Luka 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Luka 11:1-54

Yesu Afundisha Wanafunzi Wake Kuomba

(Mathayo 6:9-13; 7:7-11)

111:1 Lk 3:21; Yn 13:13Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomaliza kuomba, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tufundishe kuomba, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.”

211:2 Mt 3:211:2 Mt 6:9-13Akawaambia, “Mnapoomba, semeni:

“ ‘Baba yetu (uliye mbinguni),

jina lako litukuzwe,

ufalme wako uje.

(Mapenzi yako yafanyike

hapa duniani kama huko mbinguni.)

3Utupatie kila siku riziki yetu.

411:4 Mt 18:35; Mk 11:25; Mt 26:41; Yak 1:13Utusamehe dhambi zetu,

kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea.

Wala usitutie majaribuni

(bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu).’ ”

5Kisha akawaambia, “Ni nani miongoni mwenu mwenye rafiki yake, naye akamwendea usiku wa manane na kumwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. 6Kwa sababu rafiki yangu amekuja kutoka safarini, nami sina kitu cha kumpa.’

711:7 Mt 26:10“Kisha yule aliyeko ndani amjibu, ‘Usinisumbue. Mlango umefungwa, nami na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka nikupe chochote.’ 811:8 Lk 18:1-6Nawaambia, ingawa huyo mtu hataamka na kumpa hiyo mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ya kuendelea kwake kuomba, ataamka na kumpa kiasi anachohitaji.

911:9 Mt 7:711:9 Mt 7:7-11“Kwa hiyo nawaambia: Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. 10Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango.

11“Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba samaki, atampa nyoka badala yake? 12Au mtoto akimwomba yai atampa nge? 13Basi ikiwa ninyi mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa Roho Mtakatifu wale wamwombao!”

Yesu Na Beelzebuli

(Mathayo 12:22-30; Marko 3:20-27)

1411:14 Mt 9:32-3311:14 Mt 12:22Basi Yesu alikuwa anamtoa pepo mchafu kutoka kwa mtu aliyekuwa bubu. Yule pepo mchafu alipomtoka yule mtu aliyekuwa bubu, akaanza kuongea, nao umati wa watu ukashangaa. 1511:15 Mk 3:22; Mt 9:34Lakini wengine wakasema, “Anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli,11:15 Beelzebubu au Beelzebuli; ni mkuu wa pepo wachafu; pia 18, 19. yule mkuu wa pepo wachafu wote.” 1611:16 Mt 12:38Wengine ili kumjaribu wakataka awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

1711:17 Mt 9:34Yesu akajua mawazo yao, naye akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Nayo nyumba iliyogawanyika dhidi yake yenyewe itaanguka. 1811:18 Mt 4:10Kama Shetani amegawanyika mwenyewe, ufalme wake utasimamaje? Nawaambia haya kwa sababu ninyi mnadai ya kuwa mimi ninatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli. 1911:19 Mk 11:24; Yn 15:7; Yak 1:6; Yn 3:32; Mt 7:7Kama mimi natoa pepo wachafu kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu nao je, wao hutoa pepo wachafu kwa uwezo wa nani? Hivyo basi, wao ndio watakaowahukumu. 2011:20 Kut 8:19; Mt 3:2Lakini kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa kidole cha Mungu, basi Ufalme wa Mungu umewajia.

2111:21 Mt 12:29; Mk 3:17“Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha anapoilinda nyumba yake, mali yake iko salama. 2211:22 Isa 53:12; Kol 2:15Lakini mtu mwenye nguvu zaidi kumliko akimshambulia na kumshinda, yeye humnyangʼanya silaha zake zote alizozitegemea, na kuchukua nyara.

2311:23 Mt 12:30; Mk 9:40“Mtu asiyekuwa pamoja nami yu kinyume nami, na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, hutawanya.

Kurudi Kwa Pepo Mchafu

(Mathayo 12:43-45)

2411:24 Mt 12:43“Pepo mchafu amtokapo mtu, hutangatanga katika sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati. Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’ 25Naye arudipo na kuikuta ile nyumba imefagiliwa na kupangwa vizuri, 2611:26 2Pet 2:20ndipo huenda na kuchukua pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza.”

2711:27 Lk 23:29Ikawa Yesu alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katikati ya ule umati wa watu akapaza sauti akasema, “Limebarikiwa tumbo lililokuzaa na matiti uliyonyonya!”

2811:28 Ebr 4:12; Mit 8:32; Yn 14:21Yesu akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”

Ishara Ya Yona

(Mathayo 12:38-42)

2911:29 Mt 12:38; Yn 1:17; Mt 16:4Umati wa watu ulipokuwa unazidi kuongezeka, Yesu akaendelea kusema, “Hiki ni kizazi kiovu. Kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ya Yona. 3011:30 Yn 1:17; 2:10Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki. 3111:31 1Fal 10:1; 2Nya 9:1Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kuwahukumu watu wa kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Solomoni. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Solomoni. 3211:32 Yon 3:5Siku ya hukumu, watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona.

