Kutoka 9 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 9:1-35

Pigo La Tano: Vifo Vya Mifugo

19:1 Kut 8:1Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo Bwana, Mungu wa Waebrania asemalo: “Waachie watu wangu waende ili wapate kuniabudu.” 2Kama ukikataa kuwaachia waende, nawe ukiendelea kuwashikilia, 39:3 Kut 7:4; 1Sam 5:6; Ay 13:21; Za 32:4; 39:10; 78:50; Mdo 13:11; Law 26:25; Amo 4:10mkono wa Bwana utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ngʼombe wako, kondoo na mbuzi. 49:4 Kut 8:23Lakini Bwana ataweka tofauti kati ya mifugo ya Israeli na ile ya Misri, kwamba hakuna mnyama wa Mwisraeli atakayekufa.’ ”

5Bwana akaweka wakati na kusema, “Kesho Bwana atalitenda hili katika nchi.” 69:6 Kut 11:5; 12:29; Za 78:48-50Siku iliyofuata Bwana akalitenda: Mifugo yote ya Wamisri ikafa, lakini hakuna hata mnyama mmoja wa wana wa Israeli aliyekufa. 79:7 Kut 7:14, 22; 8:32Farao akatuma watu kuchunguza, nao wakakuta kuwa hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Lakini moyo wa Farao haukukubali kuwaachia watu waende.

Pigo La Sita: Majipu

8Kisha Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Chukueni majivu ya tanuru, naye Mose ayarushe angani mbele ya Farao. 99:9 Law 13:18-19; 2Fal 20:7; Ay 2:7; Isa 38:21; Ufu 16:2Yatakuwa vumbi jepesi juu ya nchi yote ya Misri, pia yatatokea majipu yenye kufura juu ya watu na wanyama katika nchi yote.”

10Basi wakachukua majivu kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. Mose akayarusha hewani, nayo majipu yenye kufura yakatokea miilini mwa watu na wanyama. 119:11 Kut 8:18Waganga hawakuweza kusimama mbele ya Mose kwa sababu ya majipu yale yaliyokuwa miilini mwao na juu ya miili ya Wamisri wote. 129:12 Kut 4:21; 7:4Lakini Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa amemwambia Mose.

Pigo La Saba: Mvua Ya Mawe

139:13 Kut 3:18Kisha Bwana akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi, usimame mbele ya Farao, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Waebrania: Waachie watu wangu waende, ili kwamba waweze kuniabudu, 149:14 Kut 8:10; 15:11; 1Sam 2:2; 2Sam 7:22; 1Fal 8:23; 1Nya 17:20; Za 35:10; 71:19; 86:8; 89:6; Isa 46:9; Yer 10:6; Mik 7:18au wakati huu nitaleta mapigo yangu yenye nguvu dhidi yako, maafisa wako na watu wako, ili upate kujua kuwa hakuna mwingine kama Mimi katika dunia yote. 159:15 Kut 3:20Kwa kuwa mpaka sasa ningelikuwa nimenyoosha mkono wangu na kukupiga wewe na watu wako kwa pigo ambalo lingekufutilia mbali juu ya nchi. 169:16 Mit 16:4; Kut 14:4, 17, 31; Za 20:6; 25:11; 68:28; 71:18; 106:8; 109:21; Rum 9:17Lakini nimekuinua wewe kwa kusudi hili hasa, ili nipate kukuonyesha uwezo wangu, na ili Jina langu lipate kutangazwa duniani yote. 17Bado unaendelea kujiinua juu ya watu wangu, wala hutaki kuwaachia waende. 189:18 Yos 10:11; Za 78:47-48; 105:32; 148:8; Isa 30:30; Eze 38:22; Hag 2:17; Kut 9:24; 10:6Kwa hiyo, kesho wakati kama huu nitaleta mvua mbaya sana ya mawe ambayo haijapata kunyesha katika nchi ya Misri, tangu siku ilipoumbwa mpaka leo. 19Sasa toa amri urudishe wanyama wote watoke malishoni na chochote ambacho kipo mashambani waje mpaka mahali pa usalama, kwa sababu mvua ya mawe itanyesha juu ya kila mtu na kila mnyama ambaye hajaletwa ndani ambao bado wako nje mashambani, nao watakufa.’ ”

209:20 Mit 13:13Wale maafisa wa Farao ambao waliliogopa neno la Bwana wakafanya haraka kuwaleta watumwa wao na mifugo yao ndani. 219:21 Mwa 19:14; Eze 33:4-5Lakini wale waliopuuza neno la Bwana wakawaacha watumwa wao na mifugo yao shambani.

22Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili kwamba mvua ya mawe inyeshe juu ya Misri yote, juu ya watu, wanyama na juu ya kila kitu kiotacho katika mashamba ya Misri.” 239:23 Kut 20:18; 1Sam 12:17; Za 18:13; 29:3; 68:33; 77:17; 104:7; Ufu 8:7; 16:21Mose alipoinyoosha fimbo yake kuelekea angani, Bwana akatuma ngurumo na mvua ya mawe, umeme wa radi ulimulika hadi nchi. Kwa hiyo Bwana akaifanya mvua ya mawe kunyesha juu ya nchi ya Misri, 24mvua ya mawe ikanyesha na radi ikamulika pote. Ikawa dhoruba ya kutisha ambayo haijakuwako katika nchi ya Misri, tangu nchi hiyo iwe taifa. 259:25 Za 105:32-33; Eze 13:13Mvua ya mawe ikaharibu kila kitu katika nchi ya Misri kilichokuwa katika mashamba, watu na wanyama, ikaharibu kila kitu kinachoota mashambani na kuvunja kila mti. 269:26 Isa 32:18-20; Kut 10:23; 11:7; 12:13; Amo 4:7Mahali pekee ambapo mvua ya mawe haikunyesha ni nchi ya Gosheni, ambako Waisraeli waliishi.

279:27 Kut 10:16; Hes 14:40; Kum 1:41; Yos 7:11; Amu 10:10; 1Sam 15:24; 24:17; 26:21; Za 11:7; 116:5; 119:135; 129:4; 145:17; Yer 12:1; Mao 1:18Ndipo Farao akawaita Mose na Aroni akawaambia, “Wakati huu nimetenda dhambi. Bwana ni mwenye haki, mimi na watu wangu ni wakosaji. 289:28 Kut 8:8; Mdo 8:24Mwombeni Bwana, kwa kuwa tumepata ngurumo na mvua za mawe za kututosha. Nitawaachia mwondoke; hamtahitaji kungoja zaidi.”

299:29 1Fal 8:22; Ay 11:13; Za 77:2; 88:9; 143:6; Isa 1:15; Kut 19:5; Ay 41:11; Za 24:1; 50:12; 1Kor 10:26Mose akamjibu, “Nitakapokuwa nimetoka nje ya mji, nitanyoosha mikono yangu juu kumwomba Bwana. Ngurumo zitakoma na hapatakuwepo mvua ya mawe tena, ili upate kujua kuwa, nchi ni mali ya Bwana. 309:30 Kut 8:29Lakini ninajua kuwa wewe na maafisa wako bado hammwogopi Bwana Mungu.”

319:31 Kum 8:8; Rut 1:22; 2:23; 2Sam 14:30; 17:28; Isa 28:25; Eze 4:9(Kitani na shayiri viliharibiwa, kwa kuwa shayiri ilikuwa na masuke, na kitani ilikuwa katika kutoa maua. 329:32 Isa 28:25Hata hivyo, ngano na jamii nyingine ya ngano hazikuharibiwa kwa sababu zilikuwa hazijakomaa bado.)

33Kisha Mose akaondoka kwa Farao akaenda nje ya mji. Mose akanyoosha mikono yake kuelekea kwa Bwana, ngurumo na mvua ya mawe vikakoma, mvua haikuendelea tena kunyesha nchini. 34Farao alipoona kwamba mvua ya mawe na ngurumo zimekoma, akafanya dhambi tena. Yeye na maafisa wake wakafanya mioyo yao kuwa migumu. 359:35 Kut 4:2Kwa hiyo moyo wa Farao ukawa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waende, kama vile Bwana alivyokuwa amesema kupitia Mose.