Luka 21 – NEN & HHH

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Luka 21:1-38

Sadaka Ya Mjane

(Marko 12:41-44)

121:1 Mt 27:6; Yn 8:20Yesu alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. 2Akamwona pia mjane mmoja maskini akiweka humo sarafu mbili ndogo za shaba. 321:3 2Kor 8:12Yesu akasema, “Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo zaidi ya watu wengine wote. 421:4 2Kor 8:12Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kutokana na wingi wa mali zao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo, hata kile alichohitaji ili kuishi.”

Dalili Za Siku Za Mwisho

(Mathayo 24:1-2; Marko 13:1-2)

5Baadhi ya wanafunzi wake wakawa wanamwonyesha jinsi Hekalu lilivyopambwa kwa mawe mazuri na kwa vitu vilivyotolewa kuwa sadaka kwa Mungu. Lakini Yesu akawaambia, 621:6 Lk 19:44“Kuhusu haya mnayoyaona hapa, wakati utafika ambapo hakuna jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.”

Mateso

(Mathayo 24:3-14; Marko 13:3-13)

7Wakamuuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatukia lini? Ni dalili gani itaonyesha kwamba yanakaribia kutendeka?”

821:8 Lk 17:23Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye,’ na, ‘Wakati umekaribia.’ Msiwafuate. 921:9 Dan 2:28Lakini msikiapo habari za vita na machafuko, msiogope. Kwa maana hayo ni lazima yatokee kwanza, ila ule mwisho hautakuja wakati huo.”

1021:10 2Nya 15:6; Isa 19:2Kisha akawaambia: “Taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme mmoja dhidi ya ufalme mwingine. 1121:11 Isa 29:6; Yoe 2:30Kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, na njaa kali, na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali. Pia kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.

1221:12 Lk 12:11; Mk 13:9; Ufu 2:10; Mdo 1:3; 5:18; 12:4; 16:24; 25:23; 1Pet 2:13“Lakini kabla yote hayajatokea, watawakamata ninyi na kuwatesa. Watawatia mikononi mwa wakuu wa masinagogi na kuwafunga magerezani. Nanyi mtapelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya Jina langu. 1321:13 Flp 1:12Hii itawapa nafasi ya kushuhudia. 1421:14 Lk 12:11-12Lakini kusudieni mioyoni mwenu msisumbuke awali kuhusu mtakalosema mbele ya mashtaka. 1521:15 Mdo 6:10Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo hakuna hata adui yenu mmoja atakayeweza kushindana nayo wala kuipinga. 1621:16 Lk 12:52-53Mtasalitiwa hata na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki, na baadhi yenu watawaua. 1721:17 Yn 15:21Mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu. 1821:18 Mt 10:30Lakini hapatakuwa na unywele mmoja wa kichwa chenu utakaoangamia. 1921:19 Mt 10:22Kwa kuvumilia mtaokoa roho zenu.

Kuharibiwa Kwa Yerusalemu Kwatabiriwa

(Mathayo 24:15-21; Marko 13:14-19)

2021:20 Lk 19:43“Mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, basi fahamuni kwamba kuharibiwa kwake kumekaribia. 2121:21 Lk 17:31Wakati huo, wale walio Uyahudi wakimbilie milimani, walio mjini Yerusalemu watoke humo, nao wale walioko mashambani wasiingie mjini. 2221:22 Dan 9:24-27; Hos 9:7; Mk 1:22Kwa sababu huu utakuwa ni wakati wa adhabu ili kutimiza yote yaliyoandikwa. 2321:23 Mt 24:19Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! Kutakuwa na dhiki kuu katika nchi na ghadhabu juu ya hawa watu. 2421:24 Dan 8:13; Ufu 11:2Wataanguka kwa makali ya upanga, na wengine watachukuliwa kuwa mateka katika mataifa yote. Nao mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa Mataifa hadi muda wa hao watu wa Mataifa utimie.

Kuja Kwa Mwana Wa Adamu

(Mathayo 24:29-35; Marko 13:24-31)

2521:25 2Pet 3:10-12“Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Hapa duniani, mataifa yatakuwa katika dhiki na fadhaa kutokana na ngurumo na misukosuko ya bahari. 2621:26 Mt 24:29Watu watazimia roho kutokana na hofu kuu na kuyaona yale mambo yanayotokea duniani, kwa maana nguvu za angani zitatikisika. 2721:27 Mt 8:20; Ufu 1:7Wakati huo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na uweza na utukufu mkuu. 2821:28 Lk 18:7Mambo haya yatakapoanza kutendeka, simameni na mkaviinue vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umekaribia.”

2921:29 Mt 24:32; Mk 12:28Akawaambia mfano huu: “Uangalieni mtini na miti mingine yote. 30Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia. 3121:31 Mt 3:2Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.

3221:32 Lk 11:50; 11:25“Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 3321:33 Mt 5:18Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”

Siku Ya Mwisho Itakuja Ghafula

3421:34 Mk 4:19; Lk 12:40-46; 1The 5:2-7“Jihadharini mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na fadhaa za maisha haya, nayo siku ile ikawakuta ninyi bila kutazamia kama vile mtego unasavyo. 3521:35 1The 5:2; 2Pet 3:10; Ufu 3:3; 16:15Kwa maana kama vile mtego unasavyo, ndivyo siku hiyo itakavyowapata wanadamu wote waishio katika uso wa dunia yote. 3621:36 Mt 26:41Kesheni daima na mwombe ili mweze kuokoka na yale yote yatakayotokea na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu.”

