Luka 23 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Luka 23:1-56

Yesu Apelekwa Kwa Pilato

(Mathayo 27:1-14; Marko 15:1-5; Yohana 18:28-38)

123:1 Mk 15:1; Yn 18:28Kisha umati wote wa watu ukainuka na kumpeleka Yesu kwa Pilato. 223:2 Lk 20:22; Yn 18:28Nao wakaanza kumshtaki wakisema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu, akiwazuia watu wasilipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo,23:2 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. mfalme.”

323:3 Mt 27:11; 1Tim 6:13Basi Pilato akamuuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”

Yesu akajibu, “Wewe wasema.”

423:4 1Tim 6:13; 2Kor 5:21Pilato akawaambia viongozi wa makuhani na watu wote waliokuwepo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki mtu huyu!”

523:5 Mk 1:14Lakini wao wakakazana kusema, “Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika Uyahudi yote, tangu Galilaya alikoanzia, hadi sehemu hii!”

Yesu Apelekwa Kwa Herode

623:6 Lk 22:59Pilato aliposikia hayo akauliza, “Huyu mtu ni Mgalilaya?” 723:7 Mk 14:1; Lk 3:1Alipofahamu kwamba Yesu alikuwa chini ya mamlaka ya Herode, akampeleka kwa Herode, ambaye wakati huo alikuwa pia Yerusalemu.

823:8 Lk 9:9Herode alipomwona Yesu alifurahi sana, kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amesikia mambo mengi kumhusu yeye. Pia alitarajia kumwona akifanya miujiza kadha wa kadha. 923:9 Mk 14:61Herode akamuuliza maswali mengi, lakini Yesu hakumjibu lolote. 10Wakati huo viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwepo wakitoa mashtaka yao kwa nguvu sana. 1123:11 Mk 15:17-19; Yn 19:2-3Herode na askari wake wakamdhihaki Yesu na kumfanyia mzaha. Wakamvika vazi zuri sana, wakamrudisha kwa Pilato. 1223:12 Mdo 4:27Siku hiyo, Herode na Pilato wakawa marafiki; kabla ya jambo hili walikuwa na uadui kati yao.

Yesu Ahukumiwa Kifo

(Mathayo 27:15-26; Marko 15:6-15; Yohana 18:39–19:16)

1323:13 Mt 27:23; Mk 15:14; Yn 18:38Basi Pilato akawaita pamoja viongozi wa makuhani, viongozi wengine na watu, 1423:14 Lk 23:1, 2, 4akawaambia, “Ninyi mlimleta huyu mtu kwangu kana kwamba ni mtu anayewachochea watu ili waasi. Nimemhoji mbele yenu nami nimeona hakuna msingi wowote wa mashtaka yenu dhidi yake. 15Wala Herode hakumwona na kosa lolote, ndiyo sababu amemrudisha kwetu. Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lolote linalostahili kifo. 1623:16 Mdo 16:37; 2Kor 11:23-24Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi na kumwachia.” [ 1723:17 Mt 27:15; Mk 15:6; Yn 18:39Kwa kuwa ilikuwa lazima kuwafungulia mfungwa mmoja wakati wa Sikukuu.]

1823:18 Mdo 3:13-14Ndipo watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “Mwondoe mtu huyo! Tufungulie Baraba!” 19(Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa sababu ya maasi yaliyokuwa yametokea mjini, na kwa ajili ya uuaji.)

20Pilato, akitaka kumwachia Yesu, akasema nao tena. 21Lakini wao wakaendelea kupiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!”

2223:22 Lk 23:18Kwa mara ya tatu, Pilato akawauliza, “Kwani amefanya kosa gani huyu mtu? Sikuona kwake sababu yoyote inayostahili adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi, na kisha nitamwachia.”

23Lakini watu wakazidi kupiga kelele kwa nguvu zaidi, wakidai kwamba Yesu asulubiwe. Hivyo, kelele zao zikashinda. 2423:24 Mt 27:26; Mk 15:15; Yn 19:17Kwa hiyo Pilato akatoa hukumu kwamba madai yao yatimizwe. 25Akamfungua yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika uasi dhidi ya serikali na mauaji. Akamkabidhi Yesu mikononi mwao, wamfanyie watakavyo.

