Marko 10 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Marko 10:1-52

Mafundisho Kuhusu Talaka

(Mathayo 19:1-12; Luka 16:18)

110:1 Yn 10:40; 11:7; Mt 4:23; Mk 4:2Yesu akaondoka huko, akavuka Mto Yordani, akaenda sehemu za Uyahudi. Umati mkubwa wa watu ukaenda kwake tena, naye kama ilivyokuwa desturi yake, akawafundisha.

210:2 Mk 2:16Baadhi ya Mafarisayo wakaja ili kumjaribu kwa kumuuliza, “Je, ni halali mtu kumwacha mke wake?”

3Yesu akawajibu, “Je, Mose aliwaamuru nini?”

410:4 Kum 24:1-4; Mt 5:31Wakajibu, “Mose aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.”

510:5 Za 95:8; Ebr 3:15Yesu akawaambia, “Mose aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 610:6 Mwa 1:27; 5:2Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. 710:7 Mwa 2:2; 1Kor 6:16; Efe 5:31Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.’ 810:8 Mwa 2:24; 1Kor 6:16Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena, bali mwili mmoja. 9Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”

10Walipokuwa tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamuuliza kuhusu jambo hili. 1110:11 Mt 5:32; Lk 16:8Akawajibu, “Mtu yeyote amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine, anazini naye. 1210:12 Rum 7:3; 1Kor 7:10-11Naye mwanamke amwachaye mumewe na kuolewa na mume mwingine, anazini.”

Yesu Anawabariki Watoto Wadogo

(Mathayo 19:13-15; Luka 18:15-17)

1310:13 Mt 19:13; Lk 18:15Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wake wakawakemea. 1410:14 Mt 25:34Yesu alipoona yaliyokuwa yakitukia, akachukizwa. Akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa. 1510:15 Mt 18:3Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.” 1610:16 Mk 9:36Akawachukua watoto mikononi mwake, akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.

Kijana Tajiri

(Mathayo 19:16-30; Luka 18:18-30)

1710:17 Mk 1:40; Lk 10:25; Mdo 20:32Yesu alipokuwa anaondoka, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake, akamuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

18Yesu akamwambia, “Mbona unaniita mwema? Hakuna yeyote aliye mwema ila Mungu peke yake. 1910:19 Kut 20:12-16; Kum 5:16-20Unazijua amri: ‘Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, waheshimu baba yako na mama yako.’ ”

20Akamjibu, “Mwalimu, amri hizi zote nimezishika tangu nikiwa mtoto.”

2110:21 Mdo 2:45; Mt 6:20; Lk 12:33; Mt 4:19Yesu akamtazama na kumpenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

22Yule mtu aliposikia hayo, akasikitika sana. Akaondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

2310:23 Za 62:10; 1Tim 6:9-17Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa wenye mali kuingia katika Ufalme wa Mungu!”

2410:24 Mt 7:13-14; Yn 3:5Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Yesu akawaambia tena, “Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika Ufalme wa Mungu. 2510:25 Lk 12:16-20; 16:19-31Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri10:25 Tajiri ina maana wale wanaotumainia mali. kuingia katika Ufalme wa Mungu.”

26Wanafunzi wake wakashangaa sana. Wakaulizana wao kwa wao, “Ni nani basi awezaye kuokoka?”

2710:27 Mt 19:26Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu.”

2810:28 Mt 4:18-19; Lk 18:28Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha kila kitu na kukufuata wewe!”

29Yesu akasema, “Amin, nawaambia, hakuna mtu yeyote aliyeacha nyumba, ndugu wa kiume au wa kike, au mama au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, 3010:30 Mt 6:33; 12:32; 25:46ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu: nyumba, ndugu wa kiume na wa kike, mama na baba na watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao. 3110:31 Mt 19:30Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na wa mwisho watakuwa wa kwanza.”

Yesu Atabiri Mara Ya Tatu Kufa Na Kufufuka Kwake

(Mathayo 20:17-19; Luka 18:31-34)

3210:32 Mk 3:16-19Walikuwa njiani wakipanda kwenda Yerusalemu, na Yesu alikuwa ametangulia. Wanafunzi wake walishangaa, nao watu waliowafuata walijawa na hofu. Yesu akawachukua tena wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia yatakayompata. 3310:33 Lk 9:51; Mt 8:20; 27:1-2Akasema, “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atasalitiwa kwa viongozi wa makuhani na walimu wa sheria. Wao watamhukumu kifo na kumtia mikononi mwa watu wa Mataifa, 3410:34 Mdo 2:23; Mt 16:21ambao watamdhihaki na kumtemea mate, watampiga na kumuua. Siku tatu baadaye atafufuka.”