3721:37 Mt 26:55; 21:1Kila siku Yesu alikuwa akifundisha Hekaluni, na jioni ilipofika, alikwenda zake kwenye Mlima wa Mizeituni na kukaa huko usiku kucha. 3821:38 Yn 8:2Nao watu wote walikuja asubuhi na mapema Hekaluni ili kumsikiliza.

Habrit Hakhadasha/Haderekh

הבשורה על-פי לוקס 21:1-38

1ישוע עמד בבית־המקדש והביט בעשירים שמביאים את תרומותיהם אל תיבת האוצר. 2בין התורמים הרבים הבחין גם באלמנה עניה שתרמה שתי פרוטות.

3”אומר לכם את האמת,“ העיר ישוע, ”האלמנה הענייה הזאת תרמה יותר מכל העשירים האלה גם יחד! 4כי העשירים תרמו סכומים קטנים ביחס לרכוש הרב שיש להם, ואילו האלמנה הזאת נתנה את כל מה שהיה לה.“

5אחדים מתלמידיו העירו את תשומת לבו לעבודת האבנים המהודרת של בית־המקדש, ולחפצים היקרים שתרמו האנשים.

6”אתם יכולים להתפעל מהמראה בינתיים,“ אמר להם ישוע, ”אולם יבוא היום שהכול ייהרס; אף אבן לא תישאר במקומה.“

7”רבי, מתי יקרה הדבר?“ שאלו התלמידים. ”האם נקבל אזהרה מראש?“ 8השיב ישוע: ”אל תניחו לאיש לרמות אתכם. אנשים רבים יבואו ויטענו כי הם המשיח, ויודיעו שהקץ קרוב. אבל אל תאמינו להם. 9כאשר תשמעו על מהומות ומלחמות, אל תיבהלו ואל תאבדו את עשתונותיכם. כי אמנם תפרוצנה מלחמות, אבל הקץ לא יבוא מיד. 10מדינות וממלכות תילחמנה זו בזו, 11בארצות רבות תתחוללנה רעידות אדמה אדירות ומגפות, ויהיה רעב גדול; בשמים ייראו מראות נוראים ואותות גדולים.

12”אולם לפני שיתרחשו כל הדברים האלה ירדפו אתכם, ישפטו אתכם בבתי־כנסת, ישליכו אתכם לכלא ויעמידו אתכם לפני מלכים ושליטים למען שמי. 13זאת תהיה הזדמנות עבורכם להעיד עלי. 14אל תדאגו כיצד תתגוננו בפני האשמותיהם, 15כי אשים בפיכם את המילים המתאימות, ואתן לכם חכמה שאויביכם לא יוכלו להתמודד איתה ולסתור אותה. 16גם האנשים הקרובים אליכם ביותר – הוריכם, אחיכם, חבריכם וקרובי משפחתכם – יבגדו בכם ויביאו למאסרכם, ויהיו ביניכם כאלה שימותו. 17כולם ישנאו אתכם משום שאתם שייכים לי, 18אולם אף שערה אחת לא תיפול מראשכם! 19בנאמנותכם ובעמידתכם האיתנה תושיעו את נפשותיכם.

20”כאשר תראו את ירושלים מוקפת אויבים דעו שחורבנה קרוב. 21אז תושבי יהודה יברחו אל ההרים; על תושבי ירושלים להשתדל לברוח מהעיר, ואוי לתושבי הסביבה שינסו להיכנס לירושלים! 22יהיו אלה ימי נקם אשר נועדו לקיים את נבואות התנ״ך. 23אוי לנשים ההרות ולמניקות באותם ימים, מפני שצרה גדולה תבוא על הארץ, ואלוהים ישפוך את זעמו על העם הזה. 24רבים ייהרגו בחרב האויב או יוגלו לכל קצוות תבל, וירושלים תיפול בידי גויים אשר ידכאו אותה עד שתסתיים תקופת שלטון הגויים במועד שקבע ה׳.

25”אותות מבשרי רעה יופיעו בשמש, בירח ובכוכבים, ואילו על פני האדמה – עמים שלמים יתייאשו ויפחדו מגעש הים והגלים הסוערים. 26אנשים יתעלפו מאימה ופחד מפני המאורעות שיבואו על העולם, משום שכוחות השמים יתמוטטו. 27ואז יראו אנשי הארץ את בן־האדם בא בענן, בגבורה ובכבוד רב.21‏.27 כא 27 דניאל ז 13‏-14 28כאשר יתחילו כל הדברים האלה להתרחש, התעודדו והרימו את ראשכם, כי ישועתכם קרובה!“

29אחר כך סיפר להם ישוע את המשל הבא: ”הביטו בעץ התאנה או בכל עץ אחר. 30כאשר העץ מלבלב יודעים אתם שקרב הקיץ בלי שיאמרו לכם זאת. 31כאשר כל מה שסיפרתי לכם יתחיל להתרחש, דעו לכם שמלכות האלוהים קרובה.

32”אני אומר לכם: כל הדברים האלה יתרחשו לפני שיחלוף הדור הזה. 33השמים והארץ יחלפו, אבל דברי לא יחלפו.

34”היזהרו לכם – אל תאבדו את הראש בשכרות, בבזבזנות, בתענוגות ובדאגות מחייה, פן יבוא עליכם היום ההוא במפתיע, כמלכודת. 35היום ההוא יבוא על כל יושבי תבל! 36משום כך שימרו תמיד על ערנותכם, והתפללו שאלוהים יעניק לכם כוח לצאת בשלום מכל העתיד להתרחש, ולהתייצב לפני בן־האדם.“ 37‏-38יום־יום הלך ישוע ללמד בבית־המקדש, והעם היה מתאסף בהמונים משעות הבוקר המוקדמות כדי להקשיב לדבריו. בלילות נהג ישוע ללכת לישון על הר הזיתים.