Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Marko 1:1-45

Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji

(Mathayo 3:1-12; Luka 3:1-8; Yohana 1:19-28)

11:1 Mt 4:3Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.

21:2 Mal 3:1; Lk 7:27Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:

“Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,

atakayetengeneza njia mbele yako”:

31:3 Isa 40:3; Yn 1:23“sauti ya mtu aliaye nyikani.

‘Itengenezeni njia ya Bwana,

yanyoosheni mapito yake.’ ”

41:4 Yn 1:26, 33; Mt 3:1; Mdo 11:16; Lk 1:7Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 51:5 Mt 3:5Watu kutoka Uyahudi wote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani. 61:6 Law 11:22; Mt 3:4Yohana alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 71:7 Mdo 13:25; Yn 1:27; Mdo 13:25Naye alihubiri akisema, “Baada yangu atakuja yeye aliye na uwezo kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. 81:8 Yoe 2:28; Yn 1:33Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”

Ubatizo Wa Yesu

(Mathayo 3:13-17; Luka 3:21-22)

91:9 Mt 2:23; Lk 3:21Wakati huo Yesu akaja kutoka Nazareti ya Galilaya, naye akabatizwa na Yohana katika Mto Yordani. 101:10 Yn 1:32Yesu alipokuwa akitoka ndani ya maji, aliona mbingu zikifunguka na Roho akishuka juu yake kama hua. 111:11 Mt 3:17; Mk 9:7; Za 2:7; Isa 42:1Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”

Majaribu Ya Yesu

(Mathayo 4:1-11; Luka 4:1-13)

121:12 Mt 4:1; Lk 4:1Wakati huo huo, Roho akamwongoza Yesu kwenda nyikani, 131:13 Mt 4:10; Ebr 4:15naye akawa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikaa na wanyama wa mwituni, nao malaika wakamhudumia.

Yesu Aanza Kuhubiri

141:14 Mt 4:12; 4:23; 4:12; 4:23; Lk 4:14, 15Baada ya Yohana kukamatwa na kutiwa gerezani, Yesu aliingia Galilaya akaanza kuhubiri habari njema ya Mungu, 151:15 Rum 5:6; Gal 4:4; Mdo 20:21akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.”

Yesu Awaita Wanafunzi Wanne

(Mathayo 4:12-22; Luka 4:14-15; 5:1-11)

161:16 Mt 4:18; Lk 5:4Yesu alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 171:17 Mt 13:47Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” 181:18 Mt 19:27; Lk 5:11; Mt 4:19Mara wakaacha nyavu zao, wakamfuata.

191:19 Mt 4:21Alipokwenda mbele kidogo, akamwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa kwenye mashua yao wakizitengeneza nyavu zao. 20Papo hapo akawaita, nao wakamwacha Zebedayo baba yao kwenye mashua pamoja na watumishi wa kuajiriwa, nao wakamfuata Yesu.

Yesu Amtoa Pepo Mchafu

(Luka 4:31-37)

211:21 Mk 1:39; Mt 4:23Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya Sabato, mara Yesu akaingia sinagogi, akaanza kufundisha. 221:22 Mt 7:28-29Watu wakashangaa sana kwa mafundisho yake, kwa maana aliwafundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wa sheria. 231:23 Lk 4:33Wakati huo huo katika sinagogi lao palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, 241:24 Mt 8:29; Yn 1:45-46; Mdo 4:10; Za 16:10; 1Yn 2:20naye akapiga kelele akisema, “Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!”

251:25 Mk 1:34Lakini Yesu akamkemea, akamwambia, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” 261:26 Mk 9:20Yule pepo mchafu akamtikisatikisa huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa.

271:27 Mk 10:24, 32Watu wote wakashangaa, hata wakaulizana wao kwa wao, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya, tena yenye mamlaka! Anaamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!” 281:28 Mk 9:26Sifa zake zikaanza kuenea haraka katika eneo lote la karibu na Galilaya.

Yesu Amponya Mama Mkwe Wa Simoni

(Mathayo 8:14-15; Luka 4:38-39)

291:29 Mt 8:14; Lk 4:38Mara walipotoka katika sinagogi, walikwenda pamoja na Yakobo na Yohana hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea. 30Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Yesu habari zake. 311:31 Lk 7:14Hivyo Yesu akamwendea, akamshika mkono na kumwinua. Kisha homa ikamwacha, naye akaanza kuwahudumia.

Yesu Aponya Wengi

(Mathayo 8:16-17; Luka 4:40-41)

321:32 Mt 4:24Jioni ile baada ya jua kutua, watu wakamletea Yesu wagonjwa wote na waliopagawa na pepo wachafu. 33Mji wote ukakusanyika mbele ya nyumba hiyo. 341:34 Mt 4:23; Mk 3:12; Mdo 16:17-18Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Akawatoa pepo wachafu wengi, lakini hakuwaacha hao pepo wachafu waseme, kwa sababu walimjua yeye ni nani.

Yesu Aenda Galilaya

(Luka 4:42-44)

351:35 Lk 3:21Alfajiri na mapema sana kulipokuwa bado kuna giza, Yesu akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha ili kuomba. 361:36 Lk 4:43-44Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta, 37nao walipomwona, wakamwambia, “Kila mtu anakutafuta!”

