Kutoka 16 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 16:1-36

Mana Na Kware

116:1 Kut 17:1; Hes 33:11-12; Kut 6:6; 12:1-2Jumuiya yote ya Kiisraeli ikaondoka Elimu, wakafika Jangwa la Sini, lililokuwa kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka Misri. 216:2 Kut 15:24; 14:11; 1Kor 10:10Huko jangwani hiyo jumuiya yote wakawanungʼunikia Mose na Aroni. 316:3 Kut 17:3; Hes 14:2; 20:3; 11:4, 34; Kum 12:20; Za 78:18; 106:14; Yer 44:12; Mwa 47:15Waisraeli wakawaambia, “Laiti tungelikufa kwa mkono wa Bwana huko Misri! Huko tuliketi tukizunguka masufuria ya nyama na tukala vyakula tulivyovitaka, lakini ninyi mmetuleta huku jangwani ili mpate kuua mkutano huu wote kwa njaa.”

416:4 Dan 8:3; Neh 9:15; Za 78:24; 105:40; Yn 6:31; Mwa 22:1Kisha Bwana akamwambia Mose, “Nitanyesha mikate kutoka mbinguni kwa ajili yenu. Watu watatoka kila siku na kukusanya kitakachowatosha kwa siku ile, kwa njia hii, nitawajaribu nione kama watafuata maelekezo yangu. 516:5 Law 25:21Siku ya sita watatayarisha kile waletacho ndani, nacho kitakuwa mara mbili kuliko ya kile walichokusanya kila siku.”

616:6 Kut 6:6Kwa hiyo Mose na Aroni wakawaambia Waisraeli wote, “Jioni mtajua kwamba Bwana ndiye aliwatoa Misri, 716:7 Kut 24:16; 29:43; 33:18-22; 40:34; Law 9:6; Hes 16:19; Kum 5:24; 1Fal 8:11; Za 63:2; Isa 6:3; 35:2; 40:5; 44:23; 66:18; Eze 1:28; 10:4; 43:5; Hab 2:14; Hag 2:7; Yn 11:40; Hes 11:1; 17:5; 16:11kisha asubuhi mtauona utukufu wa Bwana, kwa sababu amesikia manungʼuniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani hata mtunungʼunikie?” 816:8 Hes 23:21; Kum 33:5; Amu 8:23; 1Sam 8:17; 12:12; Mt 10:40; Rum 13:2; 1The 4:8Pia Mose akasema, “Mtajua kuwa alikuwa Bwana wakati atakapowapa nyama mle ifikapo jioni na mikate yote mtakayohitaji asubuhi kwa sababu amesikia manungʼuniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani? Hamnungʼuniki dhidi yetu, bali dhidi ya Bwana.”

9Kisha Mose akamwambia Aroni, “Iambie jumuiya yote ya Waisraeli kwamba, ‘Mje mbele zake Bwana, kwa maana amesikia manungʼuniko yenu.’ ”

1016:10 Yn 11:2; Kut 13:21; 40:34-35; 1Fal 8:10; 2Nya 7:1; Eze 10:4Aroni alipokuwa akizungumza na jumuiya yote ya Waisraeli, wakatazama kuelekea jangwani, na huko wakaona utukufu wa Bwana ukitokeza katika wingu.

11Bwana akamwambia Mose, 1216:12 Kut 6:2; 16:7; 20:2“Nimesikia manungʼuniko ya Waisraeli. Waambie, ‘Jioni mtakula nyama, na asubuhi mtashiba mikate. Ndipo mtajua ya kwamba Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ ”

1316:13 Hes 11:31; Za 78:27-28; 105:40; 106:15; Hes 11:9Jioni ile kware wakaja wakaifunika kambi na asubuhi kulikuwa na tabaka la umande kuzunguka kambi. 1416:14 Hes 11:7-9; Kum 8:3, 16; Za 105:40Wakati umande ulipoondoka, vipande vidogo vidogo kama theluji vilionekana juu ya uso wa jangwa. 1516:15 Kum 8:16; Neh 9:20; Yn 6:31Waisraeli walipoona, wakaambiana, “Hiki ni nini?” Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani.