Taa Ya Mwili

(Mathayo 5:15; 6:22-23)

3311:33 Mt 5:15; Mk 4:21“Hakuna mtu yeyote awashaye taa na kuiweka mahali palipofichika au kuifunikia chini ya bakuli. Badala yake huiweka juu ya kinara chake, ili watu wote wanaoingia waone nuru. 3411:34 Mt 6:22; 2711:34 Mt 6:22; 23Jicho lako ni taa ya mwili wako. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote pia umejaa nuru. Lakini kama jicho ni bovu, mwili wako wote pia umejaa giza. 35Kwa hiyo, hakikisha kwamba nuru iliyoko ndani yako isiwe giza. 36Basi ikiwa mwili wako wote umejaa nuru, bila sehemu yake yoyote kuwa gizani, basi utakuwa na nuru kama vile taa ikuangazavyo kwa nuru yake.”

Yesu Awashutumu Mafarisayo Na Wanasheria

(Mathayo 23:1-36; Marko 12:38-40)

3711:37 Lk 7:36; 14:1Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimwalika nyumbani mwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi katika sehemu yake mezani. 3811:38 Mk 7:3-4Yule Farisayo akashangaa kwamba Yesu hakunawa kwanza kabla ya kula.

3911:39 Lk 7:13; Mt 23:25-26; Mk 7:20-23Ndipo Bwana akamwambia, “Sasa, enyi Mafarisayo, mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyangʼanyi na uovu. 4011:40 Lk 12:20; 1Kor 15:36Enyi wapumbavu! Hamjui kuwa yeye aliyetengeneza nje ndiye alitengeneza na ndani pia? 4111:41 Lk 12:33; Mdo 10:15Basi toeni sadaka ya vile mlivyo navyo, na tazama, vitu vyote vitakuwa safi kwenu.

4211:42 Lk 18:12; Kum 6:5; Mik 6:8; Mt 23:23“Lakini ole wenu, Mafarisayo, kwa maana mnampa Mungu zaka za mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga, lakini mnapuuza haki na upendo wa Mungu. Iliwapasa kufanya haya ya pili bila kupuuza hayo ya kwanza.

4311:43 Mt 23:6-7; Mk 12:38-39“Ole wenu Mafarisayo, kwa sababu ninyi mnapenda kukalia viti vya mbele katika masinagogi, na kusalimiwa kwa heshima masokoni.

4411:44 Mt 23:27-35“Ole wenu, kwa sababu ninyi ni kama makaburi yasiyokuwa na alama, ambayo watu huyakanyaga pasipo kujua.”

4511:45 Mt 22:35Mtaalamu mmoja wa sheria akamjibu, akasema, “Mwalimu, unaposema mambo haya, unatutukana na sisi pia.”

4611:46 Mt 23:4Yesu akamjibu, “Nanyi wataalamu wa sheria, ole wenu, kwa sababu mnawatwika watu mizigo mizito ambayo hawawezi kubeba, wala ninyi wenyewe hamwinui hata kidole kimoja kuwasaidia.

4711:47 Mt 23:29“Ole wenu, kwa sababu ninyi mnajenga makaburi ya manabii waliouawa na baba zenu. 4811:48 Mt 23:29-32; Mdo 7:51-53Hivyo ninyi mwashuhudia na mnathibitisha kile baba zenu walichofanya. Wao waliwaua manabii, nanyi mnawajengea makaburi. 4911:49 1Kor 1:24; Kol 2:3Kwa sababu ya jambo hili, Mungu katika hekima yake alisema, ‘Tazama, nitatuma kwao manabii na mitume, nao watawaua baadhi yao na wengine watawatesa.’ 50Kwa hiyo kizazi hiki kitawajibika kwa ajili ya damu ya manabii iliyomwagwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, 5111:51 Mwa 4:8; 2Nya 24:20-21; Mt 23:35-36tangu damu ya Abeli mpaka damu ya Zekaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Naam, nawaambia, kizazi hiki kitawajibika kwa haya yote.

5211:52 Mt 23:13“Ole wenu ninyi wataalamu wa sheria, kwa sababu mmeuondoa ufunguo wa maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”

53Yesu alipoondoka huko, walimu wa sheria na Mafarisayo wakaanza kumpinga vikali na kumsonga kwa maswali, 5411:54 Mt 12:10; Mk 12:13wakivizia kumkamata kwa kitu atakachosema ili wamshtaki.