Matendo 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Matendo 2:1-47

Kushuka Kwa Roho Mtakatifu

12:1 Law 23:15-16; 1Kor 16:18; Mdo 1:14Siku ya Pentekoste ilipowadia, waamini wote walikuwa mahali pamoja. 22:2 Mdo 4:31Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 32:3 Mt 3:11Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. 42:4 Mk 16:17; 1Kor 12:10Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.

52:5 Lk 2:25; Mdo 8:2Basi walikuwepo Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka kila taifa chini ya mbingu. 6Waliposikia sauti hii, umati wa watu ulikusanyika pamoja wakistaajabu, kwa sababu kila mmoja wao aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. 72:7 Mdo 1:11Wakiwa wameshangaa na kustaajabu wakauliza, “Je, hawa wote wanaozungumza si Wagalilaya? 8Imekuwaje basi kila mmoja wetu anawasikia wakinena kwa lugha yake ya kuzaliwa? 92:9 Mdo 18:2; 1Pet 1:1; 2Kor 1:8; Ufu 1:4Wapathi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Uyahudi, Kapadokia, Ponto na Asia, 102:10 Mdo 16:6; 18:23; 14:24; Mt 27:32Frigia, Pamfilia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene na wageni kutoka Rumi, 11Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, sote tunawasikia watu hawa wakisema mambo makuu ya ajabu ya Mungu katika lugha zetu wenyewe.” 12Wakiwa wameshangaa na kufadhaika wakaulizana, “Ni nini maana ya mambo haya?”

132:13 1Kor 14:23; Efe 5:18Lakini wengine wakawadhihaki wakasema, “Hawa wamelewa divai!”

Petro Ahutubia Umati

14Ndipo Petro akasimama pamoja na wale mitume kumi na mmoja, akainua sauti yake na kuhutubia ule umati wa watu, akasema: “Wayahudi wenzangu na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, jueni jambo hili mkanisikilize. 152:15 1The 5:7Hakika watu hawa hawakulewa kama mnavyodhania, kwa kuwa sasa ni saa tatu asubuhi! 162:16 Yoe 2:28-32La, hili ni jambo lililotabiriwa na nabii Yoeli, akisema:

172:17 Eze 39:29; Yn 7:37-39; Mdo 21:9“ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu,

nitamimina Roho wangu

juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu na binti zenu watatabiri,

vijana wenu wataona maono,

na wazee wenu wataota ndoto.

182:18 Mdo 21:9-12; 1Kor 12:10, 28; 14:1Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,

katika siku zile nitamimina Roho wangu,

nao watatabiri.

192:19 Yoe 2:30, 31; Lk 21:11Nami nitaonyesha maajabu juu mbinguni,

na ishara chini duniani:

damu, moto, na mawimbi ya moshi.

202:20 Mt 24:29Jua litakuwa giza

na mwezi utakuwa mwekundu kama damu,

kabla ya kuja siku ile kuu ya Bwana

iliyo tukufu.

212:21 Yoe 2:28-32; Rum 10:13Na kila mtu atakayeliitia

jina la Bwana, ataokolewa.’

222:22 Yn 4:48; Mdo 10:38; Yn 3:2“Enyi Waisraeli, sikilizeni maneno haya nisemayo: Yesu wa Nazareti alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambayo Mungu alitenda miongoni mwenu kupitia kwake, kama ninyi wenyewe mjuavyo. 232:23 Isa 53:10; Lk 22:22; 24:20; Mt 16:21Huyu mtu akiisha kutolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa kwa kujua kwake Mungu tangu zamani, ninyi, kwa mikono ya watu wabaya, mlimuua kwa kumgongomea msalabani. 242:24 Rum 8:11; Ebr 13:20; Yn 20:9Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu akamwondolea uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana yeye kushikiliwa na nguvu za mauti. 252:25 Za 16:8Kwa maana Daudi asema kumhusu yeye:

“ ‘Nalimwona Bwana mbele yangu daima.

Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,

sitatikisika.

26Kwa hiyo moyo wangu unafurahia,

na ulimi wangu unashangilia;

mwili wangu nao utapumzika kwa tumaini.

272:27 Mdo 13:35Kwa maana hutaniacha kaburini,

wala hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.

282:28 Za 16:8-11Umenionyesha njia za uzima,

utanijaza na furaha mbele zako.’

292:29 Mdo 7:8-9; 1Fal 2:10; Neh 3:16“Ndugu zangu Waisraeli, nataka niwaambie kwa uhakika kwamba baba yetu Daudi alikufa na kuzikwa, nalo kaburi lake lipo hapa mpaka leo. 302:30 2Sam 7:12; Mt 1:1; Za 132:11; Lk 1:32, 69; Rum 1:3; 2Tim 2:8Lakini alikuwa nabii na alijua ya kuwa Mungu alikuwa amemwahidi kwa kiapo kwamba angemweka mmoja wa wazao wake penye kiti chake cha enzi. 312:31 Za 16:10; Mdo 13:35Daudi, akiona mambo yaliyoko mbele, akanena juu ya kufufuka kwa Kristo,2:31 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. kwamba hakuachwa kaburini, wala mwili wake haukuona uharibifu. 322:32 Mdo 1:8; 2:24; Lk 24:48Mungu alimfufua huyu Yesu na sisi sote ni mashahidi wa jambo hilo. 332:33 Flp 2:9; Mk 16:19; Yn 14:26; Mdo 10:45; Yn 15:26Basi ikiwa yeye ametukuzwa kwa mkono wa kuume wa Mungu, amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho Mtakatifu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia. 342:34 Za 110:1; Mt 22:44; 1Kor 15:25; Efe 1:20; Ebr 1:13Kwa kuwa Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini anasema,

“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:

“Keti mkono wangu wa kuume,

352:35 Za 110:1; Mt 22:44hadi nitakapowaweka adui zako

chini ya miguu yako.” ’

362:36 Lk 2:11; Mdo 5:31; Mt 28:18“Kwa hiyo Israeli wote na wajue jambo hili kwa uhakika kwamba: Mungu amemfanya huyu Yesu, ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa Bwana na Kristo.”

Waumini Waongezeka

372:37 Lk 3:10-14; Mdo 16:30Watu waliposikia maneno haya yakawachoma mioyo yao, wakawauliza Petro na wale mitume wengine, “Ndugu zetu tufanye nini?”

382:38 Mdo 22:16; Kol 2:12; Yer 36:3Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 392:39 Isa 44:3; 66:23; 57:19; Efe 2:13Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu, na kwa wote walio mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita amjie.”

402:40 Kum 32:5; Flp 2:15Petro akawaonya kwa maneno mengine mengi na kuwasihi akisema, “Jiepusheni na kizazi hiki kilichopotoka.” 412:41 Mdo 2:47; 4:4; 5:14; 9:31, 35, 42; 11:21, 24; 14:1, 21Wale wote waliopokea ujumbe wa Petro kwa furaha wakabatizwa na siku ile waliongezeka watu wapatao 3,000.

Ushirika Wa Waumini

422:42 Mdo 1:14Nao wakawa wanadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali. 432:43 Mdo 5:12Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume. 442:44 Mdo 4:32Walioamini wote walikuwa mahali pamoja, nao walikuwa na kila kitu shirika. 452:45 Mt 19:21; Lk 12:33Waliuza mali zao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake. 462:46 Lk 24:53; Mdo 3:1; 20:7; Mt 14:19Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe, 472:47 Rum 14:18; Mdo 5:14wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kanisa wale waliokuwa wakiokolewa.