Matendo 6 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Matendo 6:1-15

Mateso Na Kuenea Kwa Injili

(6:1–9:31)

Saba Wachaguliwa Kuhudumu

16:1 Mdo 2:21; 4:35; 9:29, 39-41; 1Tim 5:3Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, palitokea manungʼuniko kati ya Wayahudi wa Kiyunani, dhidi ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawanyo wa chakula wa kila siku. 26:2 Mdo 11:26; Ebr 4:12; Kut 18:17Wale mitume kumi na wawili wakakusanya wanafunzi wote pamoja wakasema, “Haitakuwa vyema sisi kuacha huduma ya neno la Mungu ili kuhudumu mezani. 36:3 Mdo 1:14-16; Lk 1:15; Kut 18:21; Neh 13:13; 1Tim 3:7, 8Kwa hiyo ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, watu wenye sifa njema, waliojawa na Roho Mtakatifu na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi kazi hii, 46:4 Mdo 2:42nasi tutatumia muda wetu kuomba na huduma ya neno.”

56:5 Mdo 11:19; 22:20; 8:5-40; 21:8; Lk 1:15Yale waliyosema yakawapendeza watu wote, nao wakamchagua Stefano (mtu aliyejawa na imani na Roho Mtakatifu) pamoja na Filipo, Prokoro, Nikanori, Timoni, Parmena na Nikolao, mwongofu kutoka Antiokia. 66:6 Mdo 13:3; 2Tim 1:6; Hes 27; 18; Mk 5:23Wakawaleta watu hawa mbele ya mitume, nao wakawaombea na kuwawekea mikono juu yao.

76:7 Mdo 12:24; 19:20Neno la Mungu likazidi kuenea. Idadi ya wanafunzi ikazidi kuongezeka sana katika Yerusalemu hata makuhani wengi wakaitii ile imani.

Kukamatwa Kwa Stefano

86:8 Yn 4:48Stefano, akiwa amejaa neema na nguvu za Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa miongoni mwa watu. 96:9 Mt 27:32; 22:3; 23:34; 2:9Hata hivyo, ukainuka upinzani wa watu wa Sinagogi la Watu Huru (kama lilivyokuwa linaitwa), la Wayahudi wa Kirene na wa Iskanderia, na wengine kutoka Kilikia na Asia. Watu hawa wakaanza kupingana na Stefano. 106:10 Lk 21:15; Mdo 5:39Lakini hawakuweza kushindana na hekima yake wala huyo Roho ambaye alisema kwake.

116:11 2Fal 21:10; Mt 26:59-61Ndipo kwa siri wakawashawishi watu fulani waseme, “Tumemsikia Stefano akisema maneno ya kufuru dhidi ya Mose na dhidi ya Mungu.”

Stefano Afikishwa Mbele Ya Baraza

126:12 Mt 5:22Wakawachochea watu, wazee na walimu wa Sheria, nao wakamkamata Stefano wakamfikisha mbele ya baraza. 136:13 Mt 24:15; Mdo 7:48Wakaweka mashahidi wa uongo ambao walishuhudia wakisema, “Mtu huyu kamwe haachi kusema dhidi ya mahali hapa patakatifu na dhidi ya Sheria. 146:14 Mdo 26:3; 28:17Kwa maana tumemsikia akisema kwamba Yesu wa Nazareti atapaharibu mahali patakatifu na kubadili desturi zote tulizopewa na Mose.”

156:15 Mt 5:22Watu wote waliokuwa wameketi katika baraza wakimkazia macho Stefano, wakaona uso wake unangʼaa kama uso wa malaika.