Marko 9 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version

Marko 9:1-50

19:1 Mk 13:30; Lk 22:18; Mt 24:30; 25:30Yesu akaendelea kuwaambia, “Amin, nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.”

Yesu Ageuka Sura

(Mathayo 17:1-13; Luka 9:28-36)

29:2 Mt 4:21Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. 39:3 Mt 28:3Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. 4Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu.

59:5 Mt 23:7Petro akamwambia Yesu, “Rabi, ni vyema sisi tukae hapa. Turuhusu tujenge vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya.” 6Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana.

79:7 Kut 24:16; Mt 3:17Ndipo pakatokea wingu, likawafunika, nayo sauti kutoka lile wingu ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Msikieni yeye.”

8Mara walipotazama huku na huku, hawakuona tena mtu mwingine yeyote pamoja nao isipokuwa Yesu.

99:9 Mk 8:20-30Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Yesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote mambo waliyoona, mpaka Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka kutoka kwa wafu. 10Wakalihifadhi jambo hilo wao wenyewe, lakini wakawa wanajiuliza, “Huku kufufuka kwa wafu maana yake nini?”

119:11 Mal 4:5; Mt 17:10Wakamuuliza, “Kwa nini walimu wa sheria husema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza?”

129:12 Mt 8:20; 16:21; Lk 13:11Yesu akawajibu, “Ni kweli, Eliya yuaja kwanza ili kutengeneza mambo yote. Mbona basi imeandikwa kwamba Mwana wa Adamu ni lazima ateseke sana na kudharauliwa? 139:13 Mt 11:14Lakini ninawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtendea walivyopenda, kama ilivyoandikwa kumhusu yeye.”

Mvulana Mwenye Pepo Mchafu Aponywa

(Mathayo 17:14-21; Luka 9:37-43)

149:14 Mt 17:14; Lk 9:37; 9:1-20; Mt 17:14-21Walipowafikia wale wanafunzi wengine, wakawakuta wamezungukwa na umati mkubwa wa watu na baadhi ya walimu wa sheria wakibishana nao. 15Mara wale watu walipomwona Yesu, wakastaajabu sana, wakamkimbilia ili kumsalimu.

16Akawauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao kuhusu nini?”

179:17 Mt 17:14; Lk 9:38Mtu mmoja miongoni mwa ule umati wa watu akajibu, “Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea. 18Kila mara huyo pepo mchafu ampagaapo mwanangu, humwangusha chini na kumfanya atokwe povu mdomoni na kusaga meno, kisha mwili wake hukauka. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.”

19Yesu akawaambia, “Enyi kizazi kisicho na imani! Nitakuwa pamoja nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni mvulana kwangu.”

209:20 Mk 1:26Nao wakamleta yule mvulana. Yule pepo mchafu alipomwona Yesu, mara akamtia yule mvulana kifafa, akaanguka, akagaagaa chini huku akitokwa na povu kinywani.

21Yesu akamuuliza baba yake, “Mwanao amekuwa katika hali hii tangu lini?”

Akamjibu, “Tangu utoto wake. 22Mara kwa mara huyo pepo mchafu amekuwa akimwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kumwangamiza. Lakini kama unaweza kufanya jambo lolote, tafadhali tuhurumie utusaidie.”

239:23 Mt 21:21; Yn 11:40Yesu akamwambia, “Kama ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye.”

249:24 Lk 17:5Mara baba yake yule mvulana akapiga kelele akisema, “Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!” 259:25 Mk 9:15; 1:26Yesu alipoona kwamba umati wa watu unakusanyika pamoja mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akimwambia, “Wewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru umtoke, wala usimwingie tena!”

26Yule pepo mchafu akiisha kupiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu, na akamtoka. Yule mvulana alikuwa kama maiti, hivyo watu wengi wakasema, “Amekufa.” 27Lakini Yesu akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama.

289:28 Mk 7:17; Mt 17:19Baada ya Yesu kuingia ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamuuliza wakiwa peke yao, “Mbona sisi hatukuweza kumtoa huyo pepo mchafu?”

29Yesu akawajibu, “Hali hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba na kufunga.”

