Kutoka 31 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 31:1-18

Bezaleli Na Oholiabu

(Kutoka 35:30–36:1)

1Ndipo Bwana akamwambia Mose, 231:2 Kut 36:1-2; 37:1; 38:22; 1Nya 21:20; 2Nya 1:5; Kut 17:10“Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, 331:3 Kut 28:3; 1Fal 7:14; 1Kor 12:4; Kut 35:31; Isa 28:26nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, 4ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, 5kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi. 631:6 Kut 36:1-2; 38:23; 1Fal 7:14; 2Nya 2:14Tena nimemteua Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, ili kumsaidia. Pia mafundi wote nimewapa ustadi wa kutengeneza kila kitu nilichokuamuru wewe: 731:7 Kut 36:8-38; 37:1-6; 40:20Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda pamoja na kiti cha rehema juu yake, pia na vifaa vyote vya kwenye hema, 831:8 Kut 37:10-24; Law 24:4; Kut 37:25-28meza na vifaa vyake, kinara cha taa cha dhahabu safi na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba, 931:9 Kut 38:3; Hes 4:14; Kut 30:18madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, sinia na kinara chake, 1031:10 Kut 28:2; 39:1, 41pamoja na mavazi matakatifu yaliyofumwa ya kuhani Aroni, na mavazi kwa ajili ya wanawe wakati wanahudumu katika kazi ya ukuhani, 1131:11 Kut 30:22-32; 37:29; 25:6-9pia mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri kwa ajili ya Mahali Patakatifu. Watavitengeneza sawasawa kama vile nilivyokuagiza wewe.”

Sabato

12Kisha Bwana akamwambia Mose, 1331:13 Kut 20:8; Isa 56:4; Eze 20:12, 20; Kut 29:42; Law 11:44; 20:8; Eze 37:28“Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni lazima mzishike Sabato zangu. Hii itakuwa ni ishara kati yangu na ninyi kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili mpate kujua kwamba Mimi Ndimi Bwana, niwafanyaye ninyi watakatifu.

1431:14 Kut 35:2; Hes 15:32-36“ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Yeyote atakayeinajisi lazima auawe, yeyote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akafie mbali na watu wake. 1531:15 Kut 20:8-11; 35:2; Law 16:29; 23:3; Hes 29:7; Mwa 2:3Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, takatifu kwa Bwana. Yeyote afanyaye kazi yoyote siku ya Sabato ni lazima auawe. 1631:16 Kut 20:8Waisraeli wataishika Sabato, kuiadhimisha kwa vizazi vijavyo kuwa Agano la milele. 1731:17 Mwa 2:2-3; Kut 20:9; Isa 56:2; 58:13; 66:23; Yer 17:21-22; Eze 20:12, 20Itakuwa ishara kati yangu na Waisraeli milele, kwa kuwa kwa muda wa siku sita Bwana aliumba mbingu na dunia, na siku ya saba akaacha kufanya kazi, akapumzika.’ ”

1831:18 Kut 19:11; 24:12; 2Kor 3:3; Ebr 9:4; Kut 32:15-16; 34:1; 28; Kum 4:30; 9:10Bwana alipomaliza kusema na Mose juu ya Mlima Sinai, Mungu akampa vile vibao viwili vya Ushuhuda, vibao vya mawe vilivyoandikwa kwa kidole cha Mungu.