Luka 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Luka 2:1-52

Kuzaliwa Kwa Yesu

(Mathayo 1:18-25)

12:1 Lk 3:1; Mt 22:17; 24:14Siku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Kirumi. 22:2 Mdo 21:3; Mt 4:24; Mdo 15:23, 41(Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio alikuwa mtawala wa Shamu2:2 Shamu inamaanisha Syria.). 3Kila mtu alikwenda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa.

42:4 Yn 7:42Hivyo Yosefu akapanda kutoka mji wa Nazareti ulioko Galilaya kwenda Uyahudi, mpaka Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi. 52:5 Lk 1:27; Mt 1:16Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Maria, ambaye alikuwa amemposa naye alikuwa mjamzito. 6Wakiwa Bethlehemu, wakati wa Maria wa kujifungua ukawa umetimia, 72:7 Mt 1:25naye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori ya kulia ngʼombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.

Wachungaji Na Malaika

8Katika eneo lile walikuwako wachungaji waliokuwa wakikaa mashambani, wakilinda makundi yao ya kondoo usiku. 92:9 Lk 1:11; Mdo 5:19Ghafula tazama, malaika wa Bwana akawatokea, nao utukufu wa Bwana ukawangʼaria kotekote, wakaingiwa na hofu. 102:10 Mt 14:27Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote. 112:11 Yn 3:17; Rum 11:14; Mdo 3:20; 9:22Leo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Kristo2:11 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Bwana. 122:12 1Sam 10:7; Za 86:17Hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu: Mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa nguo za kitoto na kulazwa katika hori ya kulia ngʼombe.”

132:13 Dan 7:10; Mwa 28:12; 32:12; Za 103:20, 21; 148:2; Ebr 1:14; Ufu 5:11Ghafula pakawa na jeshi kubwa la mbinguni pamoja na huyo malaika wakimsifu Mungu wakisema,

142:14 Isa 9:6; Rum 5:1“Atukuzwe Mungu juu mbinguni,

na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”

15Hao malaika walipokwisha kuondoka na kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakasemezana wao kwa wao, “Twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotukia, ambayo Bwana ametuambia habari zake.”

162:16 Lk 2:7Hivyo wakaenda haraka Bethlehemu, wakawakuta Maria na Yosefu na yule mtoto mchanga akiwa amelala katika hori la kulia ngʼombe. 172:17 Lk 2:10-12Walipomwona yule mtoto, wakawaeleza yale waliyokuwa wameambiwa kuhusu huyo mtoto. 18Nao wote waliosikia habari hizi wakastaajabia yale waliyoambiwa na wale wachungaji wa kondoo. 192:19 Lk 2:51Lakini Maria akayaweka mambo haya yote moyoni mwake na kuyatafakari. 202:20 Mt 9:8Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa ajili ya mambo yote waliyokuwa wameambiwa na kuyaona.

212:21 Lk 1:31, 59Hata zilipotimia siku nane, ulikuwa ndio wakati wa kumtahiri mtoto, akaitwa Yesu, jina alilokuwa amepewa na malaika kabla hajatungwa mimba.

Yesu Apelekwa Hekaluni

222:22 Law 12:2-8Ulipotimia wakati wa utakaso wake Maria kwa mujibu wa Sheria ya Mose, basi Yosefu na Maria walimpeleka mtoto Yerusalemu, ili kumweka wakfu kwa Bwana 232:23 Kut 2:12-15; Hes 3:13(kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Bwana, kwamba, “Kila mtoto wa kiume kifungua mimba atawekwa wakfu kwa Bwana”), 242:24 Law 12:8na pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa katika Sheria ya Bwana: “Hua wawili au makinda mawili ya njiwa.”

252:25 Lk 16:6; 23:51; Isa 52:9Basi alikuwako huko Yerusalemu mtu mmoja jina lake Simeoni, ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu, akitarajia faraja ya Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 262:26 Za 89:48; Ebr 11:5Roho Mtakatifu alikuwa amemfunulia kuwa hatakufa kabla hajamwona Kristo wa Bwana. 272:27 Mwa 46:30; Flp 1:23; Lk 2:22Simeoni, akiwa ameongozwa na Roho Mtakatifu, alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Yesu ili kumfanyia kama ilivyokuwa desturi ya Sheria, 28ndipo Simeoni akampokea mtoto mikononi mwake na kumsifu Mungu, akisema:

292:29 Mdo 2:24“Bwana Mwenyezi, kama ulivyoahidi,

sasa wamruhusu mtumishi wako

aende zake kwa amani.

302:30 Isa 40:5; Lk 3:6; Isa 52:10Kwa maana macho yangu yameuona wokovu wako,

31ulioweka tayari machoni pa watu wote,

322:32 Isa 49:6; Mdo 26:23nuru kwa ajili ya ufunuo kwa watu wa Mataifa

na kwa ajili ya utukufu kwa watu wako Israeli.”

33Naye Yosefu na mama yake mtoto wakastaajabu kwa yale yaliyokuwa yamesemwa kumhusu huyo mtoto. 342:34 Mt 12:46; Isa 8:14; Gal 5:11Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake, 352:35 Za 42:10; Yn 19:25ili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike. Nao upanga utauchoma moyo wako.”

362:36 Mdo 21:9Tena alikuwako Hekaluni nabii mmoja mwanamke, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa mzee sana; naye alikuwa ameolewa na kuishi na mume kwa miaka saba tu, kisha mumewe akafa. 372:37 1Tim 5:9; Mdo 14:23Hivyo alikuwa mjane na umri wake ulikuwa miaka themanini na minne. Yeye hakuondoka humo Hekaluni usiku wala mchana, bali alikuwa akimwabudu Mungu, akifunga na kuomba. 382:38 Isa 52:9; Lk 24:21Wakati huo huo, Ana alikuja akaanza kusifu, akimshukuru Mungu na kusema habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wakitarajia ukombozi wa Yerusalemu.

392:39 Mt 2:23Yosefu na Maria walipokuwa wamekamilisha mambo yote yaliyotakiwa na Sheria ya Bwana, walirudi mjini kwao Nazareti huko Galilaya. 402:40 Lk 2:52; 1:80Naye yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu, akiwa amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

Kijana Yesu Hekaluni

412:41 Kut 23:15; Lk 22:8Kila mwaka Yosefu na Maria mama yake Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka. 42Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walipanda kwenda kwenye Sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 432:43 Kut 12:18Baada ya Sikukuu kumalizika, wakati Yosefu na Maria mama yake walipokuwa wakirudi nyumbani, Yesu alibaki Yerusalemu lakini hawakutambua. 44Wao wakidhani kuwa yuko miongoni mwa wasafiri, walienda mwendo wa kutwa nzima. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa zao na marafiki. 45Walipomkosa walirudi Yerusalemu ili kumtafuta. 46Baada ya siku tatu wakamkuta ndani ya Hekalu, akiwa ameketi katikati ya walimu wa sheria, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 472:47 Mt 7:28Wote waliomsikia walistaajabishwa na uwezo wake mkubwa wa kuelewa, na majibu aliyoyatoa. 482:48 Mt 12:46; Lk 3:23; 4:22Yosefu na Maria mama yake walipomwona walishangaa. Mama yake akamuuliza, “Mwanangu, mbona umetufanyia hivi? Tazama, mimi na baba yako tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa kila mahali.”

492:49 Yn 2:16Yesu akawaambia, “Kwa nini kunitafuta? Hamkujua kwamba imenipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?”

502:50 Mk 9:32Lakini wao hawakuelewa maana ya lile alilowaambia.

512:51 Lk 2:19Ndipo akashuka pamoja nao hadi Nazareti, naye alikuwa mtiifu kwao. Lakini mama yake akayaweka moyoni mwake mambo haya yote. 522:52 Mit 3; 4; Lk 1:80Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.