Luka 12 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Luka 12:1-59

Maonyo Dhidi Ya Unafiki

(Mathayo 10:26-33)

112:1 Mt 16:6-12; Mk 8:15Wakati huo, umati mkubwa wa watu maelfu, walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu akaanza kuzungumza kwanza na wanafunzi wake, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao. 212:2 Mk 4:12; Lk 8:1712:2 Mt 10:26-33Hakuna jambo lolote lililositirika ambalo halitafunuliwa, au lililofichwa ambalo halitajulikana. 3Kwa hiyo, lolote mlilosema gizani litasikiwa nuruni. Na kile mlichonongʼona masikioni mkiwa kwenye vyumba vya ndani, kitatangazwa juu ya paa.

412:4 Yn 15:14-15“Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya lolote zaidi. 512:5 Ebr 10:31Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo! 6Mnajua kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti mbili? Lakini Mungu hamsahau hata mmoja wao. 712:7 Mt 10:30; 12:12Naam, hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. Hivyo msiogope, kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.

812:8 Lk 15:10“Ninawaambia kwamba yeyote atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri mbele za malaika wa Mungu. 912:9 Mk 8:38; 2Tim 2:12Lakini yeye atakayenikana mimi mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkana mbele ya malaika wa Mungu. 1012:10 Mt 8:20; 12:31-32; Mk 3:28-29Naye kila atakayenena neno baya dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.

1112:11 Mt 10:17-19; Mk 13:11“Watakapowapeleka katika masinagogi, na mbele ya watawala na wenye mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema. 1212:12 Kut 4:12; Mt 10:20Kwa maana Roho Mtakatifu atawafundisha wakati huo huo mnachopaswa kusema.”

Mfano Wa Tajiri Mpumbavu

13Mtu mmoja katika umati wa watu akamwambia Yesu, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane naye urithi wetu.”

1412:14 Mdo 7:27Lakini Yesu akamwambia, “Rafiki, ni nani aliyeniweka mimi kuwa hakimu wenu au msuluhishi juu yenu?” 1512:15 Ay 31:24; Za 62:10Ndipo Yesu akawaambia, “Jihadharini! Jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana maisha ya mtu hayatokani na wingi wa mali alizo nazo.”

16Kisha akawaambia mfano huu: “Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana. 17Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Sina mahali pa kuhifadhi mavuno yangu.’

18“Ndipo huyo tajiri akasema, ‘Nitafanya hivi: Nitabomoa ghala zangu za nafaka na kujenga nyingine kubwa zaidi na huko nitayahifadhi mavuno yangu yote na vitu vyangu. 1912:19 Mhu 11:9; 1Kor 15:32; Yak 5:5Nami nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, unavyo vitu vingi vizuri ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi. Pumzika; kula, unywe, ufurahi.” ’

2012:20 Yer 17:11; Lk 11:40; Ay 27:8; Za 39:6; 49:19“Lakini Mungu akamwambia, ‘Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa. Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani?’

2112:21 Mt 6:20; Lk 12:33; 1Tim 6:18, 19; Yak 2:5“Hivyo ndivyo ilivyo kwa wale wanaojiwekea mali lakini hawajitajirishi kwa Mungu.”

Msiwe Na Wasiwasi

(Mathayo 6:25-34)

2212:22 Mt 6:2512:22 Mt 6:25-33Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake: “Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. 23Maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi. 2412:24 Ay 38:41; Za 147:9Fikirini ndege! Wao hawapandi wala hawavuni, hawana ghala wala popote pa kuhifadhi nafaka; lakini Mungu huwalisha. Ninyi ni wa thamani zaidi kuliko ndege! 25Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake? 26Kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo, kwa nini basi kuyasumbukia hayo mengine?

2712:27 1Fal 10:4-7“Angalieni maua jinsi yameavyo: Hayafanyi kazi wala hayafumi. Lakini nawaambia, hata Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo maua. 2812:28 Mt 6:30Basi ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yapo, na kesho yanatupwa motoni, si atawavika ninyi vizuri zaidi, enyi wa imani haba! 29Wala msisumbuke mioyoni mwenu mtakula nini au mtakunywa nini. Msiwe na wasiwasi juu ya haya. 3012:30 Lk 6:36; Mt 6:8Watu wa mataifa ya duniani husumbuka sana kuhusu vitu hivi vyote, lakini Baba yenu anafahamu kuwa mnahitaji haya yote. 3112:31 Mt 3:2; 19:29Bali utafuteni Ufalme wa Mungu, na haya yote atawapa pia.

Utajiri Wa Mbinguni

(Mathayo 6:19-21)

3212:32 Mt 14:27; 25:34“Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa ninyi Ufalme. 3312:33 Mt 19:21; Mdo 2:45; Mt 6:20; Yak 5:2Uzeni mali zenu mkawape maskini. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha, mahali ambapo mwizi hakaribii wala nondo haharibu. 3412:34 Mt 6:21Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo moyo wako utakapokuwa pia.

