Luka 20 – NEN & CRO

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Luka 20:1-47

Swali Kuhusu Mamlaka Ya Yesu

(Mathayo 21:23-27; Marko 11:27-33)

120:1 Mt 26:55; Lk 8:120:1 Mt 21:23-27; Mk 11:27-33Siku moja, Yesu alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, pamoja na wazee wa watu wakamjia. 220:2 Yn 2:18; Mdo 4:7Wakamuuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?”

3Akawajibu, “Nami nitawauliza swali. 420:4 Mk 1:4Je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?”

5Wakahojiana wao kwa wao wakisema, “Kama tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 620:6 Lk 7:29; Mt 11:9Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ watu wote watatupiga mawe, kwa sababu wanaamini kwamba Yohana alikuwa nabii.”

7Basi wakajibu, “Hatujui ulikotoka.”

8Yesu akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”

Mfano Wa Wapangaji Waovu

(Mathayo 21:33-46; Marko 12:1-12)

920:9 Isa 5:17; Mt 25:14Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu. 1020:10 2Nya 36:15, 16Wakati wa mavuno ulipofika, akamtuma mtumishi wake kwa hao wapangaji ili wampe sehemu ya mavuno ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. 11Akamtuma mtumishi mwingine, huyo naye wakampiga, wakamfanyia mambo ya aibu na kumfukuza. 12Bado akamtuma na mwingine wa tatu, huyu pia wakamjeruhi na kumtupa nje ya shamba.

1320:13 Mt 3:17“Basi yule mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa, huenda yeye watamheshimu.’

14“Lakini wale wapangaji walipomwona, wakasemezana wao kwa wao. Wakasema, ‘Huyu ndiye mrithi. Basi na tumuue ili urithi uwe wetu.’ 15Kwa hiyo wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua.”

“Sasa basi yule mwenye shamba la mizabibu atawafanyia nini wapangaji hawa? 1620:16 Lk 19:27Atakuja na kuwaua hao wapangaji, na kuwapa wapangaji wengine hilo shamba la mizabibu.”

Watu waliposikia hayo wakasema, “Mungu apishie mbali jambo hili lisitokee!”

1720:17 Za 118:22; Mdo 4:11Lakini Yesu akawakazia macho, akasema, “Basi ni nini maana ya yale yaliyoandikwa:

“ ‘Jiwe walilolikataa waashi,

limekuwa jiwe kuu la pembeni’?

1820:18 Isa 8:14-15Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.”

1920:19 Lk 19:47; Mk 11:18Walimu wa sheria na viongozi wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja, kwa sababu walifahamu kwamba amesema mfano huo kwa ajili yao. Lakini waliwaogopa watu.

Kumlipa Kaisari Kodi

(Mathayo 22:15-22; Marko 12:13-17)

2020:20 Mt 12:10; 27:2Kwa hiyo wakawa wanamchunguza na kutuma wapelelezi waliojifanya kuwa wenye haki ili wapate kumtega kwa maneno asemayo, ili wamtie katika uwezo na mamlaka ya mtawala. 2120:21 Yn 3:2Hivyo wale wapelelezi wakamuuliza, “Mwalimu, tunajua unasema na kufundisha yaliyo kweli wala humpendelei mtu, bali wafundisha njia ya Mungu katika kweli. 22Je, ni halali sisi kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”

23Lakini Yesu akatambua hila yao, kwa hiyo akawaambia, 24“Nionyesheni dinari. Je, sura hii na maandishi haya yaliyoko juu yake ni vya nani?”

2520:25 Lk 23:2; Rum 13:7Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.”

Akawaambia, “Basi mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”

26Wakashindwa kumkamata kwa yale aliyokuwa amesema hadharani. Nao wakashangazwa mno na majibu yake, wakanyamaza kimya.

Ufufuo Na Ndoa

(Mathayo 22:23-33; Marko 12:18-27)

2720:27 Mdo 23:8; 1Kor 15:12; Mdo 4:1Baadhi ya Masadukayo, wale wasemao kwamba hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Yesu na kumuuliza, 2820:28 Kum 25:5; Mwa 38:8“Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto. 29Basi palikuwepo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa, akafa bila kuzaa mtoto. 30Kisha yule wa pili akamwoa huyo mjane, naye akafa bila mtoto, 31naye wa tatu pia akamwoa. Vivyo hivyo ndugu wote saba wakawa wamemwoa huyo mwanamke, na wote wakafa pasipo yeyote kupata mtoto. 32Mwishowe, yule mwanamke naye akafa. 33Sasa basi, siku ya ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani, maana aliolewa na ndugu wote saba?”