Yesu Atabiri Tena Kifo Chake Na Ufufuo

(Mathayo 17:22-23; Luka 9:43-45)

309:30 Yn 7:1Wakaondoka huko, wakapitia Galilaya. Yesu hakutaka mtu yeyote afahamu mahali walipo, 319:31 Mt 8:20; Mdo 2:23; 3:13; Mt 16:21kwa maana alikuwa anawafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu. Nao watamuua, lakini siku tatu baada ya kuuawa atafufuka.” 329:32 Lk 18:34; Yn 12:16Lakini wao hawakuelewa kile alimaanisha, nao waliogopa kumuuliza maana yake.

Mabishano Kuhusu Aliye Mkuu Zaidi

(Mathayo 18:1-5; Luka 9:46-48)

339:33 Mt 4:13; Mk 1:29Basi wakafika Kapernaumu na baada ya kuingia nyumbani akawauliza, “Mlikuwa mnabishana nini kule njiani?” 349:34 Lk 22:24Lakini hawakumjibu, kwa sababu njiani walikuwa wakibishana kuhusu nani miongoni mwao alikuwa mkuu zaidi ya wote.

359:35 Mt 20:26; Lk 22:26Akaketi chini, akawaita wote kumi na wawili, akawaambia: “Kama mtu yeyote akitaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa wa mwisho na mtumishi wa wote.”

369:36 Mk 10:16Kisha akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao. Akamkumbatia, akawaambia, 379:37 Mt 10:40“Mtu yeyote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba yangu aliyenituma.”

Yeyote Asiye Kinyume Nasi Yuko Upande Wetu

(Luka 9:49-50)

389:38 Hes 11:27-29Yohana akamwambia, “Mwalimu, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamkataza, kwa sababu yeye si mmoja wetu.”

399:39 1Kor 12:3Yesu akasema, “Msimkataze, kwa kuwa hakuna yeyote atendaye miujiza kwa Jina langu ambaye baada ya kitambo kidogo aweza kunena lolote baya dhidi yangu. 409:40 Mt 12:30; Lk 11:23Kwa maana yeyote asiye kinyume chetu, yuko upande wetu. 419:41 Mt 10:42Amin, nawaambia, yeyote awapaye ninyi kikombe cha maji kwa Jina langu kwa sababu ninyi ni mali ya Kristo, hakika hataikosa thawabu yake.”

Kusababisha Kutenda Dhambi

(Mathayo 18:6-9; Luka 17:1-2)

429:42 Mt 5:29; 18:6; Lk 17:2“Kama mtu yeyote akimsababisha mmojawapo wa wadogo hawa wanaoniamini kutenda dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa baharini. 439:43 Mt 5:29-30; 18:8; 25:41Kama mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili lakini ukaingia jehanamu, mahali ambako moto hauzimiki. [ 449:44 Isa 66:24Mahali ambako funza wake hawafi wala moto wake hauzimiki.] 459:45 Mt 5:29; 18:8Kama mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili lakini ukaingia jehanamu. [ 46Mahali ambako funza wake hawafi wala moto hauzimiki.] 479:47 Mt 5:29; 18:9Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe. Ni afadhali kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa jehanamu, 489:48 Isa 66:24; Mt 25:41mahali ambako

“ ‘funza wake hawafi,

wala moto wake hauzimiki.’

499:49 Law 2:13Kila mmoja atatiwa chumvi kwa moto.

509:50 Mt 5:13; Lk 14:34-35; Kol 4:6; Rum 12:18; 1The 5:13“Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake utaifanyaje ili iweze kukolea tena? Mwe na chumvi ndani yenu, mkaishi kwa amani, kila mmoja na mwenzake.”

New International Version

Mark 9:1-50

1And he said to them, “Truly I tell you, some who are standing here will not taste death before they see that the kingdom of God has come with power.”

The Transfiguration

2After six days Jesus took Peter, James and John with him and led them up a high mountain, where they were all alone. There he was transfigured before them. 3His clothes became dazzling white, whiter than anyone in the world could bleach them. 4And there appeared before them Elijah and Moses, who were talking with Jesus.

5Peter said to Jesus, “Rabbi, it is good for us to be here. Let us put up three shelters—one for you, one for Moses and one for Elijah.” 6(He did not know what to say, they were so frightened.)

7Then a cloud appeared and covered them, and a voice came from the cloud: “This is my Son, whom I love. Listen to him!”

8Suddenly, when they looked around, they no longer saw anyone with them except Jesus.

