Maombolezo 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Maombolezo 3:1-66

3 Sura hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. 13:1 Ay 19:21; Za 88:7; Yer 15:17-18Mimi ndiye mtu aliyeona mateso

kwa fimbo ya ghadhabu yake.

23:2 Ay 19:8; Za 82:5; Yer 4:23Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee

gizani wala si katika nuru;

33:3 Isa 5:25; Za 38:2hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu

tena na tena, mchana kutwa.

43:4 Za 51:8; Isa 38:13; Yer 50:17; Ay 30:30; Mao 4:8Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa

na ameivunja mifupa yangu.

53:5 Yer 23:15Amenizingira na kunizunguka

kwa uchungu na taabu.

63:6 Isa 59:10; Za 143:3; 88:5-6Amenifanya niishi gizani

kama wale waliokufa.

73:7 Ay 3:23; Yer 40:4Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka,

amenifunga kwa minyororo mizito.

83:8 Kum 1:45; Ay 30:20; Za 22:2; 5:2Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada,

anakataa kupokea maombi yangu.

93:9 Ay 9:24; Hos 2:6; Isa 63:17Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe,

amepotosha njia zangu.

103:10 Ay 10:16; Hos 13:8; Amo 5:18-19Kama dubu aviziaye,

kama simba mafichoni,

11ameniburuta kutoka njia,

akanirarua na kuniacha bila msaada.

123:12 Mao 2:4; Ay 16:12; Za 38:2; 34:2Amevuta upinde wake

na kunifanya mimi niwe lengo

kwa ajili ya mishale yake.

13Alinichoma moyo wangu kwa mishale

iliyotoka kwenye podo lake.

143:14 Mwa 38:23; Za 22:6-7; Ay 30:9; Neh 4:2-4; Mt 27:29-31; Yer 20:7Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote,

wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa.

153:15 Yer 9:15Amenijaza kwa majani machungu

na kunishibisha kwa nyongo.

163:16 Mit 20:17Amevunja meno yangu kwa changarawe,

amenikanyagia mavumbini.

17Amani yangu imeondolewa,

nimesahau kufanikiwa ni nini.

183:18 Ay 17:15; Za 31:22Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondoka

na yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa Bwana.”

19Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu,

uchungu na nyongo.

203:20 Za 42:5; 43:5Ninayakumbuka vyema,

nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu.

21Hata hivyo najikumbusha neno hili

na kwa hiyo ninalo tumaini.

223:22 Za 130:7; Mt 3:6; Neh 9:31; Ay 34:15; Za 130:1; Hos 11:9; Za 78:38; 57:10; Mal 3:6Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,

kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.

233:23 Kut 34:6; Isa 33:2; Ebr 10:23Ni mpya kila asubuhi,

uaminifu wako ni mkuu.

243:24 Za 16:5Nimeiambia nafsi yangu, “Bwana ni fungu langu,

kwa hiyo nitamngojea.”

253:25 Za 33:18; Isa 25:9; 30:18; Za 130:6Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake,

kwa yule ambaye humtafuta;

263:26 Za 37:7ni vyema kungojea kwa utulivu

kwa ajili ya wokovu wa Bwana.

273:27 Za 90:12Ni vyema mtu kuchukua nira

bado angali kijana.

283:28 Yer 15:17Na akae peke yake awe kimya,

kwa maana Bwana ameiweka juu yake.

293:29 Yer 31:17; Ay 2:8; 42:6Na azike uso wake mavumbini

bado panawezekana kuwa na matumaini.

303:30 Ay 16:10; Isa 50:6; Mik 5:1; Mt 5:39Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye,

na ajazwe na aibu.

313:31 Za 94:14; Isa 54:7Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali

na Bwana milele.

323:32 Za 106:43-45; Nah 1:12; Hos 11:8Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma,

kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.

333:33 Ay 37:23; Ebr 12:10; Yer 31:20; Eze 18:23Kwa maana hapendi kuwaletea mateso

au huzuni watoto wa wanadamu.

