Kutoka 21 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 21:1-36

Watumishi Wa Kiebrania

(Kumbukumbu 15:12-18)

121:1 Kut 24:3; 34:32; Kum 4:14; 6:1“Hizi ndizo sheria utakazoweka mbele ya Waisraeli:

221:2 Kut 22:3; Yer 34:8, 14; Law 25:39; Kum 15:12“Kama ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia kwa miaka sita. Lakini katika mwaka wa saba, atakuwa huru naye atakwenda zake pasipo kulipa chochote. 3Kama akija peke yake, atakwenda huru peke yake, lakini kama akija na mke, ataondoka pamoja naye. 421:4 Law 25:44Kama bwana wake alimpatia mke naye akamzalia wana au binti, mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wake na huyo mwanaume ataondoka peke yake.

521:5 Kum 15:16“Lakini kama mtumishi akisema, ‘Ninampenda bwana wangu, mke wangu pamoja na watoto na sitaki kuwa huru,’ 621:6 Kut 22:8-9; Kum 17:9; 19:17; 21:5; Za 40:6; Ay 39:9; 41:4ndipo bwana wake atakapolazimika kumpeleka mbele ya waamuzi. Kisha atampeleka kwenye mlango au kizingiti na kutoboa sikio lake kwa shazia. Naye atamtumikia bwana wake maisha yake yote.

721:7 Neh 5:5“Kama mtu akimuuza binti yake kuwa mtumwa, hataachwa huru kama watumwa wa kiume waachiwavyo. 8Kama hakumpendeza bwana wake aliyemchagua, huyo bwana atamwacha akombolewe. Hatakuwa na haki ya kumuuza kwa wageni, kwa sababu huyo bwana atakuwa amekosa uaminifu. 9Kama akimchagua aolewe na mwanawe, ni lazima ampe haki za kuwa binti yake. 1021:10 1Kor 7:3-5Ikiwa huyo mwana aliyeozwa mtumwa mwanamke ataoa mwanamke mwingine, ni lazima aendelee kumtosheleza huyo mke wa kwanza kwa chakula, mavazi na haki zote za ndoa. 11Iwapo hatamtosheleza kwa mambo hayo matatu, huyo mke wa kwanza ataondoka na kuwa huru bila malipo yoyote ya fedha.

Majeraha Ya Mwilini

1221:12 Mwa 4:14, 23; Kut 31:15; Law 20:9-10; 24:16; 27:29; Hes 1:51; 35:16, 30-31; Kum 13:5; 19:11; 22:22; 27:16; Ay 31:11; Mit 20:20; Mt 26:52; Mwa 9:6“Yeyote ampigaye mtu na kumuua ni lazima auawe hakika. 1321:13 Hes 35:10-34; Kum 4:42; 19:2-13; Yos 20:9; 1Sam 24:4; 10:18; Yos 20:2Hata hivyo, kama hakumuua kwa makusudi, lakini Mungu akaruhusu itendeke, basi atakimbilia mahali nitakapomchagulia. 1421:14 Mwa 4:8; Hes 35:20; 2Sam 3:27; 20:10; Ebr 10:26; Kum 19:11-12; 1Fal 2:28-34Lakini kama mtu akipanga na kumuua mwingine kwa makusudi, mwondoe katika madhabahu yangu na kumuua.

15“Yeyote amshambuliaye baba yake au mama yake ni lazima auawe.

1621:16 Mwa 37:28; Kut 22:4; Kum 24:7“Yeyote amtekaye nyara mwingine akamuuza au akamweka kwake, akikamatwa ni lazima auawe.

1721:17 Kum 5:16; Mt 15:4; Mk 7:10; Law 20:9; Mit 20:20“Yeyote atakayemlaani baba yake au mama yake ni lazima auawe.

18“Kama watu wakigombana na mmoja akimpiga mwingine kwa jiwe au kwa ngumi yake na hakufa bali akaugua na kulala kitandani, 1921:19 2Sam 3:29yule aliyempiga ngumi hatahesabiwa kuwa na hatia kama mwenzake ataamka na kujikongoja kwa fimbo yake, lakini hata hivyo, ni lazima amlipe fidia ya muda wake aliopoteza na awajibike mpaka apone kabisa.

2021:20 Law 25:43; Efe 6:9“Kama mtu akimpiga mtumwa wake wa kiume au wa kike kwa fimbo na mtumwa huyo akafa papo hapo, ni lazima aadhibiwe 2121:21 Law 25:44-46lakini ikiwa mtumwa ataamka baada ya siku moja au mbili, hataadhibiwa, kwa sababu yule mtumwa ni mali yake.

2221:22 Kum 22:18, 19“Ikiwa watu wawili wanapigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua. 2321:23 Law 24:19; Kum 19:21Lakini kukiwa na jeraha kubwa, ni lazima ulipe uhai kwa uhai, 2421:24 Kut 21:23; Mt 5:38; Kum 19:21; Mt 5:38; 7:2; Law 24:20jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, 25kuchomwa moto kwa kuchomwa moto, jeraha kwa jeraha, mchubuko kwa mchubuko.

2621:26 Kol 4:1“Ikiwa mtu atampiga mtumwa mwanaume au mwanamke kwenye jicho na kuliharibu, ni lazima amwache huru yule mtumwa kama fidia ya hilo jicho. 27Kama akimvunja jino mtumwa wa kiume au wa kike, ni lazima amwache huru huyo mtumwa kwa kufidia hilo jino.

2821:28 Mwa 9:5“Kama fahali akimuua mwanaume au mwanamke kwa kumpiga kwa pembe, fahali huyo ni lazima auawe kwa kupigwa mawe, na nyama yake haitaliwa. Lakini mwenye fahali huyo hatawajibika. 29Lakini hata hivyo, ikiwa huyo fahali amekuwa na tabia ya kupiga kwa pembe, na mwenyewe ameonywa na hakutaka kumfungia naye akamuua mwanaume au mwanamke, huyo fahali ni lazima auawe kwa mawe na mwenye fahali pia auawe. 3021:30 Hes 35:21Lakini ikiwa malipo yatatakiwa kwake, basi anaweza kulipa kinachodaiwa ili kuukomboa uhai wake. 31Sheria hii pia itatumika ikiwa fahali atampiga kwa pembe mwana au binti. 3221:32 Mwa 37:28; Mt 26:15; 27:3, 9; Zek 11:12, 13; Flp 2:7Ikiwa fahali atampiga mtumwa wa kike au wa kiume, mwenye fahali atalipa shekeli thelathini21:32 Shekeli 30 ni sawa na gramu 300. za fedha kwa bwana mwenye mtumwa, na fahali ni lazima auawe kwa mawe.

3321:33 Lk 14:5“Kama mtu akiacha shimo wazi, ama akachimba shimo kisha asilifukie, na ngʼombe au punda akatumbukia ndani yake, 34mwenye shimo ni lazima alipe hasara iliyotokea; ni lazima amlipe mwenye mnyama. Mnyama aliyekufa atakuwa wake.

35“Kama fahali wa mtu fulani atamuumiza fahali wa mtu mwingine na akafa, watamuuza yule aliye hai na wagawane sawa fedha pamoja na mnyama aliyekufa. 36Hata hivyo, kama ikifahamika kwamba fahali huyo alikuwa na tabia ya kupiga kwa pembe na mwenyewe hakumfunga, ni lazima mwenye fahali alipe mnyama kwa mnyama, na mnyama aliyekufa atakuwa wake.