Malaki 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Malaki 3:1-18

13:1 Hes 27:21; 2Nya 36:15; Isa 40:3; 63:9; Mt 11; 10; 3:3; Lk 7:27; Mik 5:2; 1Sam 9:20; Mdo 7:38; Hag 2:7“Angalieni, nitamtuma mjumbe wangu, atakayeiandaa njia mbele yangu. Ndipo ghafula Bwana mnayemtafuta atakuja hekaluni mwake. Mjumbe wa Agano, ambaye mnamwonea shauku, atakuja,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

23:2 Eze 7:7; 22:14; Ufu 6:17; Dan 7:13; Yoe 2:31; Mt 16:27; Yak 5:8; 2Pet 3:4; 1Sam 6:20; Isa 1:31; 30:30; 4:4; Zek 13:9; Mt 3:10-12; Ay 9:30Lakini ni nani atakayeweza kustahimili hiyo siku ya kuja kwake? Ni nani awezaye kusimama atakapotokea? Kwa kuwa atakuwa kama moto wa mfua fedha au kama sabuni ya afuaye nguo. 33:3 Eze 12:10; 1Kor 3:13; 1Nya 23:28; Isa 1:25; Ay 28:1; Za 12:6; 132:9; Ufu 3:18; Zek 13:9; Rum 15:16; 1Pet 2:5Ataketi kama mfuaji na asafishaye fedha. Atawatakasa Walawi, naye atawasafisha kama dhahabu na fedha. Kisha Bwana atakuwa na watu watakaoleta sadaka katika haki, 43:4 2Nya 7:3; 7:12; Za 51:19; Eze 20:40; Mal 1:11nazo sadaka za Yuda na Yerusalemu zitakubalika kwa Bwana, kama katika siku zilizopita, kama katika miaka ya zamani.

53:5 Kut 7:11; 20:14; Yak 2:11; 5:4-9; Isa 1:2; 47:9; 2Pet 2:12-14; Law 19:11-13; Yer 7:9; Yak 5:4; Kut 22:21-22; Kum 24:19; 31:12; Eze 22:7“Basi nitakuja karibu nanyi ili kuhukumu. Nami nitakuwa mwepesi kushuhudia dhidi ya wachawi, wazinzi, waapao kwa uongo, wanaopunja vibarua malipo yao, wanaowaonea wajane na yatima, na wanaowanyima wageni haki, lakini hawaniogopi mimi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

Kumwibia Mungu

63:6 Hes 23:19; Ebr 7:21; Yak 1:17; Ay 34:15; Hos 11:9; 1Sam 15:29; Rum 11:29; Mao 3:22“Mimi Bwana sibadiliki. Kwa hiyo ninyi, enyi uzao wa Yakobo, hamjaangamizwa. 73:7 Kut 32:8; Mdo 7:51; Yer 7:26; Isa 44:22; Kum 30:1-4; Isa 55:6-7; Eze 18:32; Yak 4:8; Zek 1:3Tangu wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

“Lakini mnauliza, ‘Tutarudi kwa namna gani?’

83:8 Zek 5:3; Law 27:30; Hes 18:21; Neh 13:10-12; Lk 18:12“Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia mimi.

“Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’

“Mnaniibia zaka na dhabihu. 93:9 Kum 28:15-68; 11:26; Zek 5:3Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi. 103:10 Kut 22:29; Neh 13:12; 2Fal 7:2; Isa 44:3; Yoe 2:14, 24; 2Kor 9:8-11; Law 25:21; Mit 3:9; Mwa 7:11; 1Nya 26:29Leteni zaka kamili ghalani, ili kuwe na chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, “nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha. 113:11 Kut 10:15; 23:26; Kum 28:39; Amo 4:9Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 123:12 Kum 28:3-12; Isa 61:9; 62:4; Eze 20:6; Dan 8:9; 2Nya 31:10“Ndipo mataifa yote yatawaita mliobarikiwa, kwa maana nchi yenu itakuwa ya kupendeza sana,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

133:13 Mal 2:17“Mmesema vitu vigumu dhidi yangu,” asema Bwana.

“Hata hivyo mnauliza, ‘Tumesema nini dhidi yako?’

143:14 Za 73:13; 100:2; Isa 1:14; 57:10; 58:3; Yn 12:26; Rum 12:11; Yos 22:5; Sef 1:12; Ay 21:14“Mmesema, ‘Ni bure kumtumikia Mungu. Tumepata faida gani kwa kushika maagizo yake na kwenda kama waombolezaji mbele za Bwana Mwenye Nguvu Zote? 153:15 Za 119:21; 14:1; 36:1-2; Yer 7:10; Ay 21:7Lakini sasa wenye kiburi wanabarikiwa. Hakika watenda mabaya wanastawi, pia hata wale wanaoshindana na Mungu ndio wanaosalimika.’ ”

163:16 Za 34:15; 56:8; 87:6; 33:18; Kut 32:32; Lk 10:20; Mit 1:7; Ebr 3:13; Kum 31:12; Ufu 11:18; Mwa 22:12; 1Fal 18:3, 12Ndipo wale waliomcha Bwana wakasemezana wao kwa wao, naye Bwana akasikiliza na akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimcha Bwana na kuliheshimu jina lake.

173:17 Isa 43:21; 26:20; Kut 8:22; Kum 7:6; Tit 2:14; Neh 13:22; Rum 8:14, 32; Za 103:13; Lk 15:1-32“Nao watakuwa watu wangu,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, “katika siku ile nitakapowafanya watu kuwa hazina yangu. Nitawahurumia, kama vile kwa huruma mtu amhurumiavyo mwanawe anayemtumikia. 183:18 Mwa 18:25; Kum 32:4; Mt 25:32-33Kwa mara nyingine tena utaona tofauti kati ya wenye haki na waovu, kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia.