambaye alikuwa mtawala wa Kirumi.

Yuda Ajinyonga

(Matendo 1:18-19)

327:3 Mt 10:4; 26:14-15Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti Yesu, alipoona kuwa Yesu amehukumiwa, akajuta na akarudisha vile vipande thelathini vya fedha alivyopewa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. 427:4 Mt 27:24Akasema, “Nimetenda dhambi, kwa maana nimeisaliti damu isiyo na hatia.”

Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”

527:5 Lk 1:9, 21; Mdo 1:18-19Basi Yuda akavitupa vile vipande vya fedha ndani ya Hekalu akaondoka akaenda kujinyonga.

627:6 Mk 12:41Wale viongozi wa makuhani wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.” 7Kwa hiyo baada ya kushauriana, waliamua kuzitumia kununulia shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni. 827:8 Mdo 1:19Hii ndiyo sababu lile shamba likaitwa Shamba la Damu hadi leo. 927:9 Mt 1:22Ndipo likatimia lile lililonenwa na nabii Yeremia, kwamba, “Walichukua vile vipande thelathini vya fedha, thamani aliyopangiwa na watu wa Israeli, 1027:10 Zek 11:12-13; Yer 32:6-9wakanunulia shamba la mfinyanzi, kama vile Bwana alivyoniagiza.”

Yesu Mbele Ya Pilato

(Marko 15:2-15; Luka 23:3-25; Yohana 18:33–19:16)

1127:11 Mt 2:2Wakati huo Yesu akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamuuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”

Yesu akasema, “Wewe wasema hivyo.”

1227:12 Mk 14:61; Yn 19:9Lakini viongozi wa makuhani na wazee walipomshtaki, hakujibu neno. 1327:13 Mt 26:62Ndipo Pilato akamuuliza, “Je, husikii ni mambo mangapi wanayokushtaki nayo?” 1427:14 Mk 14:61Lakini Yesu hakumjibu hata kwa shtaka moja, kiasi kwamba mtawala alishangaa sana.

1527:15 Yn 18:39Basi ilikuwa ni desturi ya mtawala kumfungua mfungwa mmoja aliyechaguliwa na umati wa watu wakati wa sikukuu. 16Wakati huo alikuwepo mfungwa mmoja mwenye sifa mbaya, aliyeitwa Baraba. 1727:17 Mt 1:16Hivyo umati wa watu walipokusanyika, Pilato akawauliza, “Mnataka niwafungulie nani, Baraba au Yesu yeye aitwaye Kristo?” 1827:18 Yn 11:47, 48; 12:19Kwa kuwa alitambua Yesu alikuwa amekabidhiwa kwake kwa ajili ya wivu.

1927:19 Yn 19:13; Mt 27:24; Hes 12:6Pilato akiwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mkewe akampelekea ujumbe huu: “Usiwe na jambo lolote juu ya mtu huyu asiye na hatia, kwa kuwa leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake.”

2027:20 Mdo 3:14Lakini viongozi wa makuhani na wazee wakaushawishi ule umati wa watu kwamba waombe Baraba afunguliwe, naye Yesu auawe.

21Mtawala akawauliza tena, “Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka niwafungulie?”

Wakajibu, “Baraba.”

2227:22 Mt 1:16Pilato akawaambia, “Basi nifanye nini na huyu Yesu aitwaye Kristo?”

Wakajibu wote, “Msulubishe!”

23Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?”

Lakini wao wakazidi kupiga kelele, wakisema, “Msulubishe!”

2427:24 Mt 26:5; Za 26:6; Kum 21:6-8Pilato alipoona kwamba hawezi kufanya lolote, lakini badala yake ghasia zilikuwa zinaanza, akachukua maji, akanawa mikono yake mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Sina hatia juu ya damu ya mtu huyu, hili ni jukumu lenu!”

2527:25 Yos 2:19; Mdo 5:28Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”

2627:26 Isa 53:5; Yn 19:1Basi akawafungulia Baraba. Lakini baada ya kuamuru Yesu achapwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe.

Askari Wamdhihaki Yesu

(Marko 15:16-20; Yohana 19:2-3)

2727:27 Yn 18:28-33; 19:9Kisha askari wa mtawala wakampeleka Yesu kwenye Praitorio27:27 Praitorio maana yake ni makao makuu ya mtawala, jumba la kifalme lililokuwa linakaliwa na Pontio Pilato huko Yerusalemu, palipokuwa na kiti cha hukumu. na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka. 2827:28 Yn 19:2Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha 2927:29 Isa 53:3; Yn 19:2-3wakasokota taji ya miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!” 3027:30 Mt 16:21; 26:27; 27:31; Isa 53:7Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena. 3127:31 Mk 15:20-41; Lk 23:26Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka ili wakamsulubishe.

Yesu Asulubishwa

(Marko 15:21-32; Luka 23:26-43; Yohana 19:17-27)

3227:32 Ebr 13:12; Mdo 11:20; Mk 15:21; Lk 23:26Walipokuwa wakienda, wakakutana na mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. 3327:33 Yn 19:17Wakafika mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). 3427:34 Mt 27:18; Za 69:21Hapo wakampa Yesu divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini alipoionja, akakataa kuinywa. 3527:35 Za 22:18Walipokwisha kumsulubisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura. [Hili lilifanyika ili litimie lile neno lililonenwa na nabii, “Waligawa nguo zangu miongoni mwao na vazi langu wakalipigia kura.”] 3627:36 Mt 27:54Kisha wakaketi, wakamchunga. 3727:37 Mk 15:26; Lk 23:38; Yn 19:19Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake hivi: Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi. 3827:38 Isa 53:12Wanyangʼanyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wa kushoto. 3927:39 Za 109:25; Mao 2:15Watu waliokuwa wakipita njiani wakamtukana huku wakitikisa vichwa vyao 4027:40 Mt 26:61; Yn 2:19; Mt 4:3-6na kusema, “Wewe ambaye utalivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe mwenyewe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu, shuka kutoka msalabani.”

41Vivyo hivyo, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamdhihaki wakisema, 4227:42 Yn 1:49; 12:13; 3:15“Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! Yeye ni Mfalme wa Israeli! Ashuke sasa kutoka msalabani, nasi tutamwamini. 4327:43 Za 22:8Anamwamini Mungu, basi Mungu na amwokoe sasa kama anamtaka, kwa maana alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’ ” 4427:44 Mk 15:32; Lk 23:39Hata wale wanyangʼanyi waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana vivyo hivyo.

Kifo Cha Yesu

(Marko 15:33-41; Luka 23:44-49; Yohana 19:28-30)

4527:45 Amo 8:9Tangu saa sita hadi saa tisa giza liliifunika nchi yote. 4627:46 Za 22:1Ilipofika saa tisa, Yesu akapaza sauti akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”)

47Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama pale waliposikia hayo, wakasema, “Anamwita Eliya.”

4827:48 Mt 27:34; Za 69:21Ghafula mmoja wao akaenda mbio na kuleta sifongo, akaichovya kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Yesu ili anywe. 49Wengine wakasema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Eliya atakuja kumwokoa.”

5027:50 Yn 19:30Yesu alipolia tena kwa sauti kuu, akaitoa roho yake.

5127:51 Kut 26:31-33; Ebr 10:19Wakati huo huo pazia la Hekalu likachanika vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. 52Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliokuwa wamekufa ikafufuliwa. 5327:53 Mt 4:5Wakatoka makaburini, na baada ya Yesu kufufuka, waliingia kwenye Mji Mtakatifu na kuwatokea watu wengi.

5427:54 Mt 4:3; 17:5Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, waliogopa, wakasema, “Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”

5527:55 Lk 8:2-3Walikuwako wanawake huko wakiangalia kwa mbali. Hawa walikuwa wamemfuata Yesu tangu Galilaya ili kushughulikia mahitaji yake. 5627:56 Lk 24:10; Yn 19:25Miongoni mwao walikuwepo Maria Magdalene, na Maria mama yao Yakobo na Yosefu, na mama yao wana wa Zebedayo.

Maziko Ya Yesu

(Marko 15:42-47; Luka 23:50-56; Yohana 19:38-42)

5727:57 Kut 34:25; Mk 15:42; Lk 23:50; Yn 19:38Ilipofika jioni, alifika mtu mmoja tajiri kutoka Arimathaya aitwaye Yosefu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58Akamwendea Pilato ili kumwomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. 59Yosefu akauchukua mwili wa Yesu, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, 6027:60 Mk 16:4; Mdo 13:29na kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake. 61Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwepo mahali pale, wakiwa wameketi mkabala na kaburi.

Walinzi Pale Kaburini

62Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalizi ya Sabato, viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakamwendea Pilato 6327:63 Mt 16:21na kusema, “Bwana, tumekumbuka kwamba yule mdanganyifu wakati alikuwa bado hai alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ 6427:64 Mt 28:13Kwa hiyo uamuru kaburi lilindwe kwa uthabiti mpaka baada ya siku tatu. La sivyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kuuiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuliwa kutoka kwa wafu. Udanganyifu huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.”

6527:65 Mt 28:11Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari walinzi. Nendeni, liwekeeni ulinzi kadri mwezavyo.” 6627:66 Dan 6:7; Mt 28:2; 28:11Kwa hiyo wakaenda na walinzi ili kulilinda kaburi kwa uthabiti, wakatia muhuri kwenye lile jiwe na kuweka ulinzi.