Kutoka 35 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 35:1-35

Masharti Ya Sabato

135:1 Kut 34:32Mose akakusanya jumuiya yote ya Waisraeli na kuwaambia, “Haya ndiyo mambo ambayo Bwana amewaamuru ninyi mfanye: 235:2 Law 23:3; Mwa 2:3; Kut 34:21; Kum 5:13-14; Kut 31:14, 15; Hes 15:32; Lk 13:14Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba itakuwa takatifu kwenu, Sabato ya kupumzika kwa Bwana. Yeyote atakayefanya kazi yoyote siku hiyo ni lazima auawe. 335:3 Kut 16:23Msiwashe moto mahali popote katika makazi yenu siku ya Sabato.”

Vifaa Kwa Ajili Ya Maskani Ya Mungu

(Kutoka 25:1-9)

435:4 Kut 25:1, 2Mose akaiambia jumuiya yote ya Waisraeli, “Hili ndilo Bwana aliloamuru: 535:5 Kut 25:2; 2Kor 9:7Toeni sadaka kwa Bwana kutoka mali mliyo nayo. Kila mmoja aliye na moyo wa kupenda atamletea Bwana sadaka ya dhahabu, fedha na shaba; 6nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi; singa za mbuzi; 7ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo;35:7 Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. mbao za mshita; 835:8 Kut 25:6mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; 9vito vya shohamu, na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani.

1035:10 Kut 31:6; 39:43; 1Fal 7:14; Isa 28:26“Wote wenye ujuzi miongoni mwenu inawapasa kuja na kutengeneza kila kitu Bwana alichoamuru: 1135:11 Kut 26:1-37; 36:8-38; Mdo 7:44, 45; Ebr 8:2, 5; 9:2-11; Ufu 21:3Maskani pamoja na hema lake na kifuniko chake, vibanio, mihimili, mataruma, nguzo na vitako; 1235:12 Kut 25:10-22; 37:1-9; 26:33Sanduku la Agano pamoja na mipiko yake, kifuniko cha kiti cha rehema na pazia linalokizuia; 1335:13 Kut 25:23-30; 37:10-16meza na mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote, mikate ya Wonyesho; 1435:14 Kut 25:31kinara cha taa kwa ajili ya mwanga pamoja na vifaa vyake vyote, taa na mafuta kwa ajili ya mwanga; 1535:15 Kut 30:1-6; 37:26-28; 30:34-38; 26:36; 1Sam 2:28; 1Nya 23:13; 2Nya 29:11; Lk 1:9madhabahu ya kufukiza uvumba pamoja na mipiko yake, mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri; pazia la mlangoni mahali pa kuingilia ndani ya maskani; 1635:16 Kut 27:1-8; 38:1-7; 30:18madhabahu ya sadaka za kuteketeza pamoja na wavu wake wa shaba, mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote; sinia la shaba pamoja na tako lake; 1735:17 Kut 27:9; 38:9-20pazia la eneo la ua pamoja na nguzo zake na vitako vyake, pazia la ingilio la kwenye ua; 1835:18 Kut 27:19; 38:20vigingi vya hema kwa ajili ya maskani pamoja na ua na kamba zake; 1935:19 Kut 28:2; 31:10; 39:1mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu kwa ajili ya kuhani Aroni, na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani.”

20Ndipo jumuiya yote ya Waisraeli ilipoondoka mbele ya Mose, 2135:21 Kut 25:2; 36:2; 1Nya 28:2, 9; 29:9; Ezr 7:27; 2Kor 8:12; 9:7na kila mmoja aliyependa na ambaye moyo wake ulimsukuma alikuja na kuleta sadaka kwa Bwana, kwa ajili ya kazi katika Hema la Kukutania, kwa ajili ya huduma yake yote na kwa ajili ya mavazi matakatifu. 22Wote waliokuwa na utayari, wanaume kwa wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kama sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana. 2335:23 Kut 39:1; 1Nya 29:8Kila mmoja aliyekuwa na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi, au singa za mbuzi, ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, au ngozi za pomboo, wakavileta. 24Wale waliotoa sadaka ya fedha au shaba wakavileta kama sadaka kwa Bwana, na kila aliyekuwa na mti wa mshita kwa ajili ya kazi yoyote ile akauleta. 2535:25 Kut 28:3; 31:6; 36:1; 2Fal 23:7; Mit 31:19-24Kila mwanamke aliyekuwa na ujuzi alisokota kwa mikono yake na alileta kile alichosokota, iwe ni nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi. 2635:26 Kut 25:2; 1Nya 29:6-8Wanawake wote waliopenda na waliokuwa na ujuzi wakasokota singa za mbuzi. 27Viongozi wakaleta vito vya shohamu pamoja na vito vingine vya thamani kwa ajili ya kuweka kwenye kisibau na kwenye kifuko cha kifuani. 2835:28 Kut 25:6Wakaleta pia vikolezi na mafuta ya zeituni kwa ajili ya mwanga, kwa ajili ya mafuta ya upako na kwa ajili ya uvumba wenye harufu nzuri. 2935:29 Kut 25:2-7; 36:3; 2Fal 12:4Waisraeli wote waume kwa wake waliokuwa wanapenda wakaleta mbele za Bwana kwa hiari yao wenyewe sadaka kwa ajili ya kazi yote ya Bwana aliyokuwa amewaagiza kuifanya kupitia kwa Mose.

