Luka 19 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Luka 19:1-48

Zakayo Mtoza Ushuru

119:1 Lk 18:35Yesu akaingia Yeriko, naye alikuwa anapita katikati ya huo mji. 2Tazama, palikuwa na mtu mmoja mkuu wa watoza ushuru naye alikuwa tajiri, jina lake Zakayo. 3Yeye alikuwa akijitahidi kumwona Yesu ni mtu wa namna gani. Lakini kutokana na umati mkubwa wa watu hakuweza kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo. 419:4 1Fal 10:27; 1Nya 27:28; Lk 18:37Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati wa watu akapanda juu ya mkuyu ili amwone Yesu, kwa sababu angeipitia njia ile.

5Yesu alipofika pale chini ya huo mkuyu, akatazama juu, akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani kwako!” 6Hivyo Zakayo akashuka upesi, akamkaribisha Yesu nyumbani kwake kwa furaha kubwa.

719:7 Mt 9:11Watu wote walipoona hivyo, wakaanza kunungʼunika wakisema, “Amekwenda kuwa mgeni wa ‘mtu mwenye dhambi.’ ”

819:8 Lk 7:13; 3:12-13; Hes 5:7; Eze 33:14-15Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana, “Tazama, Bwana! Sasa hivi nusu ya mali yangu ninawapa maskini, nami kama nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, nitamrudishia mara nne ya hicho kiwango.”

919:9 Rum 4:16; Gal 3:17Ndipo Yesu akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Abrahamu. 1019:10 Eze 34:12-16; Yn 3:17Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”

Mfano Wa Fedha

(Mathayo 25:14-30)

1119:11 Lk 17:20; Mt 3:2; Mdo 1:6Walipokuwa wanasikiliza haya, Yesu akaendelea kuwaambia mfano, kwa sababu alikuwa anakaribia Yerusalemu na watu walikuwa wakidhani ya kuwa Ufalme wa Mungu ulikuwa unakuja saa iyo hiyo. 1219:12 Mk 13:34; Mt 25:14Hivyo akawaambia: “Mtu mmoja mwenye cheo kikubwa alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi. 1319:13 Mk 13:34Hivyo akawaita kumi miongoni mwa watumishi wake, na akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Fanyeni biashara na fedha hizi mpaka nitakaporudi.’

1419:14 Yn 1:11“Lakini raiya wa nchi yake walimchukia wakapeleka ujumbe na kusema, ‘Hatutaki huyu mtu awe mfalme wetu.’

15“Hata hivyo alirudi akiwa amekwisha kupokea mamlaka ya ufalme, akawaita wale watumishi wake aliokuwa amewaachia fedha, ili afahamu ni faida kiasi gani kila mmoja wao aliyopata kwa kufanya biashara.

16“Wa kwanza akaja na kusema, ‘Bwana, kutokana na fedha uliyoniachia, nimepata faida mara kumi zaidi.’

17“Yule bwana akamjibu, ‘Umefanya vizuri mtumishi mwema! Kwa sababu umekuwa mwaminifu katika wajibu mdogo sana, nakupa mamlaka juu ya miji kumi.’

18“Wa pili naye akaja. Akasema, ‘Bwana, fedha yako imeleta faida mara tano zaidi.’

19“Bwana wake akajibu, ‘Nakupa mamlaka juu ya miji mitano.’

20“Kisha akaja yule mtumishi mwingine, akasema, ‘Bwana, hii hapa fedha yako. Niliitunza vizuri kwenye kitambaa. 2119:21 Mit 27:18; Lk 16:10Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mgumu. Unachukua ambapo hukuweka kitu, na unavuna mahali ambapo hukupanda kitu.’

2219:22 2Sam 1:16; Ay 15:6; Mt 25:26“Bwana wake akamjibu, ‘Nitakuhukumu kwa maneno yako mwenyewe, wewe mtumishi mwovu! Kama ulifahamu kwamba mimi ni mtu mgumu, nichukuaye mahali ambapo sikuweka kitu na kuvuna mahali ambapo sikupanda, 23kwa nini basi hukuweka fedha zangu kwa watoa riba, ili nitakaporudi nichukue iliyo yangu na riba yake?’

24“Ndipo akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu, ‘Mnyangʼanyeni fungu lake la fedha, mkampe yule mwenye kumi.’

25“Wakamwambia, ‘Bwana, mbona; tayari anayo mafungu kumi!’

2619:26 Mt 13:12; 25:29“Akawajibu, ‘Nawaambia kwamba kila aliye na kitu, ataongezewa. Lakini yule asiye na kitu, hata alicho nacho atanyangʼanywa. 27Lakini wale adui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme juu yao. Waleteni hapa mkawaue mbele yangu.’ ”

Yesu Aingia Yerusalemu Kwa Ushindi

(Mathayo 21:1-11; Marko 11:1-11; Yohana 12:12-19)

2819:28 Mk 10:32; Lk 9:51Baada ya Yesu kusema haya, alitangulia kupanda kwenda Yerusalemu. 2919:29 Mt 21:1, 1719:29 Mt 21:1-9; Mk 11:1-10; Yn 12:12-16Naye alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima uitwao Mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili, akawaambia, 30“Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa. 31Kama mtu akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.’ ”

3219:32 Lk 22:13Wale waliotumwa wakaenda, wakakuta kila kitu kama vile Yesu alivyokuwa amewaambia. 3319:33 2Fal 9:13Walipokuwa wanamfungua yule mwana-punda, wenyewe wakawauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwana-punda?”

34Wale wanafunzi wakajibu, “Bwana anamhitaji.”

3519:35 2Fal 9:13; Mt 21:7; Mk 11:7; Yn 12:14Wakamleta kwa Yesu, nao baada ya kutandika mavazi yao juu ya huyo mwana-punda, wakampandisha Yesu juu yake. 3619:36 Mt 21:18Alipokuwa akienda akiwa amempanda, watu wakatandaza mavazi yao barabarani.

3719:37 Mt 21:1Alipokaribia mahali yanapoanzia materemko ya Mlima wa Mizeituni, umati wote wa wafuasi wake wakaanza kumsifu Mungu kwa furaha kwa sauti kuu kwa ajili ya matendo yote ya miujiza waliyoyaona. Wakasema:

3819:38 Za 118:26; Lk 13:35; 2:14“Amebarikiwa Mfalme ajaye kwa Jina la Bwana!”

“Amani mbinguni na utukufu huko juu sana.”

3919:39 Mt 21:15-16Baadhi ya Mafarisayo waliokuwamo miongoni mwa ule umati wa watu wakamwambia, “Mwalimu, waamuru wanafunzi wako wanyamaze.”

4019:40 Ebr 2:11Yesu akawajibu, “Nawaambia ninyi, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele.”

Yesu Anaulilia Mji Wa Yerusalemu

4119:41 Isa 22:4; Lk 13:34-35Alipokaribia Yerusalemu na kuuona mji, aliulilia, 4219:42 Kum 32:29; Mt 13:14; Yn 12:38akisema, “Laiti ungalijua hata wewe leo yale ambayo yangeleta amani, lakini sasa yamefichika machoni pako. 4319:43 Yer 6:6; Lk 21:20Hakika siku zinakujia, ambazo adui zako watakuzingira, nao watakuzunguka pande zote na kukuzuilia ndani. 4419:44 Za 137:9; Mt 24:2; Mk 13:2; 1Pet 2:12Watakuponda chini, wewe na watoto walioko ndani ya kuta zako. Nao hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu hukutambua wakati wa kujiliwa kwako.”

Yesu Atakasa Hekaluni

(Mathayo 21:12-17; Marko 11:15-19; Yohana 2:13-22)

4519:45 Mt 21:12; Mk 11:11, 15; Yn 2:14, 15Ndipo akaingia eneo la Hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza vitu humo. 4619:46 Isa 56:7; Yer 7:11Naye akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyangʼanyi.’ ”

4719:47 Mt 26:55; 12:14; Mk 11:18Kila siku alikuwa akifundisha Hekaluni. Lakini viongozi wa makuhani, walimu wa sheria na viongozi wa watu walikuwa wakitafuta njia ili kumuua. 48Lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote walimfuata wakiyasikiliza maneno yake kwa usikivu mwingi.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

路加福音 19:1-48

撒该悔改

1耶稣进了耶利哥,正从城里经过。 2有个人名叫撒该,是税吏长,家财丰厚。 3他想看看耶稣是谁,可是因为周围人多,他身材矮小,无法看见。 4他便跑到前面,爬上一棵桑树观看,因为耶稣会从那里经过。

5耶稣走到那里,抬头招呼他说:“撒该,快下来!今天我必须住在你家。”

6撒该连忙爬下来,兴高采烈地迎接耶稣。 7百姓见状都埋怨说:“祂怎么到一个罪人家里作客?”