Kusulubiwa Kwa Yesu

(Mathayo 27:32-44; Marko 15:21-32; Yohana 19:17-27)

2623:26 Mt 27:32; Mk 15:21; Yn 19:17Walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni mwenyeji wa Kirene, aliyekuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Yesu. 2723:27 Lk 8:52Idadi kubwa ya watu wakamfuata Yesu, wakiwamo wanawake waliokuwa wakimlilia na kumwombolezea. 2823:28 Lk 19:41-44; 21:23-24Yesu akawageukia, akawaambia, “Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi bali jililieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 2923:29 Mt 24:19Kwa maana wakati utafika mtakaposema, ‘Wamebarikiwa wanawake tasa, ambao matumbo yao hayakuzaa, wala matiti yao hayakunyonyesha!’ 3023:30 Hos 10:8; Ufu 6:16Ndipo

“ ‘wataiambia milima, “Tuangukieni!”

na vilima, “Tufunikeni!” ’

3123:31 Eze 20:47Kwa maana kama wamefanya hivi kwa mti mbichi, kwa mti mkavu itakuwaje?”

3223:32 Isa 53:12; Mt 27:38Watu wengine wawili wahalifu, walipelekwa pamoja na Yesu ili wakasulubiwe. 33Walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, hapo ndipo walipomsulubisha Yesu pamoja na hao wahalifu, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wake wa kushoto. 3423:34 Mt 11:25; 5:44; Za 22:18Yesu akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.

3523:35 Za 22:17; Isa 42:1; Zek 12:10; Mt 27:39; Mk 15:29Watu wakasimama hapo wakimwangalia, nao viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.”

3623:36 Za 22:7; 69:21; Mt 27:48Askari nao wakaja, wakamdhihaki. Wakamletea siki ili anywe, 3723:37 Lk 4:3, 9na wakamwambia, “Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.”

3823:38 Mt 2:2Kwenye msalaba juu ya kichwa chake, kulikuwa na maandishi haya: Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi.

Maandishi haya yalikuwa yameandikwa kwa lugha za Kiyunani, Kilatini na Kiebrania.

3923:39 Mt 27:44; Mk 15:32Mmoja wa wale wahalifu waliosulubiwa pamoja naye akamtukana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe mwenyewe na utuokoe na sisi.”

40Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akasema, “Je, wewe humwogopi Mungu, wakati uko kwenye adhabu iyo hiyo? 4123:41 Lk 23:4Sisi tumehukumiwa kwa haki kwa kuwa tunapata tunayostahili kwa ajili ya matendo yetu. Lakini huyu mtu hajafanya kosa lolote.”

4223:42 Mt 16; 27Kisha akasema, “Yesu, unikumbuke utakapokuja katika Ufalme wako.”

4323:43 1Kor 12:3-4; Ufu 2:7Yesu akamjibu, “Amin, nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso.”23:43 Paradiso maana yake bustani nzuri, hapa ina maana mahali zinapokwenda roho za wacha Mungu, yaani watakatifu.

Kifo Cha Yesu

(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Yohana 19:28-30)

4423:44 Amo 8:9Ilikuwa kama saa sita mchana, nalo giza likafunika nchi yote hadi saa tisa, 4523:45 Kut 26:31-33; Ebr 3:8; 10:19-20kwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili. 4623:46 Mt 27:50; Za 31:5; 1Pet 2:23; Yn 19:30Yesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.

4723:47 Mt 9:8Yule jemadari alipoona yaliyotukia, akamsifu Mungu, akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 4823:48 Lk 18:13Watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hili walipoyaona hayo, wakapigapiga vifua vyao kwa huzuni na kwenda zao. 4923:49 Lk 8:2; Za 38:11Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wale wanawake waliokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyatazama mambo haya.

Maziko Ya Yesu

(Mathayo 27:57-61; Marko 15:42-47; Yohana 19:38-42)

5023:50 Mt 27:59; Mk 15:46Basi kulikuwa na mtu mmoja mwema na mwenye haki, jina lake Yosefu. Yeye alikuwa mjumbe wa Baraza la Wayahudi,23:50 Baraza la Wayahudi hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. 5123:51 Lk 2:25, 38lakini yeye hakuwa amekubaliana na maamuzi na vitendo vya viongozi wenzake. Huyu alikuwa mwenyeji wa Arimathaya huko Uyahudi, naye alikuwa anaungojea Ufalme wa Mungu kwa matarajio makubwa. 52Yosefu alikwenda kwa Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. 53Akaushusha kutoka msalabani, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, na kuuweka katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limezikiwa mtu mwingine bado. 5423:54 Mt 27:62Ilikuwa Siku ya Maandalizi, nayo Sabato ilikuwa karibu kuanza.

5523:55 Lk 8:2; Mk 15:47Wale wanawake waliokuwa wamekuja pamoja na Yesu wakimfuata kutoka Galilaya wakamfuata Yosefu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa. 5623:56 Mk 16:1; Lk 24:1; Kut 12:16; 20:11Kisha wakarudi nyumbani, wakaandaa manukato na marhamu ya kuupaka huo mwili. Lakini wakapumzika siku ya Sabato kama ilivyoamriwa.