Bezaleli Na Oholiabu

(Kutoka 31:1-11)

30Kisha Mose akawaambia Waisraeli, “Tazameni, Bwana amemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, 3135:31 2Nya 2:7, 14naye amemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, na uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, 32ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, 33kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi wa kupendeza. 3435:34 Kut 31:6; 2Nya 2:14Tena amempa yeye pamoja na Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, uwezo wa kufundisha wengine. 3535:35 Kut 31:3, 6; 36:1, 2; 1Fal 7:14; 1Nya 2:14; Isa 28:26; Yak 1:5Amewajaza ustadi wa kufanya kazi za aina zote zifanywazo na mafundi, na wenye kubuni michoro, pia na watarizi kwa rangi za buluu, zambarau, nyekundu na kitani safi, na wafumaji: wote wakiwa mafundi na wabunifu hodari.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

出埃及记 35:1-35

安息日的条例

1摩西招聚以色列全体会众,对他们宣布说:“以下是耶和华吩咐你们遵守的事。 2一周可以工作六天,但第七天是你们为耶和华守的圣日,是完全休息的安息日。凡在这一天工作的,必被处死。 3在安息日,你们的任何住处都不可生火。”

为造圣幕奉献

4摩西以色列全体会众说:“以下是耶和华给你们的吩咐。

5“你们要献物品给耶和华。凡慷慨乐捐的,都可以把下列物品献给耶和华为礼物,即金、银、铜, 6蓝色、紫色和朱红色毛线,细麻,山羊毛, 7染成红色的公羊皮,海狗皮,皂荚木, 8灯油,制作膏油和香的香料, 9镶嵌在以弗得和胸牌上的红玛瑙及其他宝石。

10“你们当中的能工巧匠都要来建造耶和华所吩咐的物件, 11即圣幕和圣幕的罩棚、顶盖、钩子、木板、横闩、柱子和带凹槽的底座; 12约柜和抬约柜的横杠、施恩座和遮掩约柜的幔子; 13桌子和抬桌子的横杠、桌上的一切器具和供饼; 14灯台和灯台用的器具、灯盏和灯油; 15香坛和抬香坛的横杠、膏油和芬芳的香;圣幕门口的帘子; 16燔祭坛、祭坛的铜网、抬祭坛的横杠、祭坛用的一切器具、洗濯盆和盆座; 17院子的帷幔、悬挂幔子的柱子和底座、院子入口的门帘; 18圣幕及院子用的橛子和绳子; 19在圣所供职时穿的精制礼服、亚伦祭司的圣衣及其众子供祭司之职时穿的衣服。”

20之后,以色列全体会众便从摩西面前退去。 21凡心里有感动又甘愿奉献的,都把礼物拿来献给耶和华,作会幕、会幕中的一切器具及圣衣之用。 22凡甘心奉献的,不论男女,都把别针、耳环、戒指、项链等各样金饰拿来献给耶和华。 23凡有蓝色、紫色和朱红色毛线,细麻,山羊毛,染成红色的公羊皮,海狗皮的,都把它们拿来了。 24凡奉献银器和铜器的,都拿来献给耶和华。凡有皂荚木的,只要用得上,都拿来奉献。 25凡善于纺线的妇女,都把亲手纺成的细麻和蓝色、紫色、朱红色毛线拿来奉献。 26凡心里受感动又善于纺织的妇女都来纺山羊毛。 27众首领奉献了红玛瑙和其他宝石,用来镶嵌在以弗得和胸牌上。 28他们又献出香料和油,用来做香、点灯、做膏油。 29以色列人,不论男女、凡是甘心乐意奉献的,都把礼物带来献给耶和华,好完成耶和华借摩西吩咐他们的一切工作。

30摩西以色列人说:“看啊,耶和华已经亲自在犹大支派中选出户珥的孙子、乌利的儿子比撒列31上帝的灵已经充满他,使他有聪明智慧,精于各种技能和手艺, 32能用金、银和铜制造精巧的器具, 33又能雕刻和镶嵌宝石,精通木工和各种手艺。 34耶和华又使他与支派亚希撒抹的儿子亚何利亚伯有能力教授别人。 35耶和华使他们成为能工巧匠,精通各样技艺,包括雕刻、图案设计、纺织,以及用细麻和蓝色、紫色、朱红色毛线刺绣。”