Maombolezo 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Maombolezo 2:1-22

2 Sura hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. 12:1 Mao 3:44; Za 132:7; 1Nya 28:2; Yer 12:7; Za 99:5; Mt 11:23; 2Sam 1:19Tazama jinsi Bwana alivyomfunika Binti Sayuni

kwa wingu la hasira yake!

Ameitupa chini fahari ya Israeli

kutoka mbinguni mpaka duniani,

hakukumbuka kiti chake cha kuwekea miguu

katika siku ya hasira yake.

22:2 Mao 3:43; Mik 5:11; Isa 25:12; Za 89:39-40; 21:9Bila huruma Bwana ameyameza

makao yote ya Yakobo;

katika ghadhabu yake amebomoa

ngome za Binti Yuda.

Ameuangusha ufalme wake na wakuu wake

chini kwa aibu.

32:3 Za 75:5; 74:11; Isa 42:25; Ay 16:15; Yer 21:4-5Katika hasira kali amevunja

kila pembe2:3 Pembe inawakilisha nguvu; pia 2:17. ya Israeli.

Ameuondoa mkono wake wa kuume

alipokaribia adui.

Amemteketeza Yakobo kama moto uwakao

ule uteketezao kila kitu kinachouzunguka.

42:4 Isa 63:10; Ay 3:23; Mao 3:12-13; Yer 7:20; Eze 24:16; 2Nya 34:21; Eze 20:34Ameupinda upinde wake kama adui,

mkono wake wa kuume uko tayari.

Kama vile adui amewachinja

wote waliokuwa wanapendeza jicho,

amemwaga ghadhabu yake kama moto

juu ya hema la Binti Sayuni.

52:5 Yer 30:14; Ay 13:24; Yer 9:17-20; Isa 29:2; Yer 7:20Bwana ni kama adui;

amemmeza Israeli.

Amemeza majumba yake yote ya kifalme

na kuangamiza ngome zake.

Ameongeza huzuni na maombolezo

kwa ajili ya Binti Yuda.

62:6 Yer 52:13; Sef 3:18; Yer 7:14; Isa 43:28; Mao 4:16; 5:12; Za 80:12; Isa 5:5; 1:8Ameharibu maskani yake kama bustani,

ameharibu mahali pake pa mkutano.

Bwana amemfanya Sayuni kusahau

sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake;

katika hasira yake kali amewadharau

mfalme na kuhani.

72:7 Eze 7:1-2; Isa 64:10-11; Yer 7:12-14; Law 26:31; Yer 33:4-5; 52:13; Za 78:59-61; Mik 3:12; Yer 7:12-14; Mt 24:2Bwana amekataa madhabahu yake

na kuacha mahali patakatifu pake.

Amemkabidhi adui kuta

za majumba yake ya kifalme;

wamepiga kelele katika nyumba ya Bwana

kama katika siku ya sikukuu iliyoamriwa.

82:8 2Fal 21:13; Isa 34:11; 3:26; Yer 39:8; Za 48:13; Amu 7:7Bwana alikusudia kuangusha

ukuta uliomzunguka Binti Sayuni.

Ameinyoosha kamba ya kupimia

na hakuuzuia mkono wake usiangamize.

Alifanya maboma na kuta ziomboleze,

vyote vikaharibika pamoja.

92:9 Yer 16:13; Amo 8:11-12; Hos 3:4; 2Nya 15:3; Yer 14:14; Isa 45:2; 2Fal 24:15; Kum 28:36; 2Fal 25:7; Za 74:9; Mik 3:6, 7Malango yake yamezama ardhini,

makomeo yake ameyavunja na kuyaharibu.

Mfalme wake na wakuu wake wamepelekwa uhamishoni

miongoni mwa mataifa,

sheria haipo tena,

na manabii wake hawapati tena

maono kutoka kwa Bwana.

102:10 Ay 2:12-13; Isa 3:24, 26; Eze 27:30-31; Isa 15:3; Mao 3:28; 4:5; Isa 47:1-5Wazee wa Binti Sayuni

wanaketi chini kimya,

wamenyunyiza mavumbi kwenye vichwa vyao

na kuvaa nguo za gunia.

Wanawali wa Yerusalemu

wamesujudu hadi ardhini.

