Marko 16 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Marko 16:1-20

Kufufuka Kwa Yesu

(Mathayo 28:1-8; Luka 24:1-12; Yohana 20:1-10)

116:1 Lk 24:9; Yn 19:39-40Sabato ilipomalizika, Maria Magdalene, Maria mama yake Yakobo, na Salome walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu. 216:2 Lk 24:1; Yn 20:1Asubuhi na mapema, siku ya kwanza ya juma, mara tu baada ya kuchomoza jua, walikwenda kaburini. 316:3 Mk 15:46Njiani wakawa wanaulizana wao kwa wao, “Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe kutoka kwenye ingilio la kaburi?”

4Lakini walipotazama, wakaona lile jiwe, ambalo lilikuwa kubwa sana, limekwisha kuvingirishwa kutoka pale penye ingilio la kaburi. 516:5 Lk 24:3-4Walipokuwa wakiingia mle kaburini, wakamwona kijana mmoja aliyevaa joho jeupe akiwa ameketi upande wa kuume, nao wakastaajabu.

616:6 Mk 1:24Yule malaika akawaambia, “Msistaajabu. Mnamtafuta Yesu, Mnazareti, aliyesulubiwa. Amefufuka! Hayuko hapa. Tazameni mahali walipomlaza. 716:7 Yn 21:1-23; Mk 14:28Lakini nendeni mkawaambie wanafunzi wake pamoja na Petro, kwamba, ‘Anawatangulia kwenda Galilaya. Huko ndiko mtamwona, kama alivyowaambia.’ ”

816:8 Mt 28:8; Lk 24:9Hivyo wakatoka, wakakimbia kutoka mle kaburini wakiwa na hofu kuu na mshangao. Nao hawakumwambia mtu yeyote neno lolote, kwa sababu waliogopa.

Yesu Anamtokea Maria Magdalene

(Mathayo 28:9-10; Yohana 20:11-18)

916:9 Mk 15:4-7Yesu alipofufuka alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma alimtokea kwanza Maria Magdalene, yule ambaye alikuwa amemtoa pepo wachafu saba. 1016:10 Lk 24:10; Yn 20:18Maria akaenda, naye akawaambia wale waliokuwa wamefuatana na Yesu, waliokuwa wanaomboleza na kulia. 1116:11 Mk 16:13, 14; Lk 24:11Lakini waliposikia kwamba Yesu yu hai na kwamba Maria alikuwa amemwona, hawakusadiki.

Yesu Awatokea Wanafunzi Wawili

(Luka 24:13-35)

1216:12 Lk 24:13-32Baadaye Yesu akawatokea wawili miongoni mwa wanafunzi wake walipokuwa wakienda shambani akiwa katika sura nyingine. 13Nao wakarudi na kuwaambia wenzao. Lakini hawakuwasadiki wao pia.

Yesu Awaagiza Wale Wanafunzi Kumi Na Mmoja

(Mathayo 28:16-20; Luka 24:36-49; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8)

1416:14 Lk 24:36-43Baadaye Yesu akawatokea wale wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa wakila chakula. Akawakemea kwa kutoamini kwao na kwa ugumu wa mioyo yao kwa kutosadiki wale waliomwona baada yake kufufuka.

1516:15 Mt 28:18-20; Mdo 1:8Akawaambia, “Enendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 1616:16 Mdo 16:31; Yn 12:48Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini yeyote asiyeamini atahukumiwa. 1716:17 Lk 10:17; 1Kor 13:1; 14:2-39Nazo ishara hizi zitafuatana na wanaoamini: Kwa Jina langu watatoa pepo wachafu; watasema kwa lugha mpya; 1816:18 Lk 10:19; Mdo 28:3-5; 6:6watashika nyoka kwa mikono yao; na hata wakinywa kitu chochote cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.”

[Yesu Apaa Kwenda Mbinguni

(Luka 24:50-53; Matendo 1:9-11)

1916:19 Lk 24:50-51; Yn 6:6; Mdo 1:19; 1Tim 3:16; Za 110:1; Mt 26:64; Mdo 2:33; 5:31; Rum 8:34; Kol 3:1; Ebr 1:3; 12:2Baada ya Bwana Yesu kusema nao, alichukuliwa juu mbinguni na kuketi mkono wa kuume wa Mungu. 2016:20 Yn 4:48Kisha wanafunzi wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno lake kwa ishara zilizofuatana nalo.]