Luka 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Luka 4:1-44

Yesu Ajaribiwa Na Shetani

(Mathayo 4:1-11; Marko 1:12-13)

14:1 Lk 1:15-45; 3:3-21; Eze 37:1; Lk 2:27Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani. Akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi nyikani, 24:2 Kut 34:28; 1Fal 19:8mahali ambako kwa siku arobaini alikuwa akijaribiwa na ibilisi. Kwa siku zote hizo hakula chochote, hivyo baada ya muda huo akaona njaa.

34:3 Mt 4:3Ibilisi akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”

44:4 Kum 8:3Yesu akajibu akamwambia, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’ ”

54:5 Mt 24:14Ibilisi akampeleka hadi juu ya mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia kwa mara moja. 64:6 Yn 14:30Akamwambia, “Nitakupa mamlaka juu ya milki hizi na fahari zake zote, kwa maana zimekabidhiwa mkononi mwangu nami ninaweza kumpa yeyote ninayetaka. 7Hivyo ikiwa utanisujudia na kuniabudu, vyote vitakuwa vyako.”

84:8 Kum 6:3Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake.’ ”

94:9 Mt 4:5Kisha ibilisi akampeleka mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa, 104:10 Za 91:11, 12kwa maana imeandikwa:

“ ‘Atakuagizia malaika zake

ili wakulinde;

114:11 Za 91:12nao watakuchukua mikononi mwao,

usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”

124:12 Kum 6:12Yesu akamjibu, “Imesemwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”

134:13 Ebr 4:15; Yn 14:30Ibilisi alipomaliza kila jaribu, akamwacha Yesu mpaka wakati mwingine ufaao.

Mwanzo Wa Huduma Ya Galilaya

(Mathayo 4:12-17; Marko 1:14-15)

144:14 Mt 4:12; 9:26Kisha Yesu akarudi mpaka Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando. 154:15 Mt 4:23Akaanza kufundisha kwenye masinagogi yao, na kila mmoja akamsifu.

Yesu Akataliwa Nazareti

(Mathayo 13:53-58; Marko 6:1-6)

164:16 Mt 2:23; 13:54Yesu akaenda Nazareti, alipolelewa, na siku ya Sabato alikwenda katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome, 174:17 Isa 61:1, 2; 58:6naye akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na kukuta mahali palipoandikwa:

184:18 Yn 3:34“Roho wa Bwana yu juu yangu,

kwa sababu amenitia mafuta

kuwahubiria maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao,

na vipofu kupata kuona tena,

kuwaweka huru wanaoonewa,

19na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika.”

204:20 Mt 26:55Kisha akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi na akaketi. Watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 214:21 Mt 1:22Ndipo akaanza kwa kuwaambia, “Leo Andiko hili limetimia mkiwa mnasikia.”

224:22 Yn 6:42; 7:15Wote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake yaliyojaa neema, wakaulizana, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”

234:23 Mt 2:23; Mk 1:21-28; 2:1-12Yesu akawaambia, “Bila shaka mtatumia mithali hii: ‘Tabibu, jiponye mwenyewe! Mambo yale tuliyosikia kwamba uliyafanya huko Kapernaumu, yafanye na hapa kwenye mji wako.’ ”

244:24 Mt 13:57; Yn 4:44Yesu akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika katika mji wake mwenyewe. 254:25 1Fal 18:1; Ufu 11:6Lakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Eliya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima. 264:26 1Fal 17:8-16; Mt 11:21Hata hivyo Eliya hakutumwa hata kwa mmoja wao, bali kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. 274:27 2Fal 5:1-14Pia palikuwa na wengi wenye ukoma katika Israeli katika siku za nabii Elisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyetakaswa, isipokuwa Naamani mtu wa Shamu.”4:27 Shamu hapa inamaanisha Syria.

28Watu wote katika sinagogi waliposikia maneno haya, wakakasirika sana. 294:29 Hes 15:35; Ebr 13:12Wakasimama, wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hadi kwenye kilele cha mlima mahali ambapo mji huo ulikuwa umejengwa, ili wamtupe chini kutoka kwenye mteremko mkali. 304:30 Yn 8:59; 10:39Lakini yeye akapita papo hapo katikati ya huo umati wa watu akaenda zake.

Yesu Atoa Pepo Mchafu

(Marko 1:21-28)

314:31 Mt 4:13Kisha Yesu akashuka kwenda Kapernaumu, mji wa Galilaya, na katika siku ya Sabato akawa anafundisha. 324:32 Mt 7:28-29Wakashangazwa sana na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka.

334:33 Mk 1:23Ndani ya sinagogi palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu. Naye akapiga kelele kwa nguvu akisema, 344:34 Mt 8:28-29; Mk 1:24; Yak 2:19“Tuache! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!”

354:35 Mt 8:26; Lk 8:24Basi Yesu akamkemea yule pepo mchafu, akisema, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” Yule pepo mchafu akamwangusha yule mtu chini mbele yao wote, akatoka pasipo kumdhuru. 364:36 Mt 7:28-29; 10:1Watu wote wakashangaa, wakaambiana, “Mafundisho haya ni ya namna gani? Anawaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na nguvu, nao wanatoka!” 374:37 Mt 9:26Habari zake zikaanza kuenea kila mahali katika sehemu ile.

Yesu Awaponya Wengi

(Mathayo 8:14-17; Marko 1:29-34)

384:38 Mt 8:14; Mk 1:29Yesu akatoka katika sinagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni. Basi huko alimkuta mama mkwe wa Simoni akiwa ameshikwa na homa kali, nao wakamwomba Yesu amsaidie. 394:39 Lk 4:35, 41Hivyo Yesu akamwinamia na kukemea ile homa, nayo ikamwacha. Akaamka saa ile ile, naye akaanza kuwahudumia.

404:40 Mk 5:23; Mt 4:23Jua lilipokuwa linatua, watu wakamletea Yesu watu wote waliokuwa na maradhi mbalimbali, naye akaweka mikono yake juu ya kila mgonjwa, naye akawaponya. 414:41 Mt 4:3; 8:4Pepo wachafu pia wakawatoka watu wengi, nao walipokuwa wakitoka wakapiga kelele, wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea na kuwazuia wasiseme, kwa maana walimjua kuwa yeye ndiye Kristo.4:41 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.

424:42 Mk 1:35Kesho yake, kulipopambazuka, Yesu alikwenda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, nao walipomwona wakajaribu kumzuia asiondoke. 434:43 Mt 3:2Lakini yeye akawaambia, “Imenipasa kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, kwa maana kwa kusudi hili nilitumwa.” 444:44 Mt 4:23Naye aliendelea kuhubiri katika masinagogi ya Uyahudi.