Mathayo 21 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mathayo 21:1-46

Yesu Anaingia Yerusalemu Kwa Shangwe

(Marko 11:1-11; Luka 19:28-40; Yohana 12:12-19)

121:1 Yn 8:1; Mdo 1:12Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika Mlima wa Mizeituni. Ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili, 2akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu, nanyi mtamkuta punda amefungwa hapo, na mwana-punda pamoja naye. Wafungueni na mniletee. 321:3 Mt 26:18Kama mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara.”

421:4 Mt 1:22Haya yalitukia ili litimie lile lililonenwa na nabii, akisema:

521:5 Zek 9:9; Isa 62:11“Mwambieni Binti Sayuni,

‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako,

ni mnyenyekevu, naye amepanda punda,

juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’ ”

621:6 Mk 11:4Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyokuwa amewaagiza. 721:7 1Fal 9:13Wakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda, naye Yesu akaketi juu yake. 821:8 2Fal 9:3Umati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti, wakayatandaza barabarani. 921:9 Mt 9:27; Za 118:26; Mt 23:29; Lk 2:14Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema,

“Hosana,21:9 Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe. Mwana wa Daudi!”

“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”

“Hosana juu mbinguni!”

1021:10 Mk 11:15; Lk 19:45; Yn 2:13, 15Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?”

1121:11 Kum 18:15; Yn 1:21Ule umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”

Yesu Atakasa Hekalu

(Marko 11:15-19; Luka 19:45-48; Yohana 2:13-22)

1221:12 Kum 14:26; Kut 30:13; Law 1:14Yesu akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 1321:13 Isa 56:7; Yer 7:11Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi.”

1421:14 Mt 4:23Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya. 1521:15 Mt 9:27; Lk 19:39Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika.

1621:16 Za 8:2Wakamuuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?”

Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma,

“ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao

umeamuru sifa’?”

1721:17 Lk 24:50; Yn 11:18Akawaacha, akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko.

Mtini Wanyauka

(Marko 11:12-14, 20-24)

1821:18 Mk 11:12Asubuhi na mapema, Yesu alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa. 1921:19 Isa 34:4; Yer 8:13Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka.

2021:20 Mk 11:20Wanafunzi wake walipoona jambo hili, wakashangaa, wakamuuliza, “Imekuwaje mtini huu kunyauka ghafula?”

2121:21 1Kor 13:2; Yak 1:6Yesu akawajibu, “Amin, nawaambia, kama mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata mkiuambia huu mlima, ‘Ngʼoka, ukatupwe baharini,’ litafanyika. 2221:22 Mt 7:7Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea.”

Wahoji Kuhusu Mamlaka Ya Yesu

(Marko 11:27-33; Luka 20:1-8)

2321:23 Mdo 4:7; 7:27Yesu alipoingia Hekaluni, viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakamjia alipokuwa anafundisha na kusema, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Na ni nani aliyekupa mamlaka hayo?”

24Yesu akawajibu, “Nami nitawauliza swali moja. Kama mkinijibu, nami nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 25Ubatizo wa Yohana, ulitoka wapi? Je, ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?”

Wakahojiana wao kwa wao na kusema, “Tukisema ulitoka mbinguni atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’ 2621:26 Mt 11:9; Mk 6:20Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ tunawaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yohana kuwa ni nabii.”

27Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Sisi hatujui.”

Naye akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”

Mfano Wa Wana Wawili

2821:28 Mt 21:33; 20:1“Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Akamwendea yule wa kwanza akamwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’

2921:29 Mt 7:21“Yule mwanawe akamjibu ‘Mimi sitakwenda.’ Baadaye akabadili mawazo yake akaenda.

30“Kisha yule baba akamwendea yule mwanawe mwingine akamwambia vilevile. Yeye akajibu, ‘Nitakwenda, bwana,’ lakini hakwenda.

3121:31 Lk 7:29; 7:50“Ni yupi kati yao hao wawili aliyetimiza kile alichotaka baba yake?”

Wakamjibu, “Ni yule wa kwanza.”

Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika Ufalme wa Mungu. 3221:32 Mt 3:1-12; Lk 3:12-13; 7:29-30; 7:36-50Kwa maana Yohana alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumsadiki, lakini watoza ushuru na makahaba wakamsadiki. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kumsadiki.

Mfano Wa Wapangaji Waovu

(Marko 12:1-12; Luka 20:9-19)

3321:33 Za 80:8; Isa 5:1-7; Mt 25:14-25“Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu mmoja mwenye shamba ambaye alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akatengeneza shinikizo ndani yake na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha hilo shamba la mizabibu kwa wakulima fulani, naye akaondoka, akasafiri kwenda nchi nyingine. 3421:34 Mt 22:3Wakati wa mavuno ulipokaribia, akawatuma watumishi wake kwa hao wapangaji ili kukusanya matunda yake.

3521:35 2Nya 24:1; Ebr 11:36-37“Wale wapangaji wakawakamata wale watumishi, wakampiga mmoja, wakamuua mwingine, na yule wa tatu wakampiga mawe. 3621:36 Mt 22:4Kisha akawatuma kwao watumishi wengine, wengi kuliko wale wa kwanza, nao wale wapangaji wakawatendea vilevile. 37Mwisho wa yote, akamtuma mwanawe kwao, akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’

3821:38 Ebr 1:2; Mt 12:14; Za 2:8“Lakini wale wapangaji walipomwona mwanawe, wakasemezana wao kwa wao, ‘Huyu ndiye mrithi. Njooni tumuue, ili tuchukue urithi wake.’ 3921:39 Mt 26:50; Mk 14:46; Lk 22:54; Yn 18:12; Mdo 2:32Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua.

40“Kwa hiyo, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyia nini hao wakulima?”

4121:41 Mt 8:11-12; Mdo 18:6; 28:28Wakamjibu, “Kwa huzuni kuu atawaangamiza kabisa hao wadhalimu na kulipangisha shamba lake la mizabibu kwa wakulima wengine ambao watampatia fungu lake la matunda wakati wa mavuno.”

4221:42 Za 118:22-23; 1Pet 2:7Yesu akawaambia, “Je, hamjasoma katika Maandiko kwamba:

“ ‘Jiwe walilolikataa waashi

limekuwa jiwe kuu la pembeni.

Bwana ndiye alitenda jambo hili,

nalo ni la ajabu machoni petu’?

4321:43 Mt 8:12“Kwa hiyo ninawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa watu wengine wawezao kuzaa matunda yake. 4421:44 Lk 2:34Yeye aangukaye juu ya jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.”

45Viongozi wa Makuhani na Mafarisayo waliposikia mifano ya Yesu, walitambua kuwa alikuwa akiwasema wao. 4621:46 Mt 21:11, 26Wakatafuta njia ya kumkamata, lakini wakaogopa umati wa watu, kwa kuwa watu walimwona Yesu kuwa ni nabii.