Kukesha

3512:35 Efe 6:14; 1Pet 1:13; Mt 25:1“Kuweni tayari mkiwa mmevikwa kwa ajili ya huduma na taa zenu zikiwa zinawaka, 3612:36 Mt 25:1-13kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka kwenye karamu ya arusi, ili ajapo na kubisha mlango waweze kumfungulia mara. 3712:37 Mt 24:42-46; 25:13; 20:28Heri wale watumishi ambao bwana wao atakapokuja atawakuta wakiwa wanakesha. Amin, nawaambia, atajifunga mkanda wake na kuwaketisha ili wale, naye atakuja na kuwahudumia. 38Itakuwa heri kwa watumwa hao ikiwa bwana wao atakapokuja atawakuta wamekesha hata kama atakuja mnamo usiku wa manane, au karibu na mapambazuko. 3912:39 1The 5:2; 2Pet 3:10Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angalijua saa mwizi atakuja, asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. 4012:40 Mk 13:33; Lk 21:36Ninyi nanyi hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.”

Mtumishi Mwaminifu Na Yule Asiye Mwaminifu

(Mathayo 24:45-51)

41Ndipo Petro akamuuliza, “Bwana, mfano huu unatuambia sisi peke yetu au watu wote?”

4212:42 Lk 7:13Yesu akamjibu, “Ni yupi basi wakili mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamfanya msimamizi juu ya watumishi wake wote, ili awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa? 43Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 4412:44 Mt 24:47Amin nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. 4512:45 Mt 24:48Lakini kama yule mtumishi atasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia kurudi,’ kisha akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa. 4612:46 Lk 12:40Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wale wasioamini.

4712:47 Kum 25:2“Yule mtumishi anayefahamu vyema mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, atapigwa kwa mapigo mengi. 4812:48 Law 5:17; Hes 15:27-30Lakini yeyote ambaye hakujua naye akafanya yale yastahiliyo kupigwa, atapigwa kidogo. Yeyote aliyepewa vitu vingi, atadaiwa vingi; na yeyote aliyekabidhiwa vingi, kwake vitatakiwa vingi.

Yesu Kuleta Mafarakano

(Mathayo 10:34-36)

4912:49 Lk 12:51“Nimekuja kuleta moto duniani; laiti kama ungekuwa tayari umewashwa! 5012:50 Mk 10:38; Yn 19:30Lakini ninao ubatizo ambao lazima nibatizwe, nayo dhiki yangu ni kuu mpaka ubatizo huo ukamilike! 5112:51 Mt 10:34; Lk 12:49; Mik 7:6; Yn 7:46; 9:16Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? La, nawaambia sivyo, nimekuja kuleta mafarakano. 5212:52 Mt 10:35Kuanzia sasa, kutakuwa na watu watano katika nyumba moja, watatu dhidi ya wawili, na wawili dhidi ya watatu. 5312:53 Mik 7:6; Mt 10:21Watafarakana baba dhidi ya mwanawe na mwana dhidi ya babaye, mama dhidi ya bintiye na binti dhidi ya mamaye, naye mama mkwe dhidi ya mkwewe na mkwe dhidi ya mama mkwe wake.”

Kutambua Majira

(Mathayo 16:2-3)

5412:54 Mt 16:2-3Pia Yesu akauambia ule umati wa watu, “Mwonapo wingu likitokea magharibi, mara mwasema, ‘Mvua itanyesha,’ nayo hunyesha. 55Nanyi mwonapo upepo wa kusini ukivuma, ninyi husema, ‘Kutakuwa na joto,’ na huwa hivyo. 5612:56 Mt 16:3Enyi wanafiki! Mnajua jinsi ya kutambua kuonekana kwa dunia na anga. Inakuwaje basi kwamba mnashindwa kutambua wakati huu wa sasa?

57“Kwa nini hamwamui wenyewe lililo haki? 5812:58 Mt 5:25Uwapo njiani na mshtaki wako kwenda kwa hakimu, jitahidi kupatana naye mkiwa njiani. La sivyo, atakupeleka kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa afisa, naye afisa atakutupa gerezani. 5912:59 Mt 5:26; Mk 12:42Nakuambia, hautatoka humo hadi uwe umelipa senti ya mwisho.”

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

路加福音 12:1-59

警戒门徒

1这时,成千上万的人聚集在一起,甚至互相践踏。耶稣先对门徒说:“你们要提防法利赛人的酵,就是他们的伪善。 2掩盖的事终会暴露出来,隐藏的秘密终会被人知道。 3你们暗中说的话将被公布于众,你们在密室里的私语将在屋顶上被传扬。

4“朋友们,我告诉你们,不要惧怕那些杀害人的身体后再也无计可施的人。 5我告诉你们应该惧怕谁,要惧怕上帝——祂有权终结人的生命,并把人扔进地狱里。是的,我告诉你们,要惧怕祂!

6“五只麻雀不是只卖两个铜钱吗?但没有一只麻雀会被上帝遗忘。 7其实就连你们的头发都被数过了。不要害怕,你们比许多麻雀要贵重!