Mose akawaambia, “Huu ndio mkate ambao Bwana amewapa mle. 16Hivi ndivyo Bwana alivyoamuru: ‘Kila mmoja akusanye kiasi anachohitaji. Chukueni pishi16:16 Pishi ni kipimo cha ujazo, kwa Kiebrania ni omeri, ambacho ni sawa na kilo mbili. moja kwa kila mtu mliye naye katika hema yenu.’ ”

17Waisraeli wakafanya kama walivyoambiwa, baadhi yao wakakusanya zaidi, wengine pungufu. 1816:18 2Kor 8:15Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji.

1916:19 Kut 12:10; 23:18Kisha Mose akawaambia, “Mtu yeyote asibakize chochote mpaka asubuhi.”

2016:20 Kut 32:31Hata hivyo, wengine hawakuzingatia aliyosema Mose, wakahifadhi kiasi fulani mpaka asubuhi, lakini kile alichohifadhi kikajaa mabuu na kuanza kunuka. Kwa hiyo Mose akawakasirikia.

21Kila asubuhi, kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji na jua lilipokuwa kali, iliyeyuka. 2216:22 Kut 34:31Siku ya sita, wakakusanya mara mbili, kiasi cha pishi mbili kwa kila mtu, nao viongozi wa jumuiya wakaja kumwarifu Mose. 2316:23 Mwa 2:3; Kut 20:8; Kum 5:13-14Mose akawaambia, “Hivi ndivyo alivyoagiza Bwana: ‘Kesho itakuwa siku ya mapumziko, Sabato takatifu kwa Bwana. Kwa hiyo okeni kile mnachotaka kuoka na mchemshe kile mnachotaka kuchemsha. Hifadhini chochote kinachobaki na mkiweke mpaka asubuhi.’ ”

24Kwa hiyo wakavihifadhi mpaka asubuhi, kama Mose alivyoagiza, na havikunuka wala kuwa na mabuu. 25Mose akawaambia, “Kuleni leo, kwa sababu leo ni Sabato kwa Bwana. Hamtapata chochote juu ya nchi leo. 2616:26 Kut 20:9-10Kwa siku sita mtakusanya, lakini siku ya saba, yaani Sabato, hakutakuwepo chochote.”

27Hata hivyo, baadhi ya watu wakatoka kwenda kukusanya siku ya saba, lakini hawakupata chochote. 2816:28 Yos 9:14; Za 78:10; 106:13; 107:11; Yer 32:23; 2Fal 17:14Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Je, mtaacha kushika maagizo na maelekezo yangu mpaka lini? 29Fahamuni kuwa Bwana amewapa ninyi Sabato, ndiyo sababu katika siku ya sita amewapa mikate ya siku mbili. Kila mmoja inampasa kukaa pale alipo katika siku ya saba. Hata mmoja haruhusiwi kutoka.” 30Kwa hiyo watu wakapumzika siku ya saba.

31Watu wa Israeli wakaita ile mikate mana16:31 Mana maana yake ni mkate kutoka mbinguni. Ilikuwa myeupe kama mbegu za mtama na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotengenezwa kwa asali. 32Mose akasema, “Hivi ndivyo alivyoagiza Bwana: ‘Chukueni pishi ya mana na kuhifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo ili vione mikate niliyowapa mle jangwani nilipowatoa katika nchi ya Misri.’ ”

3316:33 Ebr 9:4; Ufu 2:17Kwa hiyo Mose akamwambia Aroni, “Chukua gudulia na uweke pishi moja ya mana ndani yake. Kisha uweke mbele za Bwana ili kihifadhiwe kwa ajili ya vizazi vijavyo.”

3416:34 Kut 25:16, 21-22; 27:21; 31:18; 40:20; Law 16:13; Hes 1:50; 7:89; 10:11; 17:4; Kum 2:10; 1Fal 8:9; 2Nya 5:10Kama Bwana alivyomwagiza Mose, hatimaye Aroni alikuja kuihifadhi ndani ya Sanduku la Ushuhuda. 3516:35 Yn 6:31, 49; Hes 14:33; 33:38; Kum 1:3; 2:7; 8:2-4; Yos 5:6; Amu 3:11; Neh 9:21; Za 95:10; Amu 5:25; Yos 5:12Waisraeli wakala mana kwa miaka arobaini, mpaka walipofika katika nchi iliyokaliwa na watu; walikula mana hadi walipofika mpakani mwa Kanaani.

3616:36 Law 5:11; 6:20; Hes 5:15; 15:4; 28:5(Pishi moja ni sehemu ya kumi ya kipimo cha efa.16:36 Efa moja ni sawa na kilo 22.)