381:38 Isa 61:1Yesu akawajibu, “Twendeni mahali pengine kwenye vijiji jirani, ili niweze kuhubiri huko pia, kwa sababu hicho ndicho nilichokuja kukifanya.” 391:39 Mt 4:23-24Kwa hiyo akazunguka Galilaya kote, akihubiri katika masinagogi yao na kutoa pepo wachafu.

Yesu Amtakasa Mwenye Ukoma

(Mathayo 8:1-4; Luka 5:12-16)

401:40 Mk 10:17Mtu mmoja mwenye ukoma alimjia Yesu, akamwomba akipiga magoti, akamwambia, “Ukitaka, waweza kunitakasa.”

41Yesu, akiwa amejawa na huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka. Takasika!” 42Mara ukoma ukamtoka, naye akatakasika. 431:43 Mk 3:12; 7:36Baada ya Yesu kumwonya vikali, akamruhusu aende zake 441:44 Mt 8:4; Law 13:49; 14:1-32akimwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote habari hizi, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka alizoagiza Mose kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.” 451:45 Lk 5:15-16, 17; Yn 6:2Lakini yule mtu akaenda akaanza kutangaza habari za kuponywa kwake waziwazi. Kwa hiyo, Yesu hakuweza tena kuingia katika miji waziwazi lakini alikaa sehemu zisizo na watu. Hata hivyo watu wakamfuata huko kutoka kila upande.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

马可福音 1:1-45

施洗者约翰预备道路

1有关上帝的儿子耶稣基督的福音是这样开始的。

2以赛亚先知书上说:

“看啊,

我要差遣我的使者在你前面为你预备道路。

3他在旷野大声呼喊,

‘预备主的道,

修直祂的路。’”

4果然,约翰出现了,他在旷野劝人悔改,接受洗礼,使罪得到赦免。 5犹太全境和耶路撒冷的居民都到约翰面前承认他们的罪,在约旦河里接受他的洗礼。

6约翰身穿骆驼毛的衣服,腰束皮带,吃的是蝗虫和野蜜。 7他传道说:“在我之后,有一位能力比我更大的要来,我连弯腰替祂解鞋带也不配。 8我是用水给你们施洗,但祂要用圣灵给你们施洗。”

耶稣受洗

9那时,耶稣从加利利拿撒勒约旦河接受约翰的洗礼。 10耶稣从水中一上来,就看见天开了,圣灵好像鸽子一样降在祂身上, 11从天上有声音说:“你是我的爱子,我甚喜悦你。”

耶稣受试探

12圣灵随即催促祂到旷野。 13祂在旷野受撒旦的试探四十天。祂与野兽在一起,有天使服侍祂。

呼召四渔夫

14约翰被捕后,耶稣来到加利利宣讲上帝的福音,说: 15“时候到了,上帝的国临近了,你们要悔改,相信福音。”

16耶稣沿着加利利湖边走,看见两个渔夫——西门和他的弟弟安得烈正在湖上撒网捕鱼。 17耶稣对他们说:“来跟从我!我要使你们成为得人的渔夫。” 18他们立刻抛下渔网,跟从了耶稣。

19耶稣往前走了不远,又看见西庇太的两个儿子雅各约翰正在船上补网, 20便立刻呼召他们。他们就辞别父亲和船上的工人,跟从了耶稣。

传道赶鬼

21他们到了迦百农,耶稣在安息日去会堂里讲道。 22那里的人都很吃惊,因为祂教导他们时像个有权柄的人,不像律法教师。 23当时会堂里有一个被污鬼附身的人喊道: 24拿撒勒的耶稣啊,我们和你有什么关系?你是来毁灭我们吗?我知道你是谁,你是上帝的圣者!”

25耶稣责备它说:“住口,从他身上出来!”

26污鬼使那人抽搐了一阵,大叫一声,就出来了。 27在场的人十分惊讶,彼此议论说:“这是怎么回事?真是充满权柄的新教导啊!竟然连污鬼都服从祂的命令。” 28于是,耶稣的名声立刻传遍了整个加利利

医病赶鬼

29耶稣同雅各约翰离开会堂,来到西门安得烈家。 30当时西门的岳母正发烧,躺在床上,他们立刻把这事告诉耶稣。 31耶稣走到她的床边,拉着她的手扶她起来,她的烧立刻退了,便起来服侍他们。

32日落之后,有人把病人和被鬼附身的人都带来见耶稣。 33全城的人都聚在门前。 34耶稣医好了许多患各种疾病的人,又赶出很多鬼。祂不准鬼说话,因为鬼认识祂。

在加利利传道

35第二天清早,天还没亮,耶稣就起来独自走到旷野去祷告。 36西门和同伴们四处寻找耶稣, 37找到了,便对祂说:“大家都在找你呢!”

38耶稣却回答说:“我们到附近的乡镇去吧,我也好在那里传道,因为我就是为这事来的。”

39于是,耶稣走遍加利利,在各会堂传道,赶鬼。

治好麻风病人

40有一次,一个患麻风病的人来到耶稣面前,跪下央求:“只要你肯,一定能使我洁净。”

41耶稣动了慈心,就伸手摸他,说:“我肯,你洁净了吧!” 42那人的麻风病立即消失了,他就洁净了。 43耶稣让他回去并郑重地叮嘱: 44“不要把这事告诉别人,要去让祭司察看你的身体,并照摩西的规定献祭,向众人证明你已经洁净了。”

45但那人离开之后,却到处传扬这件事,以致耶稣无法再公开进城。祂只能待在城外的旷野,可是人们仍从各处来找祂。