112:11 Isa 15:3; Ay 30:27; Za 22:14; Ay 16:13; Mao 3:48-51; Za 119:82; 6:7Macho yangu yamedhoofika kwa kulia,

nina maumivu makali ndani,

moyo wangu umemiminwa ardhini

kwa sababu watu wangu wameangamizwa,

kwa sababu watoto na wanyonyao wanazimia

kwenye barabara za mji.

12Wanawaambia mama zao,

“Wapi mkate na divai?”

wazimiapo kama watu waliojeruhiwa

katika barabara za mji,

maisha yao yadhoofikavyo

mikononi mwa mama zao.

132:13 Isa 37:22; Yer 14:17; 30:12-15; Dan 9:12; 2Fal 19:2; Ay 5:1Ninaweza kusema nini kwa ajili yako?

Nikulinganishe na nini,

ee Binti Yerusalemu?

Nitakufananisha na nini,

ili nipate kukufariji,

ee Bikira Binti Sayuni?

Jeraha lako lina kina kama bahari.

Ni nani awezaye kukuponya?

142:14 Isa 58:1; Yer 8:11; 20:6; Eze 13:3; Yer 28:3; 28:15; Eze 22:28Maono ya manabii wako

yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu,

hawakuifunua dhambi yako

ili kukuzuilia kwenda utumwani.

Maneno waliyokupa

yalikuwa ya uongo na ya kupotosha.

152:15 Hes 24:20; Eze 25:6; Nah 3:19; Za 45:11; Eze 16:14; Za 48:2; Yer 19:8; 1Fal 9:8Wote wapitiao njia yako

wanakupigia makofi,

wanakudhihaki na kutikisa vichwa vyao

kwa Binti Yerusalemu:

“Huu ndio ule mji ulioitwa

mkamilifu wa uzuri,

furaha ya dunia yote?”

162:16 Za 22:13; 56:2; Ay 16:19; Za 35:25; Eze 36:3; Mao 3:46Adui zako wote wanapanua

vinywa vyao dhidi yako,

wanadhihaki na kusaga meno yao

na kusema, “Tumemmeza.

Hii ndiyo siku tuliyoingojea,

tumeishi na kuiona.”

172:17 Kum 28:15-45; Eze 8:18; Isa 44:26; Mao 1:5; Law 26:16; Za 38:16Bwana amefanya lile alilolipanga;

ametimiza neno lake

aliloliamuru siku za kale.

Amekuangusha bila huruma,

amewaacha adui wakusimange,

ametukuza pembe ya adui yako.

182:18 Za 119:145; Mao 1:16; 3:19; Yer 9:1; 14:7Mioyo ya watu

inamlilia Bwana.

Ee ukuta wa Binti Sayuni,

machozi yako na yatiririke kama mto

usiku na mchana;

usijipe nafuu,

macho yako yasipumzike.

192:19 Mk 13:35; 1Sam 1:15; Za 62:8; Isa 51:20; Neh 3:10; Isa 26:9; Mao 4:1Inuka, lia usiku,

zamu za usiku zianzapo;

mimina moyo wako kama maji

mbele za Bwana.

Mwinulie yeye mikono yako

kwa ajili ya maisha ya watoto wako,

ambao wanazimia kwa njaa

kwenye kila mwanzo wa barabara.

202:20 Kum 28:53; Eze 5:10; Mao 4:10; Yer 23:11-12; 19:9; Za 78:64; Yer 14:15; Kut 32:11; Law 26:29“Tazama, Ee Bwana, ufikirie:

Ni nani ambaye umepata

kumtendea namna hii?

Je, wanawake wakule wazao wao,

watoto waliowalea?

Je, kuhani na nabii auawe

mahali patakatifu pa Bwana?

212:21 Kum 32:25; 2Nya 36:17; Yer 13:14; Zek 11:6“Vijana na wazee hujilaza pamoja

katika mavumbi ya barabarani,

wavulana wangu na wasichana

wameanguka kwa upanga.

Umewaua katika siku ya hasira yako,

umewachinja bila huruma.

222:22 Za 31:13; Yer 6:25; Ay 27:14; Hes 9:13; Yer 20:10“Kama ulivyoita siku ya karamu,

ndivyo ulivyoagiza hofu kuu

dhidi yangu kila upande.

Katika siku ya hasira ya Bwana

hakuna yeyote aliyekwepa au kupona;

wale niliowatunza na kuwalea,

adui yangu amewaangamiza.”