Marko 8 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Marko 8:1-38

Yesu Alisha Wanaume 4,000

(Mathayo 15:32-39)

18:1 Mt 15:32Katika siku hizo, umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, 28:2 Mt 9:36“Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula. 3Nikiwaaga waende nyumbani bila kula, watazimia njiani kwa sababu baadhi yao wametoka mbali.”

4Wanafunzi wake wakamjibu, “Lakini hapa nyikani tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha?”

58:5 Mt 15:34; Mk 6:38Yesu akawauliza, “Mna mikate mingapi?”

Wakajibu, “Tuna mikate saba.”

6Akawaambia watu waketi chini. Akiisha kuichukua mikate saba na kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi wake ili wawagawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo. 78:7 Mt 14:19Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. 88:8 Mk 8:20Wale watu walikula na kutosheka. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. 9Watu waliokula walikuwa wapata 4,000. Akiisha kuwaaga, 108:10 Mt 15:39aliingia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda sehemu za Dalmanutha.

Mafarisayo Waomba Ishara

(Mathayo 12:38-42; 16:1-4)

118:11 Mt 12:38Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. 128:12 Mk 7:34Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Amin nawaambieni, hakitapewa ishara yoyote.” 13Kisha akawaacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ngʼambo.

Chachu Ya Mafarisayo Na Ya Herode

(Mathayo 16:5-12)

148:14 Mt 16:5Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. 158:15 1Kor 5:6-8; Lk 12:1; Mt 14:1; Mk 12:13Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.”

168:16 Mt 16:7Wakajadiliana wao kwa wao, na kusema, “Anasema hivi kwa sababu hatukuleta mikate.”

178:17 Isa 6:9-10; Mk 6:52Yesu, akifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mnajadiliana kuhusu kutokuwa na mikate? Je, bado hamtambui wala hamwelewi? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho? 188:18 Yer 5:21; Eze 12:2Je, mna macho lakini mnashindwa kuona, na mna masikio lakini mnashindwa kusikia? Je, hamkumbuki? 198:19 Lk 9:17; Yn 6:13Nilipoimega ile mikate mitano kuwalisha watu 5,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?”

Wakamjibu, “Kumi na viwili.”

208:20 Mk 8:6-9; Mt 15:37“Je, nilipoimega ile mikate saba kuwalisha watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?”

Wakamjibu, “Saba.”

218:21 Mk 6:52Ndipo akawauliza, “Je, bado hamwelewi?”

Yesu Amponya Kipofu Huko Bethsaida

228:22 Mt 11:21; Mk 10:46; Yn 9:1Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta mtu mmoja kipofu wakamsihi Yesu amguse. 238:23 Mk 7:33; 5:23Yesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamuuliza, “Unaona chochote?”

24Yule kipofu akaangalia, akasema, “Ninaona watu, wanaonekana kama miti inayotembea.”

25Yesu akamwekea tena mikono machoni. Kisha macho yake yakafunguka, kuona kwake kukarejea naye akaona kila kitu dhahiri. 268:26 Mt 8:14; Mk 5:43Yesu akamuaga aende nyumbani kwake, akimwambia, “Hata kijijini usiingie.”

Petro Amkiri Yesu Kuwa Ndiye Kristo

(Mathayo 16:13-20; Luka 9:18-21)

278:27 Mt 16:13; Lk 9:18Yesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria-Filipi. Walipokuwa njiani, Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

288:28 Mt 3:1; Mal 4:5Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.”

298:29 Yn 6:69; 11:27Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo.”8:29 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.

308:30 Mt 17:9; Lk 9:21Yesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake.

Yesu Atabiri Kifo Chake

(Mathayo 16:21-28; Luka 9:22-27)

318:31 Mt 8:20; 16:21; 27:1-2; Mdo 2:23Ndipo akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa Mwana wa Adamu lazima atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini baada ya siku tatu afufuke. 328:32 Yn 18:20Aliyasema haya waziwazi, ndipo Petro akamchukua kando na akaanza kumkemea.

