15:1 Za 44:13-16; 89:50Kumbuka, Ee Bwana, yaliyotupata,
tazama, nawe uione aibu yetu.
25:2 Za 79:1; Sef 1:13; Yer 17:4Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni,
na nyumba zetu kwa wageni.
35:3 Kut 22:24; Yer 15:8; 18:21Tumekuwa yatima wasio na baba,
mama zetu wamekuwa kama wajane.
45:4 Isa 55:1; Eze 4:16-17; Isa 3:1Ni lazima tununue maji tunayokunywa,
kuni zetu zapatikana tu kwa kununua.
55:5 Isa 47:6; Neh 9:37; Yos 1:13Wanaotufuatilia wapo kwenye visigino vyetu,
tumechoka na hakuna pumziko.
65:6 Yer 2:36; Mwa 24:2; Hos 5:13; 7:11; Yer 50:15; Hos 12:1Tumejitolea kwa Misri na Ashuru
tupate chakula cha kutosha.
75:7 Yer 14:20; 16:12; Eze 8:2; Yer 31:29; Eze 18:2; Mt 23:32Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena,
na sisi tunachukua adhabu yao.
85:8 Neh 5:15; Zek 11:6Watumwa wanatutawala
na hakuna wa kutuokoa mikononi yao.
9Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu
kwa sababu ya upanga jangwani.
105:10 Ay 30:30; Mao 4:8-9Ngozi yetu ina joto kama tanuru,
kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa.
115:11 Mwa 34:29; Zek 14:2; Isa 13:16Wanawake wametendwa jeuri katika Sayuni,
na mabikira katika miji ya Yuda.
12Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao,
wazee hawapewi heshima.
135:13 Amu 13:16; 16:21Vijana wanataabika kwenye mawe ya kusagia,
wavulana wanayumbayumba chini ya mizigo ya kuni.
145:14 Isa 24:8; Yer 7:34; 2Fal 25:18Wazee wameondoka langoni la mji,
vijana wameacha kuimba nyimbo zao.
155:15 Amu 8:10; Yer 25:10Furaha imeondoka mioyoni mwetu,
kucheza kwetu kumegeuka maombolezo.
165:16 Yer 13:18; 14:20; Za 89:39; Ay 19:9; Isa 3:11Taji imeanguka kutoka kichwani petu.
Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!
175:17 Ay 17:7; Za 6:7; 16:8; Yer 8:18Kwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia,
kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia,
185:18 Isa 27:10; Mik 3:12; Za 74:2-4kwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa,
nao mbweha wanatembea juu yake.
195:19 1Nya 16:31; Za 45:6; 102:22-27Wewe, Ee Bwana unatawala milele,
kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi.
205:20 Za 13:1; 44:24; 71:11Kwa nini watusahau siku zote?
Kwa nini umetuacha kwa muda mrefu?
215:21 Isa 60:20-22; Za 80:3Turudishe kwako mwenyewe, Ee Bwana,
ili tupate kurudi.
Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale,
225:22 Isa 64:9; Yer 6:30; Za 53:5; 60:12isipokuwa uwe umetukataa kabisa
na umetukasirikia pasipo kipimo.