34Yesu akawajibu, “Katika maisha haya watu huoa na kuolewa. 3520:35 Mt 12:32Lakini wale ambao wamehesabiwa kwamba wanastahili kupata nafasi katika ulimwengu ule na katika ufufuo wa wafu, hawaoi wala hawaolewi. 3620:36 Yn 1:12; 1Yn 3:1-2Hawa hawawezi kufa tena, kwa maana wao ni kama malaika. Wao ni watoto wa Mungu, kwa sababu ni watoto wa ufufuo. 3720:37 Kut 3:6Hata Mose alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Bwana, ‘Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo.’ 3820:38 Rum 6:10-11Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa kuwa kwake wote ni hai.”

39Baadhi ya walimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umesema sawasawa kabisa!”

4020:40 Mt 22:46; Mk 12:34Baada ya hayo hakuna mtu aliyethubutu kumuuliza maswali tena.

Kristo Ni Mwana Wa Nani?

(Mathayo 22:41-46; Marko 12:35-37)

4120:41 Mt 22:42; Mk 12:3520:41 Mt 22:41-45; Mk 12:35-37Kisha Yesu akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Kristo20:41 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. ni Mwana wa Daudi? 4220:42 Za 110:1; Mdo 2:34Daudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi:

“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:

“Keti mkono wangu wa kuume,

4320:43 Za 110:1; Mt 22:44hadi nitakapowaweka adui zako

chini ya miguu yako.” ’

44Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”

Yesu Awashutumu Walimu Wa Sheria

(Mathayo 23:1-36; Marko 12:38-40)

4520:45 Lk 11:43Wakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Yesu akawaambia wanafunzi wake, 4620:46 Lk 11:43“Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu. 4720:47 Mt 23:14Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”

Knijga O Kristu

Luka 20:1-47

O Isusovoj vlasti

(Mt 21:23-27; Mk 11:27-33)

1Dok je poučavao i naviještao Radosnu vijest u Hramu, priđu mu svećenički poglavari, pismoznanci i starješine 2pa ga upitaju: “Tko ti je dao pravo da to činiš? Tko te je ovlastio za to?”

3On im odgovori: “Upitat ću i ja vas. Recite mi: 4je li Ivanovo krštenje bilo s neba ili od ljudi?”

5Oni počnu umovati i međusobno raspravljati: “Ako kažemo da je s neba, pitat će nas zašto mu onda nismo vjerovali. 6A ako kažemo da je od ljudi, narod će nas kamenovati jer su uvjereni da je Ivan prorok.” 7Zato odgovore Isusu da ne znaju odakle je.

8A Isus im reče: “Onda ni ja vama neću reći otkuda mi vlast!”

Prispodoba o zlim vinogradarima

(Mt 21:33-46; Mk 12:1-12)

9Isus zatim narodu ispriča prispodobu: “Neki čovjek posadi vinograd i iznajmi ga vinogradarima. Zatim otputovao na mnogo godina. 10Kad dođe vrijeme berbe, pošalje slugu da ubere njegov dio uroda. Ali vinogradari ga pretuku i pošalju natrag praznih ruku. 11Pošalje im zatim drugog slugu, ali oni i njega pretuku, izgrde i pošalju natrag praznih ruku. 12Pošalje im i trećega, ali oni ga rane i otjeraju ga.

13‘Što da učinim?’ pitao se vlasnik vinograda. ‘Poslat ću im svojega ljubljenog sina. Prema njemu će se valjda odnositi s poštovanjem.’

14Ali kad vinogradari ugledaju sina, počnu umovati: ‘Ovaj će naslijediti imanje. Ubijmo ga pa ćemo se domognuti imanja umjesto njega!’ 15Izbace ga iz vinograda i ubiju.

Što mislite da će učiniti vlasnik kad čuje što se dogodilo? 16Doći će i pobiti te vinogradare, a vinograd dati u najam drugima.”