Ombi La Yakobo Na Yohana

(Mathayo 20:20-28)

3510:35 Mt 20:20; 20:20-28Kisha Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakaja kwake na kumwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie lolote tutakalokuomba.”

36Naye akawaambia, “Je, mwataka niwafanyie jambo gani?”

3710:37 Mt 19:28Wakamwambia, “Tupe kukaa mmoja upande wako wa kuume na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wako.”

3810:38 Ay 38:2; Mt 20:22; Lk 12:50Lakini Yesu akawaambia, “Ninyi hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kukinywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?”

3910:39 Mdo 12:22; Ufu 1:9Wakajibu, “Tunaweza.”

Kisha Yesu akawaambia, “Kikombe nikinyweacho mtakinywea na ubatizo nibatizwao mtabatizwa, 40lakini kuketi mkono wangu wa kuume au wa kushoto si juu yangu mimi kuwapa. Nafasi hizi ni kwa ajili ya wale walioandaliwa.”

4110:41 Mt 20:24Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana. 4210:42 Lk 22:25-27Lakini Yesu akawaita wote pamoja na kuwaambia, “Mnafahamu kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala watu kwa nguvu, nao wenye vyeo huonyesha mamlaka yao. 4310:43 Mk 5:35Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu, 44na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa mtumwa wa wote. 4510:45 Mt 20:28Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”

Yesu Amponya Kipofu Bartimayo

(Mathayo 20:29-34; Luka 18:35-43)

4610:46 Mt 20:29; Lk 18:35-43; Mt 20:29-34; Lk 18:35-43Kisha wakafika Yeriko. Yesu alipokuwa akiondoka mjini na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mmoja, jina lake Bartimayo, mwana wa Timayo, alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. 4710:47 Mk 1:24; Mt 9:27Aliposikia kuwa ni Yesu wa Nazareti aliyekuwa anapita, akaanza kupaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”

48Watu wengi wakamkemea, wakamwambia akae kimya, lakini yeye akazidi kupaza sauti, akisema, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”

49Yesu akasimama na kusema, “Mwiteni.”

Hivyo wakamwita yule mtu kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Inuka, anakuita.” 50Akiwa analivua lile joho lake, alisimama na kumwendea Yesu.

5110:51 Mt 23:7Yesu akamuuliza, “Unataka nikufanyie nini?”

Yule kipofu akajibu, “Mwalimu, nataka kuona.”

5210:52 Mt 9:22; 4:19; Mk 5:34Yesu akamwambia, “Nenda zako, imani yako imekuponya.” Mara akapata kuona, akamfuata Yesu njiani.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

马可福音 10:1-52

论婚姻

1耶稣离开那里,来到犹太地区和约旦河东岸,人群又聚集到祂那里。耶稣像往常一样教导他们。 2一些法利赛人想试探耶稣,就来问祂:“男人可以休妻吗?” 3耶稣反问道:“摩西怎么吩咐你们的?”

4他们说:“摩西准许人写休书休妻。”

5耶稣说:“摩西因为你们心硬,才给你们写了这条诫命。 6太初创造时,‘上帝造了男人和女人。’ 7‘因此,人要离开父母,与妻子结合, 8二人成为一体。’这样,夫妻不再是两个人,而是一体了。 9因此,上帝配合的,人不可分开。”

10回到屋里后,门徒追问耶稣这件事。 11耶稣说:“任何人休妻另娶,就是对妻子不忠,是犯通奸罪。 12同样,妻子若离弃丈夫另嫁,也是犯通奸罪。”

祝福孩童

13有人带着小孩子来要让耶稣摸一摸,门徒却责备他们。 14耶稣看见后很生气,对门徒说:“让小孩子到我这里来,不要阻止他们,因为上帝的国属于这样的人。 15我实在告诉你们,人若不像小孩子一样接受上帝的国,绝不能进去。” 16于是,耶稣抱起小孩子,把手按在他们身上,为他们祝福。

永生的代价

17耶稣正要上路,有一个人跑来跪在祂跟前,问祂:“良善的老师,我该做什么才能承受永生?”