9As they were coming down the mountain, Jesus gave them orders not to tell anyone what they had seen until the Son of Man had risen from the dead. 10They kept the matter to themselves, discussing what “rising from the dead” meant.

11And they asked him, “Why do the teachers of the law say that Elijah must come first?”

12Jesus replied, “To be sure, Elijah does come first, and restores all things. Why then is it written that the Son of Man must suffer much and be rejected? 13But I tell you, Elijah has come, and they have done to him everything they wished, just as it is written about him.”

Jesus Heals a Boy Possessed by an Impure Spirit

14When they came to the other disciples, they saw a large crowd around them and the teachers of the law arguing with them. 15As soon as all the people saw Jesus, they were overwhelmed with wonder and ran to greet him.

16“What are you arguing with them about?” he asked.

17A man in the crowd answered, “Teacher, I brought you my son, who is possessed by a spirit that has robbed him of speech. 18Whenever it seizes him, it throws him to the ground. He foams at the mouth, gnashes his teeth and becomes rigid. I asked your disciples to drive out the spirit, but they could not.”

19“You unbelieving generation,” Jesus replied, “how long shall I stay with you? How long shall I put up with you? Bring the boy to me.”

20So they brought him. When the spirit saw Jesus, it immediately threw the boy into a convulsion. He fell to the ground and rolled around, foaming at the mouth.

21Jesus asked the boy’s father, “How long has he been like this?”

“From childhood,” he answered. 22“It has often thrown him into fire or water to kill him. But if you can do anything, take pity on us and help us.”

23“ ‘If you can’?” said Jesus. “Everything is possible for one who believes.”

24Immediately the boy’s father exclaimed, “I do believe; help me overcome my unbelief!”

25When Jesus saw that a crowd was running to the scene, he rebuked the impure spirit. “You deaf and mute spirit,” he said, “I command you, come out of him and never enter him again.”

26The spirit shrieked, convulsed him violently and came out. The boy looked so much like a corpse that many said, “He’s dead.” 27But Jesus took him by the hand and lifted him to his feet, and he stood up.

28After Jesus had gone indoors, his disciples asked him privately, “Why couldn’t we drive it out?”

29He replied, “This kind can come out only by prayer.9:29 Some manuscripts prayer and fasting

Jesus Predicts His Death a Second Time

30They left that place and passed through Galilee. Jesus did not want anyone to know where they were, 31because he was teaching his disciples. He said to them, “The Son of Man is going to be delivered into the hands of men. They will kill him, and after three days he will rise.” 32But they did not understand what he meant and were afraid to ask him about it.

33They came to Capernaum. When he was in the house, he asked them, “What were you arguing about on the road?” 34But they kept quiet because on the way they had argued about who was the greatest.

35Sitting down, Jesus called the Twelve and said, “Anyone who wants to be first must be the very last, and the servant of all.”

36He took a little child whom he placed among them. Taking the child in his arms, he said to them, 37“Whoever welcomes one of these little children in my name welcomes me; and whoever welcomes me does not welcome me but the one who sent me.”

Whoever Is Not Against Us Is for Us

38“Teacher,” said John, “we saw someone driving out demons in your name and we told him to stop, because he was not one of us.”

39“Do not stop him,” Jesus said. “For no one who does a miracle in my name can in the next moment say anything bad about me, 40for whoever is not against us is for us. 41Truly I tell you, anyone who gives you a cup of water in my name because you belong to the Messiah will certainly not lose their reward.

Causing to Stumble

42“If anyone causes one of these little ones—those who believe in me—to stumble, it would be better for them if a large millstone were hung around their neck and they were thrown into the sea. 43If your hand causes you to stumble, cut it off. It is better for you to enter life maimed than with two hands to go into hell, where the fire never goes out. 449:44 Some manuscripts include here the words of verse 48. 45And if your foot causes you to stumble, cut it off. It is better for you to enter life crippled than to have two feet and be thrown into hell. 469:46 Some manuscripts include here the words of verse 48. 47And if your eye causes you to stumble, pluck it out. It is better for you to enter the kingdom of God with one eye than to have two eyes and be thrown into hell, 48where

“ ‘the worms that eat them do not die,

and the fire is not quenched.’9:48 Isaiah 66:24

49Everyone will be salted with fire.

50“Salt is good, but if it loses its saltiness, how can you make it salty again? Have salt among yourselves, and be at peace with each other.”