Kutoka 30 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 30:1-38

Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba

(Kutoka 37:25-28)

130:1 Kut 40:5, 26; Hes 4:11; 1Fal 6:20; Eze 41:22; Kut 25:6; 37:29; Lk 1:11; Ebr 9:4; Ufu 8:3“Tengeneza madhabahu kwa mbao za mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba. 230:2 Kut 27:2; Ufu 9:13Madhabahu hayo yawe mraba, urefu na upana wake dhiraa moja,30:2 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. na kimo cha dhiraa mbili,30:2 Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90. nazo pembe zake zitakuwa kitu kimoja nayo. 330:3 Kut 25:11Funika hayo madhabahu juu na pande zote na pia pembe zake kwa dhahabu safi, na uifanyizie ukingo wa dhahabu kuizunguka. 430:4 Kut 25:12Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, ziwe mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko itumikayo kuibebea madhabahu. 530:5 Kut 25:13Tengeneza mipiko kwa miti ya mshita na uifunike kwa dhahabu. 630:6 Kut 25:22; 26:34Weka hayo madhabahu mbele ya lile pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, lililo mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya Sanduku la Ushuhuda, mahali ambapo nitakutana nawe.

730:7 Kut 26:6; 40:27; Hes 3:10; Kum 33:10; 1Sam 2:28; 1Nya 6:49; 2Nya 2:4; 26:18“Itampasa Aroni kufukiza uvumba wenye harufu nzuri juu ya madhabahu kila siku asubuhi wakati anapowasha zile taa. 830:8 Kut 25:37; 29:42Itampasa afukize uvumba tena wakati anapowasha taa wakati wa machweo ili uvumba ufukizwe daima mbele za Bwana kwa vizazi vijavyo. 930:9 Law 10:1; Hes 16:7, 40Usifukize uvumba mwingine wowote juu ya madhabahu haya au sadaka nyingine yoyote ya kuteketezwa wala sadaka ya nafaka, wala usimimine sadaka ya kinywaji juu yake. 1030:10 Law 16:2; 9:7; 16:18-19; 23:27-28; 25:9; Kut 29:14; Law 4:3; 6:25; 7:7; 8:2; 14; Hes 6:11; Kut 29:42Mara moja kwa mwaka Aroni atafanya upatanisho juu ya pembe za hayo madhabahu. Upatanisho huu wa mwaka lazima ufanywe kwa damu ya sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa vizazi vijavyo. Ni takatifu sana kwa Bwana.”

Fedha Ya Upatanisho

11Naye Bwana akamwambia Mose, 1230:12 Kut 38:25; Hes 1:2, 49; 4:2, 29; 14:29; 14:29; 26:2; 31:26; 2Sam 24:1; 2Fal 12:4; Kut 38:26; Hes 31:50; Mt 20:28; Hes 14:12; Kum 28:58-61; 2Sam 24:13; 1Fal 8:37“Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwa Bwana fidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu. 1330:13 Kut 38:24-26; Law 15:15; 27:3; Hes 3:47; 7:13; 18:16; Eze 4:10; 45:12; Mt 17:24Kila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli,30:13 Nusu shekeli ni sawa na gramu 6. kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.30:13 Gera 20 ni sawa na shekeli moja au gramu 12. Hii nusu shekeli ni sadaka kwa Bwana. 1430:14 Kut 38:26; Hes 14:29; 26:2; 32:11; 2Nya 25:5Wote wale wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwa Bwana. 1530:15 Mit 22:2; Efe 6:9Matajiri hawatalipa zaidi ya nusu shekeli, nao maskini hawatatoa pungufu wakati mnatoa sadaka kwa Bwana kwa kufanya upatanisho wa nafsi zenu. 1630:16 Kut 38:25-28; 2Nya 24:5; Hes 31:54Utapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.”