338:33 Mt 4:10Lakini Yesu alipogeuka na kuwaangalia wanafunzi wake, akamkemea Petro. Akasema, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

348:34 Mt 10:38; Lk 14:27Ndipo akauita ule umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, akasema, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 358:35 Yn 12:25Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa. 36Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? 37Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 388:38 Mt 8:20; 10:33; Lk 12:9; 1The 2:19Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

馬可福音 8:1-38

耶穌使四千人吃飽

1那時,又有一大群人聚在一起,他們沒有東西吃。耶穌就叫來門徒,說: 2「我憐憫這些人,他們跟我在一起已經三天,沒有任何吃的了。 3如果我讓他們餓著肚子回家,他們在路上會體力不支,因為有些人是遠道而來的。」

4門徒說:「在這荒郊野外,如何找到足夠的食物給這些人吃呢?」

5耶穌問:「你們有多少餅?」

門徒答道:「七個。」

6耶穌便吩咐眾人坐在地上,然後拿著那七個餅祝謝後,掰開,遞給門徒,讓門徒分給眾人,門徒就把餅分給眾人。 7他們還有幾條小魚。耶穌祝謝了,叫門徒分給眾人。 8大家都吃了,並且吃飽了,剩下的零碎裝滿了七個筐子。 9吃的人約有四千。耶穌讓眾人回家後, 10隨即和門徒上船,來到大瑪努他地區。

11法利賽人出來盤問耶穌,要求祂從天上顯一個神蹟,好試探祂。 12耶穌深深歎息道:「這世代的人為什麼總是要看神蹟呢?我實在告訴你們,沒有神蹟給這世代的人看。」 13然後,耶穌離開他們,乘船回對岸去了。

防備法利賽人和希律的酵

14門徒忘了帶餅,船上只有一個餅。 15耶穌警告他們:「你們要謹慎,要提防法利賽人和希律的酵!」

16他們彼此議論說:「這是因為我們沒有帶餅吧。」

17耶穌知道他們的心思,就說:「你們為什麼議論沒有帶餅的事呢?你們還不明白、不領悟嗎?你們的心還是愚頑嗎? 18你們有眼不會看,有耳不會聽嗎?你們不記得嗎? 19我掰開五個餅分給五千人吃的時候,你們撿了多少籃的零碎呢?」

門徒答道:「十二籃。」

20耶穌又說:「我用七個餅餵飽四千人的時候,你們撿了多少筐零碎呢?」

門徒答道:「七筐。」

21耶穌接著說:「你們還不明白嗎?」

治好伯賽大瞎眼的人

22他們到了伯賽大,有人帶來一個瞎眼的人,求耶穌摸他。 23耶穌拉著他的手帶他走到村外,吐唾沫在他的眼睛上,並把手按在他身上,問他:「你看見什麼了?」

24他抬頭看了看,說:「我看見人們,好像一棵棵的樹,走來走去。」

25耶穌又把手按在他的眼睛上,他的眼睛便睜開了,視力也恢復了,什麼都看得清清楚楚。 26耶穌叫他回家,並對他說:「不要再進這個村子了。」

彼得宣告耶穌是基督

27耶穌和門徒前往凱撒利亞·腓立比境內的村莊。在路上,祂問門徒:「人們說我是誰?」

28他們說:「有人說是施洗者約翰,有人說是以利亞,還有人說是其他某位先知。」

29耶穌又問他們:「那麼,你們說我是誰?」

彼得回答說:「你是基督!」

30耶穌叮囑他們不可洩露祂的身分。

耶穌預言自己的受難和復活

31從此,耶穌開始教導他們,人子必須受許多苦,被長老、祭司長和律法教師棄絕,並且被殺害,但必在三天之後復活。 32耶穌清楚地把這些事告訴了他們,彼得就把祂拉到一邊,開始責怪祂。 33耶穌轉身看了看門徒,斥責彼得說:「撒旦,退到我後面去!因為你不考慮上帝的意思,只考慮人的意思。」

34祂叫眾人和門徒一起過來,對他們說:「人若想跟從我,就當捨己,背起他的十字架跟從我。 35因為想救自己生命的,必失去生命;但為了我和福音失去生命的,必得到生命。 36人就算賺得全世界,卻喪失自己的生命,又有什麼益處呢? 37人還能拿什麼換回自己的生命呢?

38「在這淫亂、罪惡的世代,如果有人以我和我的道為恥,人子在祂父的榮耀中與聖天使再來的時候,也要以他為恥。」