18耶稣说:“你为什么称呼我‘良善的老师’呢?只有上帝是良善的。 19你知道‘不可杀人,不可通奸,不可偷盗,不可作伪证,不可欺诈,要孝敬父母’这些诫命。”

20那人说:“老师,我从小就遵行这些诫命。”

21耶稣望着他,心中爱他,便说:“你还有一件事没有做,就是变卖你所有的产业,送给穷人,你必有财宝存在天上,然后你还要来跟从我。”

22那人听了,脸色骤变,便沮丧地走了,因为他有许多产业。 23耶稣看看周围的人,对门徒说:“有钱人进上帝的国真难啊!”

24门徒听了感到惊奇,耶稣便再次对他们说:“孩子们,10:24 有古卷此处有“依靠钱财的人”。进上帝的国多么难啊! 25骆驼穿过针眼比有钱人进上帝的国还容易呢!”

26门徒更加惊奇,便议论说:“这样,谁能得救呢?”

27耶稣看着他们说:“对人而言,这不可能,但对上帝而言,凡事都可能。”

28彼得说:“你看,我们已经撇下一切来跟从你了。”

29耶稣说:“我实在告诉你们,任何人为了我和福音而撇下房屋、弟兄、姊妹、父母、儿女或田地, 30今世必在房屋、弟兄、姊妹、父母、儿女或田地方面获得百倍的回报,来世必得永生。当然他也会受到迫害。 31然而,许多为首的将要殿后,殿后的将要为首。”

耶稣第三次预言自己的受难

32在前往耶路撒冷的路上,耶稣走在众人前面,门徒感到惊奇,其他跟随的人也很害怕。

耶稣把十二个门徒叫到一旁,再把自己将要遭遇的事告诉他们,说: 33“听着,我们现在前往耶路撒冷,人子将被交在祭司长和律法教师的手中,他们要判祂死刑,把祂交给外族人。 34他们会嘲弄祂,向祂吐唾沫,鞭打祂,杀害祂。但是,三天之后祂必复活!”

雅各与约翰的请求

35西庇太的两个儿子雅各约翰上前对耶稣说:“老师,请你答应我们一个要求。”

36耶稣问:“什么要求?”

37他们说:“在你的荣耀中,求你让我们一个坐在你右边,一个坐在你左边。”

38耶稣说:“你们不知道自己在求什么。我要喝的那杯,你们能喝吗?我要受的洗,你们能受吗?”

39他们说:“我们能。”

耶稣说:“我要喝的那杯,你们也要喝;我所受的洗,你们也要受。 40不过谁坐在我的左右不是我来定,而是为谁预备的,就让谁坐。”

41其他十个门徒听见这事后,很生雅各约翰的气。 42于是,耶稣把他们叫来,对他们说:“你们知道,外族人有君王统治他们,有大臣管理他们, 43但你们不可这样。你们中间谁要当首领,谁就要做大家的仆人; 44谁要居首位,谁就要做大家的奴仆。 45因为就连人子也不是来受人服侍,而是来服侍人,并且牺牲性命,作许多人的赎价。”

治好瞎子巴底买

46耶稣和门徒来到耶利哥。当耶稣和门徒及众人出城的时候,遇见一个瞎眼的乞丐坐在路旁乞讨,他的名字叫巴底买,是底买的儿子。 47巴底买一听到经过的是拿撒勒人耶稣,就喊道:“大卫的后裔耶稣啊,可怜我吧!”

48许多人都责备他,叫他不要吵,但他却更加大声喊道:“大卫的后裔啊,可怜我吧!”

49耶稣停下脚步,叫人带他过来。

他们就对瞎子巴底买说:“好了,起来吧,祂叫你呢。”

50巴底买丢下外衣,跳了起来,走到耶稣面前。

51耶稣问他:“你要我为你做什么?”

瞎子说:“老师,我想能够看见。”

52耶稣说:“回去吧!你的信心救10:52 ”或译“医治”。了你。”那人立刻得见光明,在路上跟从了耶稣。