Mathayo 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mathayo 13:1-58

Mfano Wa Mpanzi

(Marko 4:1-9; Luka 8:4-8)

113:1 Mt 13:36; 9:28Siku iyo hiyo Yesu akatoka nje ya nyumba, akaketi kando ya bahari. 213:2 Lk 5:3Umati mkubwa mno wa watu ukakusanyika kumzunguka, hata ikabidi aingie katika chombo na kuketi humo, nao watu wote wakawa wamesimama ukingoni mwa bahari. 313:3 Lk 8:5Ndipo akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema: “Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. 4Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. 5Nyingine zilianguka kwenye ardhi yenye mwamba isiyo na udongo wa kutosha. Zikaota haraka, kwa kuwa udongo ulikuwa haba. 6Lakini jua lilipozidi, mimea ikanyauka na kukauka kwa kuwa mizizi yake haikuwa na kina. 7Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo miiba hiyo ikakua, ikaisonga hiyo mimea. 813:8 Mwa 26:12Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri ambapo zilitoa mazao, nyingine mara mia moja, nyingine mara sitini, na nyingine mara thelathini. 913:9 Mt 11:15Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”

Sababu Ya Kufundisha Kwa Mifano

(Marko 4:10-12; Luka 8:9-10)

10Wanafunzi wake wakamwendea, wakamuuliza, “Kwa nini unasema na watu kwa mifano?”

1113:11 Kol 1:27; 1Yn 2:20, 27Akawajibu, “Ninyi mmepewa kuzifahamu siri za Ufalme wa Mbinguni, lakini wao hawajapewa. 1213:12 Mt 25:29; Lk 19:26Kwa maana yule aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa. 1313:13 Yer 5:21; Eze 12:2Hii ndiyo sababu nasema nao kwa mifano:

“Ingawa wanatazama, hawaoni;

wanasikiliza, lakini hawasikii, wala hawaelewi.

1413:14 Mt 1:22; 13:35; Eze 12:2; Isa 6:9; Mdo 28:26-28Kwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema:

“ ‘Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa;

na pia mtatazama lakini hamtaona.

1513:15 Isa 6:9-10; Rum 11:8Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu;

hawasikii kwa masikio yao,

na wamefumba macho yao.

Wasije wakaona kwa macho yao,

na wakasikiliza kwa masikio yao,

wakaelewa kwa mioyo yao,

na kugeuka nami nikawaponya.’

1613:16 Mt 16:17; Lk 10:23-24Lakini heri macho yenu kwa sababu yanaona, na heri masikio yenu kwa sababu yanasikia. 1713:17 Ebr 11:13; 1Pet 1:10-12Amin, nawaambia, manabii wengi na wenye haki walitamani kuona yale mnayoyaona lakini hawakuyaona, na walitamani kusikia yale mnayoyasikia lakini hawakuyasikia.

Maelezo Ya Mfano Wa Mbegu

(Marko 4:13-20; Luka 8:11-15)

1813:18 Mk 4:14; Lk 8:11“Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi: 1913:19 Mt 4:23; 5:37Mtu yeyote anaposikia neno la Ufalme naye asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake. Hii ndiyo ile mbegu iliyopandwa kando ya njia. 2013:20 Isa 58:2; Eze 33:31, 32; Yn 5:35Ile mbegu iliyopandwa kwenye sehemu yenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na mara hulipokea kwa furaha. 2113:21 Mt 11:6; 26:31Lakini kwa kuwa hana mizizi yenye kina ndani yake, lile neno hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, yeye mara huchukizwa. 2213:22 Mt 19:23; 1Tim 6:9-10, 17Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno, lakini masumbufu ya maisha haya na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda. 2313:23 Mt 13:8Lakini ile mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu ambaye hulisikia neno na kulielewa. Naye hakika huzaa matunda, akizaa mara mia, au mara sitini, au mara thelathini ya mbegu iliyopandwa.”

Mfano Wa Magugu

2413:24 Mt 25:1; Mk 4:26-39Yesu akawaambia mfano mwingine, akasema: “Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. 25Lakini wakati kila mtu alipokuwa amelala, adui yake akaja na kupanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. 26Ngano ilipoota na kutoa masuke, magugu nayo yakatokea.

27“Watumishi wa yule mwenye shamba wakamjia na kumwambia, ‘Bwana, si tulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Basi, magugu yametoka wapi?’

28“Akawajibu, ‘Adui ndiye alifanya jambo hili.’

“Wale watumishi wakamuuliza, ‘Je, unataka twende tukayangʼoe?’