8撒该站起来对主说:“主啊,我要把一半的财产分给穷人。我欺骗过谁,就还谁四倍。”

9耶稣说:“今天救恩临到这家了,因为他也是亚伯拉罕的子孙。 10人子来是要寻找和拯救迷失的人。”

十个奴仆的比喻

11众人在听的时候,耶稣又为他们讲了一个比喻,因为祂快到耶路撒冷了,人们以为上帝的国马上就要显现了。

12耶稣说:“有一位贵族要到远方去受封为王,然后返回。 13临行前,他召集了十个奴仆,发给每人一千个银币,吩咐他们,‘你们在我出门期间要用这些钱做生意。’

14“可是他的人民却憎恨他,他们随后派一个代表团去请愿说,‘我们不要这人做我们的王。’

15“那贵族受封为王回来后,召齐十个奴仆,想知道他们做生意赚了多少。 16第一个奴仆上前禀告说,‘主啊,我用你给我的一千个银币赚了一万个银币。’

17“主人说,‘好,你真是个好奴仆!你既然在小事上忠心,就派你管理十座城。’

18“第二个奴仆上前说,‘主啊,我用你给我的一千个银币赚了五千个银币。’

19“主人说,‘我派你管理五座城。’

20“另一个奴仆上前说,‘主啊,这是你先前给我的一千个银币,我一直把它包在手帕里。 21因为你很严厉,没有存还要取,没有种还要收,所以我怕你。’

22“主人对那奴仆说,‘你这个恶奴仆!我要按你自己的话定你的罪。你既然知道我很严厉,没有存还要取,没有种还要收, 23为什么不把我的银币存进钱庄,等我回来可以连本带利收回来?’

24“接着,他吩咐站在旁边的奴仆,‘收回他的一千银币,给那个有一万银币的。’

25“他们说,‘主啊,那个人已经有一万银币了。’

26“主人答道,‘我告诉你们,凡有的,还要给他更多;凡没有的,连他仅有的也要夺去。 27至于那些反对我做王的仇敌,把他们带来,在我面前处决。’”

骑驴进耶路撒冷

28耶稣说完这个比喻,就走在众人前面上耶路撒冷去。

29快到橄榄山的伯法其伯大尼时,耶稣派了两个门徒,并嘱咐说: 30“你们去前面的村庄,一进村就会看见一头从来没有人骑过的驴驹拴在那里,你们把它解开牵来。 31若有人问你们为什么把它解开,就说,‘主要用它。’”

32两个门徒出去后,所遇见的情形正如耶稣所说的。 33当他们解开驴驹时,主人问他们:“你们解开驴驹干什么?”

34他们说:“主要用它。”

35他们把驴驹牵到耶稣那里,把自己的外衣搭在驴背上,扶耶稣上驴。

36耶稣骑着驴前行,众人把衣服铺在路上。 37祂正走下橄榄山,将近耶路撒冷的时候,众门徒因为以往所见的神迹奇事,就欢腾起来,高声赞美上帝:

38“奉主名来的王当受称颂!”19:38 诗篇118:26

“天上有平安,至高之处有荣耀!”

39百姓中有几个法利赛人对耶稣说:“老师,责备你的门徒吧。”

40耶稣说:“我告诉你们,如果他们闭口不言,这些石头都要呼喊了!”

为耶路撒冷哀哭

41耶稣快到耶路撒冷时,看见那城,就为它哀哭, 42说:“今天你若知道那能带给你平安的事就好了!可惜这事现在是隐藏的,你看不见! 43因为有一天敌人要在你周围筑垒把你团团围住,四面攻击你。 44他们要把你夷为平地,毁灭你城墙里的儿女,不会留下两块叠在一起的石头,因为你没有认出上帝眷顾你的时刻。”

耶稣洁净圣殿

45耶稣进入圣殿赶走里面做买卖的人, 46并对他们说:“圣经上说,‘我的殿要成为祷告的殿’19:46 以赛亚书56:7,你们竟把它变成了贼窝19:46 耶利米书7:11。”

47祂天天在圣殿教导人,祭司长、律法教师和百姓的官长都想杀祂, 48只是无从下手,因为百姓都十分喜爱听祂讲道。