Malaki 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Malaki 4:1-6

Siku Ya Bwana

14:1 Isa 2:12; 5:24; 1:31; 2Fal 10:11; Nah 1:10; Eze 17:8; Mt 3:10“Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao. 24:2 Kum 28:58; 2Pet 1:19; Za 61:5; 111:9; 118:27; 2Nya 7:14; Ufu 14:1; 22:2; Isa 9:2; 45:8; 30:26; Lk 1:78; Efe 5:14; Mt 4:23Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini. 34:3 Ay 40:12; Za 18:40-42; Eze 28:18; Mik 7:10Kisha ninyi mtawakanyaga waovu, nao watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku ile nitakayofanya mambo haya,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

44:4 Kum 28:61; 4:10; Za 147:19; Mt 5:17; 7:12; Rum 2:13; 4:15“Kumbukeni sheria ya mtumishi wangu Mose, amri na sheria nilizompa huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote.

54:5 1Fal 17:1; Yoe 2:31; Mt 11:14; 16:14“Tazama, nitawapelekea nabii Eliya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana. 64:6 Dan 9:26; Lk 19:27, 43; 21:20; Mk 13:14; Lk 1:17; Zek 5:3; Isa 11:4; Ufu 19:15; Kum 13:15; Yos 6:17; 23:15; 4:2Ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, la sivyo nitakuja na kuipiga nchi kwa laana.”