Kutoka 29 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 29:1-46

Kuweka Wakfu Makuhani

(Walawi 8:1-36)

129:1 Law 20:7; Yos 3:5; 1Nya 15:12; Eze 43:23“Hili ndilo utakalofanya ili kuwaweka wakfu makuhani ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani: Chukua fahali mchanga mmoja na kondoo dume wawili wasio na dosari. 229:2 Law 2:1-4; 6:19-23; Hes 6:15Kutokana na unga laini wa ngano usiotiwa chachu, tengeneza mikate na maandazi yaliyokandwa kwa mafuta, pamoja na mikate midogo myembamba. 3Viwekwe vyote ndani ya kikapu na kuvitoa pamoja na yule fahali na wale kondoo dume wawili. 429:4 Kut 40:12; Law 14:8; 16:4; Ebr 10:22Kisha mlete Aroni na wanawe kwenye lango la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. 529:5 Kut 28:2; 28:8; Law 8:7Chukua yale mavazi na umvike Aroni koti, joho la kisibau na kisibau chenyewe pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kisibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliosukwa kwa ustadi. 629:6 Kut 28:39; Isa 3:23; Zek 3:5; Kut 28:36Weka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu ishikamane na hicho kilemba. 729:7 Kut 28:41; 30:25-31; 37:29; Law 21:10; 1Sam 10:1; Za 89:20; 133:2; 141:5; Hes 35:25; Za 133:1, 2; Isa 61:1Chukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake. 829:8 Kut 28:4; Law 16:4Walete wanawe na uwavike makoti, 929:9 Kut 28:40; 27:21; 40:15; Hes 3:10; 18:7; 25:13; Kum 18:5; Amu 17:5; 1Sam 2:30; 1Fal 12:31pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Aroni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Aroni na wanawe.

1029:10 Law 1:4; 4:15; 16:21; Hes 8:12“Mlete yule fahali mbele ya Hema la Kukutania, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake. 1129:11 Law 1:5, 11; 4:24; 6:16, 25; 14:13Mchinje huyo fahali mbele za Bwana kwenye mlango wa Hema la Kukutania. 1229:12 Kut 27:2; Law 4:7; 9:9Chukua sehemu ya damu ya huyo fahali na kuipaka kwenye pembe za hayo madhabahu kwa kidole chako, na damu iliyobaki uimwage sehemu ya chini ya madhabahu. 1329:13 Law 1:8; 3:3-9; 4:10; 6:12; 9:10; Hes 18:17; 1Sam 2:15; 1Fal 8:64; 2Nya 7:7; 29:35; 35:14; Isa 43:24; Eze 44:15; Kut 12:9Kisha chukua mafuta yote ya huyo mnyama ya sehemu za ndani, yale yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, uviteketeze juu ya madhabahu. 1429:14 Nah 3:6; Mal 2:3; Law 4:12, 21; 16:17; Hes 19:3-5; Ebr 13:11; Hes 4:12, 21Lakini nyama ya huyo fahali na ngozi yake na matumbo yake utavichoma nje ya kambi. Hii ni sadaka ya dhambi.

1529:15 2Nya 29:23; 29:18; Mwa 8:21; 2Kor 2:15“Chukua mmoja wa wale kondoo dume, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake. 16Mchinje huyo kondoo dume, chukua damu yake na uinyunyize pande zote za hayo madhabahu. 17Mkate huyo kondoo dume vipande vipande na usafishe sehemu za ndani pamoja na miguu, ukiviweka pamoja na kichwa na vipande vingine. 1829:18 Mwa 8:21; 2Kor 2:15Kisha mteketeze huyo kondoo dume mzima juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

1929:19 Kut 30:25; Law 8:30“Mchukue yule kondoo dume mwingine, naye Aroni na wanawe waweke mikono yao juu ya kichwa chake. 2029:20 Law 14:14, 25; 1:5; 3:2Mchinje, uchukue sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye masikio ya Aroni na wanawe, kwenye vidole gumba vya mikono yao ya kuume, pia kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kuume. Kisha nyunyiza hiyo damu pande zote za madhabahu. 2129:21 Ebr 9:22; Kut 30:25-31Pia chukua sehemu ya damu iliyo juu ya madhabahu na sehemu ya mafuta ya upako, umnyunyizie Aroni na mavazi yake, pia wanawe na mavazi yao. Ndipo Aroni na wanawe pamoja na mavazi yao watakuwa wamewekwa wakfu.

22“Chukua mafuta ya huyu kondoo dume, mafuta ya mkia, mafuta ya sehemu za ndani yale yanayofunika ini, figo zote mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Huyo ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwaweka wakfu.) 2329:23 Law 8:26Kutoka kwenye kile kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu, kilichoko mbele za Bwana, chukua mkate, andazi lililokandwa kwa mafuta na mkate mdogo mwembamba. 2429:24 Law 7:30; 9:21; 10:15; 14:12; 23:11, 20; Hes 6:20; 8:11-15Viweke vitu hivi vyote mikononi mwa Aroni na wanawe na uviinue mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa. 2529:25 Law 8:28Kisha vichukue vitu hivyo kutoka mikononi mwao, uviteketeze juu ya madhabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kupendeza kwa Bwana, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 2629:26 Law 7:31-34Baada ya kuchukua kidari cha huyo kondoo dume wa kuwekwa wakfu kwa Aroni, kiinue mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa, nayo itakuwa fungu lako.