Sinia La Kunawia

17Kisha Bwana akamwambia Mose, 1830:18 Kut 31:9; 35:16; 38:8; 39:39; 40:7, 30; 1Fal 7:38; 2Nya 4:6“Tengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kwa ajili ya kunawia. Liweke kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, kisha uweke maji ndani yake. 1930:19 Kut 40:31-32; Yn 13:10; Kut 29:4; 40:12; Law 8:6; Za 26:6; Ebr 10:22Aroni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji yatokayo katika hilo sinia. 2030:20 Kut 28:43Wakati wowote wanapoingia katika Hema la Kukutania, watanawa kwa maji ili kwamba wasije wakafa. Pia, wanapokaribia madhabahu ili kuhudumu kwa kuleta sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, 2130:21 Kut 27:21; 28:43; 29:42watanawa mikono na miguu yao ili kwamba wasije wakafa. Hii itakuwa ni amri ya kudumu kwa ajili ya Aroni na wazao wake kwa vizazi vijavyo.”

Mafuta Ya Upako

2230:22 Mwa 43:11; 37:25; Mit 7:17; Wim 4:14; Isa 43:24; Yer 6:20Kisha Bwana akamwambia Mose, 2330:23 Wim 4:14; Eze 27:22; Za 45:8; Yer 6:20“Chukua vikolezi bora vifuatavyo: shekeli 50030:23 Shekeli 500 ni sawa na kilo 6. za manemane ya maji, shekeli 25030:23 Shekeli 250 ni sawa na kilo 3. za mdalasini wenye harufu nzuri, shekeli 250 za miwa yenye harufu nzuri, 2430:24 Za 45:8; Eze 27:19; Kut 29:40shekeli 500 za aina nyingine ya mdalasini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, pia hini30:24 Hini moja ni sawa na lita 4. ya mafuta ya zeituni. 2530:25 1Nya 9:30; Kut 37:29; 29:7; 1Sam 9:16; Hes 35:25; Za 133:2Vitengeneze vikolezi hivi kuwa mafuta matakatifu ya upako yenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Yatakuwa mafuta matakatifu ya upako. 2630:26 Kut 40:9; Law 8:10; Hes 7:1Kisha yatumie kupaka hilo Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda, 27meza na vifaa vyake vyote, kinara cha taa na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba, 28madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote na sinia pamoja na kitako chake. 2930:29 Law 8:10-11; 6:18, 27; Kut 29:37; Mt 23:17Utaviweka wakfu ili viwe vitakatifu sana na kila kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu.

3030:30 Kut 29:7; Law 8:2, 12, 30; 10:7; 16:32; 21:10-12; 1Nya 15:12; Za 133:2; Kut 28:41“Mtie Aroni na wanawe mafuta na uwaweke wakfu ili waweze kunitumikia katika kazi ya ukuhani. 3130:31 Kut 29:7, 42Waambie Waisraeli, ‘Haya yatakuwa mafuta matakatifu yangu ya upako kwa vizazi vijavyo. 32Usiyamimine juu ya miili ya wanadamu wala usitengeneze mafuta ya aina nyingine kwa utaratibu huu. Ni mafuta matakatifu na ni lazima myaone kuwa ni matakatifu. 3330:33 Mwa 17:14; Law 7:20, 21Mtu yeyote atakayetengeneza manukato kama hayo na yeyote atakayeyamimina juu ya mtu yeyote ambaye si kuhani atakatiliwa mbali na watu wake.’ ”

Uvumba

3430:34 Wim 3:6; Kut 25:6; 37:29Kisha Bwana akamwambia Mose, “Chukua vikolezi vyenye harufu nzuri vifuatavyo: natafi, shekelethi, kelbena na uvumba safi vyote vikiwa na vipimo sawa, 3530:35 Kut 25:6pia tengeneza mchanganyiko wa uvumba wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Utiwe chumvi ili upate kuwa safi na mtakatifu. 3630:36 Kut 29:37; Law 2:3Saga baadhi yake kuwa unga na uweke mbele ya Sanduku la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, mahali ambapo nitakutana nawe. Itakuwa takatifu sana kwenu. 37Msitengeneze uvumba mwingine wowote wa namna hii kwa ajili yenu wenyewe; uoneni kuwa ni mtakatifu kwa Bwana. 38Yeyote atakayetengeneza uvumba kama huu ili kufurahia harufu yake nzuri lazima akatiliwe mbali na watu wake.”