Kutoka 17 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 17:1-16

Maji Kutoka Kwenye Mwamba

(Hesabu 20:1-13)

117:1 Kut 16:1; 19:2; Hes 3:15; 20:5; 33:14Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama Bwana alivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa. 217:2 Hes 20:2; 33:14; Za 107:5; Kut 14:12; Kum 6:16; Za 78:18, 41; 106:14; Mt 4:7; 1Kor 10:9Kwa hiyo wakagombana na Mose wakisema, “Tupe maji ya kunywa.”

Mose akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribu Bwana?”

317:3 Kut 15:22-24; 14:11; 16:2-3Lakini watu walikuwa na kiu huko, wakanungʼunika dhidi ya Mose, wakisema, “Kwa nini ulitutoa kule Misri, ukatuleta hapa utuue kwa kiu sisi, watoto wetu na mifugo yetu?”

417:4 Hes 14:10; Isa 30:6; Yn 8:59Kisha Mose akamlilia Bwana, akasema, “Niwafanyie nini watu hawa? Sasa wanakaribia kunipiga kwa mawe.”

517:5 Kut 4:2; 10:12-13; 7:20Bwana akamjibu Mose, “Pita mbele ya watu. Wachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa Israeli, ichukue mkononi mwako ile fimbo uliyopiga nayo Mto Naili, nawe uende. 617:6 Hes 20:8-11; Kum 8:15; Amu 15:19; 2Fal 3:20; Neh 9:15; Za 74:15; 78:15-16; 105:41; 107:35; 114:8; Isa 30:25; 35:6; 43:19; 48:21; 1Kor 10:4Huko nitasimama mbele yako karibu na mwamba wa Horebu. Uupige mwamba na maji yatatoka ndani yake kwa ajili ya watu kunywa.” Kwa hiyo Mose akafanya haya mbele ya wazee wa Israeli. 717:7 Kum 6:16; 9:22; 33:8; Za 95:8; Hes 20:13, 24; 27:14; Za 81:7; 106:32Naye akapaita mahali pale Masa,17:7 Masa maana yake ni Kujaribu. na Meriba17:7 Meriba maana yake ni Kugombana. kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu Bwana wakisema, “Je, Bwana yu pamoja nasi au la?”

Vita Na Waamaleki

817:8 Mwa 36:12; Kum 25:17-19Waamaleki wakaja na kuwashambulia Waisraeli huko Refidimu. 917:9 Kut 24:13; 32:17; 33:11; Hes 11:28; 27:22; Kum 1:38; Mdo 7:45; Kut 4:17Mose akamwambia Yoshua, “Chagua baadhi ya watu wetu na uende kupigana na Waamaleki. Kesho nitasimama juu ya kilima nikiwa na fimbo ya Mungu mkononi mwangu.”

1017:10 Kut 24:14; 31:2Kwa hiyo Yoshua akapigana na Waamaleki kama Mose alivyomwagiza, nao Mose, Aroni na Huri wakapanda juu ya kilima. 1117:11 Yak 5:16Ikawa wakati wote Mose alipokuwa amenyanyua mikono yake, Waisraeli walikuwa wakishinda, lakini kila aliposhusha mikono yake Waamaleki walishinda. 1217:12 Yos 8:26Mikono ya Mose ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Aroni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Mose, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki thabiti mpaka jua lilipozama. 13Kwa hiyo Yoshua akalishinda jeshi la Waamaleki kwa upanga.

1417:14 Kut 24:4; 34:27; 33:2; Kum 31:9; Ay 19:23; Isa 30:8; Yer 36:2; 45:1; 51:60; Kut 32:33; Kum 29:20; Ay 18:17; Za 9:5; 34:15; 109:15; Eze 18:4; Mwa 36:12; Hes 24:7; Amu 3:13; Isa 30:17-18; Za 83:7Kisha Bwana akamwambia Mose, “Andika mambo haya katika kitabu ili yakumbukwe, na uhakikishe kwamba Yoshua amesikia, kwa sababu nitafuta kabisa kumbukumbu la Amaleki chini ya mbingu.”

1517:15 Mwa 8:20; 22:14Mose akajenga madhabahu na kuiita Yehova Nisi.17:15 Yehova Nisi maana yake ni Bwana ni Bendera yangu. 1617:16 Hes 24:7; 1Sam 15:8, 32; 1Nya 4:43; Es 3:1; 8:3; 9:5, 24Mose akasema, “Kwa maana mikono iliinuliwa mpaka kwenye kiti cha enzi cha Bwana. Bwana atakuwa na vita dhidi ya Waamaleki kutoka kizazi hata kizazi.”