“Ne daj Bože da se takvo što dogodi!” rekoše Isusovi slušatelji.

17Ali Isus ih dobro promotri i reče: “A što onda znači onaj ulomak iz Svetoga pisma:

‘Kamen koji su graditelji odbacili

postane ugaonim kamenom’?

18Padne li tko na taj kamen, smrskat će se, i padne li kamen na koga, satrt će ga.”

19Pismoznanci i svećenički poglavari htjeli su ga uhvatiti jer su dobro znali da se ta prispodoba odnosi na njih, ali bojali su se naroda.

O porezu

(Mt 22:15-22; Mk 12:13-17)

20Vrebajući ga, pošalju mu uhode koji su se izdavali za pravednike da ga uhvate u riječi pa da ga mogu predati upraviteljevoj vlasti. 21“Učitelju,” kazaše Isusu, “znamo da govoriš istinu i da si nepristran jer ne gledaš tko je tko, nego prema istini poučavaš putu Božjemu. 22Reci nam je li dopušteno plaćati porez caru ili nije.”

23Isus prozre njihovo lukavstvo pa reče: 24“Pokažite mi kovani novac.20:24 U grčkome: denar. Čiji su ovo lik i natpis na kovanici?”

“Carevi”, odgovore.

25“Onda dajte caru carevo, ali Bogu valja dati Božje”, reče im. 26Tako ga nisu uspjeli uhvatiti u riječi pred narodom, već su ušutjeli zadivljeni odgovorom.

O uskrsnuću

(Mt 22:23-33; Mk 12:18-27)

27Tada dođu k njemu neki od saduceja, koji tvrde da nema uskrsnuća, i upitaju ga: 28“Gospodine, Mojsije nam je dao zakon prema kojemu, umre li oženjen muškarac bez djece, njegov se brat mora oženiti njegovom udovicom kako bi ona rodila sina koji će naslijediti posjed umrloga i nositi njegovo ime.20:28 Ponovljeni zakon 25:5-6. 29Bilo je sedmero braće. Prvi se brat oženi i umre a da nije imao djece. 30Drugi se brat oženi njegovom udovicom, ali također umre, 31treći i sva ostala braća također. Tako nijedan od sedmorice ne ostavi potomstva. 32Na posljetku umre i žena. 33Čija će onda ona biti žena o uskrsnuću kad je bila udana za svu sedmoricu?”

34“Ljudi ovoga svijeta žene se i udaju,” odgovori im Isus, 35“ali oni koji budu dostojni biti dionicima onoga svijeta i uskrsnuća od mrtvih, neće se ni ženiti ni udavati. 36Neće više moći ni umrijeti: bit će poput anđela. Oni su Božja djeca, djeca uskrsnuća. 37A da će mrtvi uskrsnuti, čak je i Mojsije potvrdio u ulomku o gorućem grmu gdje Gospodina naziva ‘Bogom Abrahamovim, Izakovim i Jakovljevim’ dugo nakon što su oni poumirali.20:37 Izlazak 3:6. 38A Bog nije Bog mrtvih, već Bog živih! Svi su oni za Boga živi.”

39“Dobro si rekao, Učitelju!” rekoše neki pismoznanci. 40I više se nisu usuđivali išta ga upitati.

Čiji sin je Mesija

(Mt 22:41-46; Mk 12:35-37)

41Tada Isus upita njih: “Kako mogu tvrditi da je Mesija Davidov sin? 42Pa sâm je David u Knjizi psalama napisao:

‘Gospodin je rekao mojem Gospodinu:

Sjedni mi s desne strane

43dok ti ne bacim pod noge tvoje neprijatelje.’20:42-43 Psalam 110:1.

44Sâm ga je David nazvao svojim Gospodinom. Kako bi mu onda mogao biti sin?”

45Zatim pred svim narodom reče učenicima: 46“Čuvajte se pismoznanaca! Vole se šetati u dugim haljinama i da ih ljudi pozdravljaju na trgovima. U sinagogama vole sjediti na počasnim mjestima, a na gozbama na pročelju stola. 47Besramno troše udovička dobra, a prikrivaju se dugačkim molitvama u javnosti. Oni će biti strože kažnjeni.”