Kutoka 22 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 22:1-31

Ulinzi Wa Mali

122:1 Law 6:1-7; 2Sam 12:6; Mit 6:31; Lk 19:8“Kama mtu akiiba maksai au kondoo na kumchinja au kumuuza, ni lazima alipe ngʼombe watano badala ya maksai mmoja na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja.

222:2 Ay 24:16; Yer 2:34; Hos 7:1; Mt 6:19-20; 24:43; Hes 35:27; Kut 20:15; Law 19:11; Kum 5:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Efe 4:28; 1Pet 4:15“Kama mwizi akishikwa anavunja nyumba akapigwa hata akafa, aliyemuua hana hatia ya kumwaga damu; 322:3 Kut 21:2; Mt 18:25lakini jambo hilo likitokea wakati jua limechomoza, huyo mtu atakuwa na hatia ya kumwaga damu.

“Mwizi huyo sharti alipe, lakini kama hana kitu, lazima auzwe ili alipe kwa ajili ya wizi wake.

422:4 1Sam 12:5; Mwa 43:12; Kut 21:16; Mit 6:31“Kama mnyama aliyeibwa akikutwa hai mikononi mwake, ikiwa ni maksai au punda au kondoo, lazima alipe mara mbili.

5“Kama mtu akichunga mifugo yake katika shamba au shamba la mizabibu, na akawaachia wajilishe katika shamba la mtu mwingine, ni lazima alipe vitu bora kutoka kwenye shamba lake mwenyewe au kutoka shamba lake la mizabibu.

622:6 Amu 15:5“Kama moto ukiwaka na kuenea kwenye vichaka vya miiba na kuteketeza miganda ya nafaka au nafaka ambayo haijavunwa, au kuteketeza shamba lote, mtu yule aliyewasha moto lazima alipe.

722:7 Law 6:2; Mwa 43:12“Kama mtu akimpa jirani yake fedha au mali nyingine amtunzie, na kama vikiibwa kutoka nyumba ya huyo jirani, kama mwizi atashikwa, lazima alipe mara mbili. 822:8 Kut 21:6; Kum 17:8-9Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atafika mbele ya waamuzi ili kuthibitisha kuwa hakuchukua mali ya mwenzake. 922:9 Kum 25:1Pakiwepo jambo lolote la mali isiyo halali, ikiwa ni maksai, punda, kondoo, mavazi, ama mali yoyote iliyopotea ambayo fulani atasema, ‘Hii ni mali yangu,’ pande zote mbili wataleta mashauri yao mbele ya waamuzi. Yule ambaye waamuzi watamwona kuwa na hatia atamlipa jirani yake mara mbili.

10“Kama mtu akimpa jirani yake punda, ngʼombe, kondoo au mnyama mwingine yeyote amtunzie, akifa au akijeruhiwa au akichukuliwa wakati haonekani na mtu yeyote, 1122:11 Law 6:3; 1Fal 8:31; 2Nya 6:22; Ebr 6:16jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa kiapo mbele za Bwana, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika. 12Lakini kama mnyama aliibwa kwa jirani, itampasa amlipe mwenye mnyama. 1322:13 Mwa 31:39Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa kulipa mnyama aliyeraruliwa.

14“Kama mtu akimwazima mnyama kutoka kwa jirani yake, na kama akiumia au akafa na mwenye mnyama hayupo, lazima amlipe huyo mnyama. 1522:15 Law 19:13; Ay 17:5Lakini mwenye mnyama akiwa angalipo na mnyama wake, mwazimaji hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara.

Uwajibikaji Wa Kijamii

1622:16 Kum 22:28; Mwa 34:12“Kama mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa na akilala naye, lazima alipe mahari, kisha atamwoa msichana huyo. 17Baba wa msichana akikataa katakata kumpa huyo mtu huyo msichana wake, bado ni lazima huyo mtu atalipa mahari kama inavyostahili malipo ya ubikira.

1822:18 Kut 7:11; Law 19:26, 31; 20:27; Kum 18:17; 1Sam 28:3; 2Nya 33:6; Isa 57:3“Usiruhusu mwanamke mchawi aishi.

1922:19 Law 18:23; 20:15; Kum 27:21“Mtu yeyote aziniye na mnyama lazima auawe.

2022:20 Kut 20:23; 22:21“Mtu awaye yote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwa Bwana, lazima aangamizwe.

21“Usimtendee mgeni vibaya au kumwonea, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.

2222:22 Kum 10:18; 24:6, 10-17; Ay 22:6-9; 24:3; 21; Za 68:5; 146:9; Mit 23:10; Isa 1:17; Yer 7:5-6; 21:12; 22:3; Eze 18:5-12; Zek 7:9-10; Mal 3:5; Yak 1:27“Usimdhulumu mjane wala yatima. 2322:23 Lk 18:7; Kum 10:18; 15:9; 24:15; Ay 34:28; 35:9; Za 10:14-17; 12:5; 18:6; Yak 5:4Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao. 2422:24 Za 10:9; 69:24; Mao 5:3Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima.

2522:25 Law 25:35-37; Kum 15:7-11; 23:20; Neh 5:7-10; Za 15:5; Eze 18:8“Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba. 2622:26 Mit 20:16; Eze 33:15; Amo 2:8Kama ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama, 2722:27 Kum 24:13, 17; Ay 22:6; 24:7; 29:11; 31:19-20; Eze 18:12, 16; Kut 34:6; Kum 4:31; 2Nya 30:9; Neh 9:17; Za 99:8; 103:8; 116:5; 145:8; Yoe 2:13; Yon 4:2kwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilo nalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma.

2822:28 Kut 20:7; 2Sam 16:5, 9; 1Sam 19:21; 1Fal 21:10; 2Fal 2:23; Za 102; 8; Mhu 10:20; Mdo 23:5“Usimkufuru Mungu au kumlaani mtawala wa watu wako.

2922:29 Kut 23:15-19; 34:20-26; Law 19:24; 23:10; Hes 18:13; 28:26; Kum 18:4; 26:2, 10; 1Sam 6:3; Neh 10:35; Mit 3:9; Mal 3:10; Kut 13:2; Hes 8:16-17; Lk 2:23“Usiache kutoa sadaka kutoka ghala lako au mapipa yako.

“Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako. 3022:30 Kut 34:19; Kum 15:19; Law 12:3; 22:27; Mwa 17:12Ufanye vivyo hivyo kwa ngʼombe wako na kwa kondoo wako. Waache wakae na mama zao kwa siku saba, lakini siku ya nane unipe.

3122:31 Kut 19:6; Law 19:2; 22:31; Ezr 9:2; Law 7:24; 17:15; 22:8; Kum 14:21; Eze 4:14; 44:31“Ninyi mtakuwa watu wangu watakatifu. Kwa hiyo msile nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori; mtupieni mbwa.