34Kuwaponda chini ya nyayo

wafungwa wote katika nchi,

353:35 Mwa 14:18-22Kumnyima mtu haki zake

mbele za Aliye Juu Sana,

363:36 Za 140:12; Mit 17:15; Hab 1:13; Yer 22:3kumnyima mtu haki:

Je, Bwana asione mambo kama haya?

373:37 Mit 19:21; Za 33:9-11; Mit 21:30Nani awezaye kusema nalo likatendeka

kama Bwana hajaamuru?

383:38 Ay 2:10; Isa 45:7; Yer 32:42Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana

ndiko yatokako maafa na mambo mema?

393:39 Yer 30:15; Mik 7:9Mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamika

wakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake?

403:40 2Kor 13:5; Za 119:59; 139:23-24Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu,

na tumrudie Bwana Mungu.

413:41 Dan 9:5; Yer 14:20; 2Fal 24:4; Yer 5:7-9; Za 86:4Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu

kwa Mungu mbinguni, na tuseme:

423:42 Dan 9:5“Tumetenda dhambi na kuasi

nawe hujasamehe.

433:43 Mao 2:2, 17, 21; Za 35:6“Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia;

umetuchinja bila huruma.

443:44 Mao 2:1; Zek 7:13; Za 97:2; Isa 58:4Unajifunika mwenyewe kwa wingu,

ili pasiwe na ombi

litakaloweza kupenya.

453:45 1Kor 4:13Umetufanya takataka na uchafu

miongoni mwa mataifa.

463:46 Za 22:13; Mao 2:16“Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao

wazi dhidi yetu.

473:47 Yer 48:43; Isa 24:17-18; 51:19Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula,

uharibifu na maangamizi.”

483:48 Yer 9:1; Mao 2:18Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu,

kwa sababu watu wangu wameangamizwa.

49Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma,

bila kupata nafuu,

503:50 Za 14:2; 80:14; Isa 63:15hadi Bwana atazame chini

kutoka mbinguni na kuona.

51Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini

kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu.

523:52 Za 35:7; 69:4Wale waliokuwa adui zangu bila sababu

wameniwinda kama ndege.

533:53 Yer 38:6; 37:16; Dan 6:17Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo

na kunitupia mawe;

543:54 Za 69:2; Yon 2:3-5; Eze 37:11; Za 88:5maji yalifunika juu ya kichwa changu,

nami nikafikiri nilikuwa karibu

kukatiliwa mbali.

553:55 Za 130:1; 2Nya 33:12; Yon 2:2; Za 18:5, 6Nililiitia jina lako, Ee Bwana,

kutoka vina vya shimo.

563:56 Rum 8:26; Za 116:1-2; 6:8Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako

kilio changu nikuombapo msaada.”

573:57 Isa 41:10; Yak 4:8; Za 46:1; 69:18; Isa 58:9Ulikuja karibu nilipokuita,

nawe ukasema, “Usiogope.”

583:58 Yer 51:36; Za 34:22; Yer 50:34; 1Sam 25:39Ee Bwana, ulichukua shauri langu,

ukaukomboa uhai wangu.

593:59 Yer 18:19; Za 35:23Umeona, Ee Bwana, ubaya niliotendewa.

Tetea shauri langu!

603:60 Yer 11:20; 18:18Umeona kina cha kisasi chao,

mashauri yao yote mabaya dhidi yangu.

61Ee Bwana, umesikia matukano yao,

mashauri yao yote mabaya dhidi yangu:

623:62 Eze 36:3kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikia

dhidi yangu mchana kutwa.

633:63 Ay 30:9; Za 139:2Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama,

wananidhihaki katika nyimbo zao.

643:64 Za 28:4; Yer 51:6; 2Tim 4:14; Yer 11:20; Ufu 6:10Uwalipe kile wanachostahili, Ee Bwana,

kwa yale ambayo mikono yao imetenda.

653:65 Kut 14:8; Kum 2:30; Isa 6:10; Za 8:3Weka pazia juu ya mioyo yao,

laana yako na iwe juu yao!

66Wafuatilie katika hasira na uwaangamize

kutoka chini ya mbingu za Bwana.