2729:27 Kut 22:29; Law 7:31-34; Hes 18:11-12; Kum 18:3“Weka wakfu zile sehemu za kondoo dume aliyetumika kwa kumweka wakfu Aroni na wanawe: kidari kile kilichoinuliwa na lile paja lililotolewa. 2829:28 Law 7:30-34; 10:15Siku zote hili litakuwa fungu la kawaida kutoka kwa Waisraeli kwa ajili ya Aroni na wanawe. Hili ni toleo la Waisraeli watakalotoa kwa Bwana kutoka sadaka zao za amani.

2929:29 Kut 28:2; Law 16:4; Hes 20:28“Mavazi matakatifu ya Aroni yatakuwa ya wazao wake ili kwamba waweze kutiwa mafuta na kuwekwa wakfu wakiwa wameyavaa. 3029:30 Law 6:22; Hes 3:3; 20:28Mwana atakayeingia mahali pake kuwa kuhani na kuja kwenye Hema la Kukutania kuhudumu katika Mahali Patakatifu atayavaa kwa siku saba.

3129:31 Law 7:37; 2Nya 13:9; Law 10:14; Hes 19:9; Eze 42:13“Chukua nyama ya huyo kondoo dume wa kuwaweka wakfu uipike katika Mahali Patakatifu. 3229:32 Mt 12:4Aroni na wanawe wataila ile nyama ya huyo kondoo dume pamoja na ile mikate iliyo kwenye hicho kikapu wakiwa hapo ingilio la Hema la Kukutania. 3329:33 Law 22:10-13Watakula sadaka hizi ambazo upatanisho ulifanywa kwazo kwa ajili ya kuwaweka wakfu na kuwatakasa. Lakini hakuna mtu mwingine yeyote anayeruhusiwa kuvila, kwa sababu ni vitakatifu. 3429:34 Kut 12; 10Ikiwa nyama yoyote ya huyo kondoo dume iliyotumika kwa kuwaweka wakfu au mkate wowote umebaki mpaka asubuhi, vichomwe. Kamwe visiliwe, kwa sababu ni vitakatifu.

3529:35 Law 8:33“Hivyo utamfanyia Aroni na wanawe kila kitu kama vile nilivyokuamuru: Utachukua muda wa siku saba kuwaweka wakfu. 3629:36 Ebr 10:11; Kut 30:10; Law 1:4; 4:20; 16:16; Hes 6:11; 8:12-19; 16:46; 23:25; 2Nya 29:24; Hes 7:10; Kut 40:10Utatoa dhabihu ya fahali kila siku kuwa sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho. Takasa madhabahu kwa kufanya upatanisho kwa ajili yake, nayo uitie mafuta na kuiweka wakfu. 3729:37 Kut 30:28-29; 40:10; Eze 43:25; Mt 23:19Kwa muda wa siku saba fanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu na kuiweka wakfu. Ndipo madhabahu itakuwa takatifu sana na chochote kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu.

3829:38 Law 23:2; Hes 28:3-8; 1Nya 16:40; 2Nya 8:13; Eze 46:13-15; Dan 12:11“Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja. 3929:39 Hes 28:4; 1Fal 18:36; 2Nya 13:11; Ezr 3:3; Za 141:2; Dan 9:21Utamtoa mmoja asubuhi na huyo mwingine jioni. 4029:40 Kut 30:24; Hes 15:4; 28:5; Mwa 35:14; Law 23:37; 2Fal 16:13Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja29:40 Efa moja ni sawa na kilo 22. ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini29:40 Robo ya hini ni sawa na lita moja. ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji. 4129:41 1Fal 18:29, 36; 2Fal 3:20; 16:15; Ezr 9:4-5; Za 141:2; Dan 9:21; Law 2:1; 5:3; 10:12; Hes 4:16; 6:17; 1Fal 8:64; Isa 43:23Huyo mwana-kondoo mwingine mtoe dhabihu wakati wa machweo pamoja na sadaka za unga na za kinywaji kama vile ulivyofanya asubuhi, kuwa harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

4229:42 Kut 30:8, 10, 21, 31; 31:13; Eze 46:15; Kut 26:1; 27:21; 25:22; 33:9, 11; Hes 7:89“Kwa vizazi vijavyo itakuwa kawaida kutoa sadaka hii ya kuteketezwa kila mara kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za Bwana. Hapo ndipo nitakapokutana na ninyi na kusema nanyi, 4329:43 Kut 33:18; 40:34; Law 9:6; 1Fal 8:11; 2Nya 5:14; 7:2; Za 26:8; 85:9; Eze 1:28; 43:5; Hag 1:8; 2:7Huko ndipo nitakapokutana na Waisraeli, nalo Hema la Kukutania litatakaswa na utukufu wangu.

4429:44 Law 21:15“Kwa hiyo nitaliweka wakfu Hema la Kukutania pamoja na madhabahu, nami nitamweka wakfu Aroni na wanawe ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani. 4529:45 Kut 25:8; Hes 35:34; Yn 14:17; Rum 8:10; Mwa 17:7; 2Kor 6:16; Ufu 21:3Ndipo nitakapofanya makao miongoni mwa Waisraeli na kuwa Mungu wao. 4629:46 Kut 6:6; 19:4-6; Kum 5:6; Za 114:1; Hag 2:5; Mwa 17:7; Kut 20:2Nao watajua kuwa Mimi Ndimi Bwana Mungu wao, aliyewatoa Misri ili nipate kufanya makao miongoni mwao. Mimi Ndimi Bwana Mungu wao.