8“我告诉你们,凡在人面前承认我的,人子在上帝的天使面前也必承认他。 9凡在人面前否认我的,人子在上帝的天使面前也必否认他。 10凡说话得罪人子的,还可以得到赦免,但亵渎圣灵的,必得不到赦免! 11当你们被押到会堂,或到官员和当权者面前时,不要顾虑如何申辩,或说什么话, 12因为到时候圣灵必指教你们该说什么。”

无知富翁的比喻

13这时,人群中有人对耶稣说:“老师,请你劝劝我的兄长跟我分家产吧。”

14耶稣答道:“朋友,谁派我做你们的审判官或仲裁,为你们分家产呢?” 15接着,祂对众人说:“你们要小心防范一切的贪心,因为人的生命并不在于家道富足。”

16耶稣又讲了一个比喻,说:“有一个财主,他的田里大丰收, 17便心里盘算,‘我储藏农产的地方不够了,怎么办呢?’ 18于是他说,‘我有办法了。我要把我的仓库拆掉,建几座更大的,好储藏我所有的粮食和财物! 19那时,我就可以对自己说:你存了这么多财产,能享用多年,现在大可高枕无忧、尽情地吃喝玩乐吧!’ 20但上帝对他说,‘无知的人啊,今晚就要取走你的命!你所预备的一切留给谁享用呢?’

21“这就是那些只顾为自己积财、在上帝面前却不富足之人的写照。”

不要为衣食忧虑

22耶稣继续对门徒说:“所以,我告诉你们,不要为生活忧虑,比如吃什么,也不要为身体忧虑,比如穿什么。 23因为生命比饮食重要,身体比穿着重要。 24你们看,乌鸦不种也不收,没仓也没库,上帝尚且养活它们,你们比飞鸟不知要贵重多少!

25“你们谁能用忧虑使自己多活片刻呢? 26既然你们连这样的小事都无能为力,又何必为其余的事忧虑呢? 27看看百合花如何生长吧,它们既不劳苦,也不纺织,但我告诉你们,就连所罗门王最显赫时的穿戴还不如一朵百合花!

28“野地的草今天还在,明天就被扔进炉中,上帝还这样装扮它们,何况你们呢?你们的信心太小了! 29你们不要追求吃什么喝什么,不要为此忧虑, 30因为这些都是不信的世人追求的,你们的天父知道你们需要这些。 31你们要寻求祂的国,这些会加给你们。

32“你们这一小群人啊,不要怕!因为你们的天父乐意把祂的国赐给你们。 33要变卖你们的家产去周济穷人,要为自己预备永不破损的钱袋,在天上积攒取之不尽的财宝,那里没有贼偷,也没有虫蛀。 34因为你们的财宝在哪里,你们的心也在哪里。

警醒预备

35“你们要束上腰带,准备服侍,要点亮灯, 36像奴仆们等候主人从婚宴回来。主人回来一叩门,奴仆就可以立即给他开门。 37主人回来,看见奴仆警醒等候,奴仆就有福了!我实在告诉你们,主人必束上腰带请他们坐席,并亲自服侍他们。 38无论主人在深夜或黎明回家,若发现奴仆警醒等候,奴仆就有福了。

39“你们都知道,家主若知道贼什么时候来,一定不会让贼入屋偷窃。 40同样,你们也要做好准备,因为在你们意想不到的时候,人子就来了。”

忠仆和恶仆

41彼得问:“主啊!你这比喻是讲给我们听的,还是讲给众人听的呢?”

42主说:“谁是那个受主人委托管理家中大小仆役、按时分粮食给他们、又忠心又精明的管家呢? 43主人回家时,看见他尽忠职守,他就有福了。 44我实在告诉你们,主人一定会把所有产业都交给他管理。 45但他若以为主人不会那么快回来,就动手殴打仆婢、吃喝醉酒, 46主人会在他想不到的日子、不知道的时辰回来,严厉地惩罚12:46 “严厉地惩罚”或作“腰斩”。他,使他和不忠不信的人同受严刑。 47明知主人的意思却不准备,也不遵行主人吩咐的仆人,必受更重的责打。 48但因不知道而做了该受惩罚之事的仆人,必少受责打。多赐给谁,就向谁多取;多托付谁,就向谁多要。

家庭分裂

49“我来是要把火扔在地上,我多么希望这火已经燃烧起来。 50我有要受的‘洗礼’,我何等迫切地想完成这‘洗礼’啊! 51你们以为我来是要使天下太平吗?不!我告诉你们,我来是要使地上起纷争。 52从今以后,一家五口会彼此相争,三个人反对两个人,或是两个人反对三个人, 53父子相争,母女对立,婆媳反目。”

世事洞明

54然后,祂又对众人说:“你们看见云从西方升起,立刻说,‘快下雨了!’果然如此。 55南风一起,你们就说,‘天必燥热’,你们也说对了。 56你们这些伪善的人!既然懂得分辨天地气象,为什么不懂得分辨这个世代呢? 57你们为什么不自己明辨是非呢? 58如果你和告你的人要去对簿公堂,要尽量在路上与对方和解,以免被拉到审判官面前,审判官把你交给差役,差役把你关进监牢。 59我告诉你,除非你还清所欠的每一分钱,否则休想出来。”