29“Lakini akasema, ‘Hapana, msiyangʼoe, kwa maana wakati mkingʼoa magugu mnaweza mkangʼoa na ngano pamoja nayo. 3013:30 Mt 3:12Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto; kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.’ ”

Mfano Wa Mbegu Ya Haradali

(Marko 4:30-32; Luka 13:18-19)

3113:31 Mt 17:20; Lk 17:6Akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa Mbinguni ni kama punje ya haradali, ambayo mtu aliichukua, akaipanda shambani mwake. 3213:32 Za 104:12; Dan 4:12Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hadi ndege wa angani wanakuja na kutengeneza viota katika matawi yake.”

Mfano Wa Chachu

(Luka 13:20-21)

3313:33 Mt 13:24; Mwa 18:6; Gal 5:9Akawaambia mfano mwingine, “Ufalme wa Mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga mpaka wote ukaumuka.”

Sababu Ya Yesu Kutumia Mifano

(Marko 4:33-34)

3413:34 Mk 4:33-34Yesu alinena mambo haya yote kwa makutano kwa mifano. Wala hakuwaambia lolote pasipo mfano. 3513:35 Za 78:2; 1Kor 2:7Hii ilikuwa ili kutimiza lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii aliposema:

“Nitafungua kinywa changu niseme nao kwa mifano;

nitahubiri mambo yaliyofichika

tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.”

Ufafanuzi Wa Mfano Wa Magugu

3613:36 Mt 15:15; 13:24-30Kisha Yesu akaagana na makutano, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamjia wakamwambia, “Tueleze maana ya ule mfano wa magugu shambani.”

3713:37 Mt 8:20Akawaambia, “Aliyepanda mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu. 3813:38 Yn 8:44-45; 1Yn 3:10Shamba ni ulimwengu na mbegu nzuri ni wana wa Ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu. 3913:39 Yoe 3:13; Mt 24:3; 28:20; Ufu 14:15Yule adui aliyepanda magugu ni ibilisi. Mavuno ni mwisho wa dunia, nao wavunaji ni malaika.

4013:40 Yn 15:6“Kama vile magugu yangʼolewavyo na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. 4113:41 Mt 8:20; 24:31Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote. 4213:42 Mt 13:50; 8:12Nao watawatupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 4313:43 Dan 12:3; Mt 11:15Ndipo wenye haki watangʼaa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio, na asikie.

Mfano Wa Hazina Iliyofichwa Na Lulu

4413:44 Mt 13:24; Isa 55:1; Flp 3:7-8“Ufalme wa Mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba.”

4513:45 Mt 13:24“Tena, Ufalme wa Mbinguni unafanana na mfanyabiashara aliyekuwa akitafuta lulu safi. 4613:46 Mt 2:4; 3:14, 15; 8:10, 19Alipoipata lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza vyote alivyokuwa navyo akainunua.”

Mfano Wa Wavu

4713:47 Mt 13:24; 22:9-10“Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama wavu wa kuvua samaki uliotupwa baharini ukavua samaki wa kila aina. 48Ulipojaa, wavuvi wakavuta pwani, wakaketi na kukusanya samaki wazuri kuwaweka kwenye vyombo safi, lakini wale samaki wabaya wakawatupa. 4913:49 Mt 25:32Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki. 5013:50 Mt 8:12Nao watawatupa hao waovu katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.”

51Yesu akauliza, “Je, mmeyaelewa haya yote?”

Wakamjibu, “Ndiyo.”

5213:52 Wim 7:13Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa sheria aliyefundishwa elimu ya Ufalme wa Mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka ghala yake mali mpya na mali ya zamani.”

Yesu Akataliwa Nazareti

(Marko 6:1-6; Luka 4:16-30)

5313:53 Mt 7:28Yesu alipomaliza kutoa mifano hii, akaondoka. 5413:54 Mt 4:23; 7:28Alipofika mji wa kwao, akawafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza?” 5513:55 Lk 3:23; Yn 6:42; Mt 12:46“Huyu si yule mwana wa seremala? Mama yake si yeye aitwaye Maria, nao ndugu zake si Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 5613:56 Yn 7:15, 52Nao dada zake wote, hawako hapa pamoja nasi? Mtu huyu amepata wapi basi mambo haya yote?” 5713:57 Yn 6:61; Lk 4:24; Yn 4:44Wakachukizwa naye.

Lakini Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani kwake.”

5813:58 Mk 6:5, 6Naye hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao.