Kutoka 24 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 24:1-18

Agano Lathibitishwa

124:1 Kut 19:24; 6:23; Hes 11:16; Law 10:1-2Kisha Mungu akamwambia Mose, “Njooni huku juu kwa Bwana, wewe na Aroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli. Mniabudu kwa mbali, 224:2 Hes 12:6-8lakini Mose peke yake ndiye atakayemkaribia Bwana; wengine wasije karibu. Nao watu wasije wakapanda pamoja naye.”

324:3 Kut 21:1; Gal 3:19; Kut 19:8; Yos 24:24; Kum 5:27Mose alipokwenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za Bwana, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema Bwana tutakifanya.” 424:4 Kut 17:14; Mwa 8:20; 28:18; Kum 31:9; 27:2Ndipo Mose akaandika kila kitu Bwana alichokuwa amesema.

Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli. 524:5 Law 1:3; Mwa 31:54Kisha akawatuma vijana wanaume wa Kiisraeli, nao wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu za mafahali wachanga kuwa sadaka za amani kwa Bwana. 624:6 Kut 14:15; 32:31; Za 99:6; Ebr 9:18; Law 1:11; 3:2, 8; 5:9; Mt 26:28Mose akachukua nusu ya damu ya wale wanyama na kuiweka kwenye mabakuli na nusu nyingine akainyunyiza juu ya madhabahu. 724:7 2Fal 23:2, 21; Ebr 9:19; Kut 19:8; Yer 40:3; 42:6, 21; 43:2Kisha akachukua kile Kitabu cha Agano na kuwasomea watu. Nao wakajibu, “Tutafanya kila kitu alichosema Bwana, nasi tutatii.”

824:8 Ebr 9:19; 1Pet 1:2; Law 26:3; Kum 5:2-3; Yos 24:25; 2Fal 11:17; Yer 11:4-8; 31:32; 34:13; Zek 9:11; Mt 26:28; Lk 22:20; Ebr 9:20Ndipo Mose akachukua ile damu, akawanyunyizia wale watu, akasema, “Hii ni damu ya agano ambalo Bwana amelifanya nanyi kufuatana na maneno haya yote.”

9Mose na Aroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli wakapanda mlimani, 1024:10 Mwa 16:13; Hes 12:6; Isa 6:1; Eze 8:3; 40:2; Yn 1:18; Ay 28:16; Isa 54:11; Ufu 4:3nao wakamwona Mungu wa Israeli. Chini ya miguu yake kulikuwa na kitu kama sakafu ya mawe ya yakuti samawi, iliyo safi kama anga angavu. 1124:11 Kut 3:6; 19:2; Eze 44:3; Mt 26:29; Mwa 32:30Lakini Mungu hakuinua mkono wake dhidi ya hawa viongozi wa Waisraeli; walimwona Mungu, nao wakala na kunywa.

1224:12 Kut 31:18; 32:15-16; 34:1, 28, 29; Kum 4:13; 5:22; 8:3; 9:9-11; 2Kor 3:12Bwana akamwambia Mose, “Panda uje kwangu huku mlimani na ukae hapa, nami nitakupa vibao vya mawe, vyenye sheria na amri ambazo nimeziandika ziwe mwongozo wao.”

1324:13 Kut 17:9; 3:1Basi Mose akaondoka na Yoshua mtumishi wake, naye Mose akapanda juu kwenye mlima wa Mungu. 1424:14 Kut 17:10; 18:16Mose akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Aroni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na neno aweza kuwaendea wao.”

1524:15 Kut 19:9; Mt 17:5Mose alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, 1624:16 Kut 16:7; Law 9:23; Hes 14:10; 1Sam 4:21-22; Eze 8:4; 11:22; Kut 19:11; Za 99:7nao utukufu wa Bwana ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba Bwana akamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu. 1724:17 Kut 15:7; 19:18; Ebr 12:18, 29Kwa Waisraeli utukufu wa Bwana ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima. 1824:18 1Fal 19:8; Mwa 7:4; Mt 4:2; Kut 34:28; Kum 9:9Kisha Mose akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, usiku na mchana.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

出埃及记 24:1-18

在西奈山立约

1耶和华又指示摩西说:“你和亚伦拿答亚比户以色列的七十位长老上我这里来,远远地敬拜我。 2只有你可以靠近我,其他百姓都不得与你一同走近。”

3摩西下山把耶和华的话和法令都告诉百姓,百姓齐声回答:“我们愿意遵行耶和华的一切吩咐。” 4摩西把耶和华的这些话记录下来。他清早起来,在山脚筑了一座坛,立了十二根柱子,代表以色列的十二支派。 5他又吩咐以色列的青年去给耶和华献燔祭,又献上公牛作平安祭。 6摩西把祭牲的血一半放在盆里,一半洒在坛上。 7他又把约书念给百姓听,百姓听了都说:“我们愿意遵行耶和华的一切吩咐,我们愿意顺服。” 8摩西便把盆中的血洒在百姓身上,说:“这是立约的血,是耶和华按所说的话与你们立约的凭据。”

9之后,摩西亚伦拿答亚比户以色列的七十位长老便上了山。 10他们都看见了以色列的上帝,祂的脚下好像是一片蓝宝石,像天一样明净。 11上帝没有伸手杀这些以色列的首领,允许他们看见祂,在祂面前吃喝。

12耶和华对摩西说:“你上山到我这里来,留在这里,我要把写着律法和诫命的石版赐给你,你可以用来教导百姓。” 13于是,摩西带着他的助手约书亚动身上了上帝的山。 14离开之前,摩西吩咐长老说:“你们在这里等候我们回来。亚伦户珥跟你们在一起,民中有什么诉讼的事情,可以去找他们。”

15摩西上了山,密云遮盖着整座山。 16耶和华的荣耀停留在西奈山上,密云遮盖了山六天。第七天,耶和华在云中召唤摩西17以色列人眼中,耶和华的荣耀在山上好像烈火。 18摩西上到山上,走进云中,在那里停留了四十昼夜。