Kutoka 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 13:1-22

Kuwekwa Wakfu Kwa Wazaliwa Wa Kwanza

1Bwana akamwambia Mose, 213:2 Kut 22:29; 34:20; Law 27:26; Hes 3:13; 8:17; 18:15; Kum 15:19; Neh 10:34; Lk 2:23“Niwekeeni wakfu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume. Kila mtoto wa kwanza aliye kifungua tumbo miongoni mwa Waisraeli ni mali yangu, akiwa wa mwanadamu au wa mnyama.”

313:3 Kut 7:4; Law 26:13; Hes 22:5; 26:4; Kum 4:45; 5:6; Za 81:10; 114:1; Kut 3:20; 12:8Ndipo Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu Bwana aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu. 413:4 Kut 12:2Leo, katika mwezi wa Abibu,13:4 Abibu ni jina la mwezi wa kwanza kwa Wayahudi, ambao ni mwezi wa nne katika kalenda yetu. mnatoka. 513:5 Kut 3:8; 12:25-26Bwana atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi itiririkayo maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu: 613:6 Kut 12:15-20Kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu na katika siku ya saba utamfanyia Bwana sikukuu. 7Kwa muda wa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu, pasionekane kitu chochote kilicho na chachu miongoni mwako, wala chachu yoyote isionekane popote ndani ya mipaka yako. 813:8 Kut 10:2; Za 78:5-6Siku ile utamwambia mwanao, ‘Nafanya hivi kwa sababu ya jambo ambalo Bwana alinitendea nilipotoka katika nchi ya Misri.’ 913:9 Isa 44:5; Kum 6:8; 11:18; Mit 3:3; Mt 23:5; Kut 3:20Adhimisho hili, litakuwa kama alama kwenye mkono wako na ukumbusho katika paji lako la uso, kwamba sheria ya Bwana inapaswa iwe kinywani mwako. Kwa kuwa Bwana alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu. 1013:10 Kut 12:14; Za 75:2; 102:13Ni lazima uishike amri hii kwa wakati uliopangwa mwaka baada ya mwaka.

1113:11 Mwa 22:16; Kum 1:8; Mwa 12:7; 17:19; Za 105:42-45“Baada ya Bwana kukuingiza katika nchi ya Wakanaani na kukupa nchi hiyo, kama alivyokuahidi kwa kiapo na kwa baba zako, 1213:12 Mwa 4:4; Law 27:26; Hes 3:13; 18:15-17; Lk 2:23inakupasa kumtolea Bwana mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya Bwana. 1313:13 Law 27:11; Kut 34:20; Isa 66:3; Hes 3:46-47; 18:15Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo, lakini kama hukumkomboa, utamvunja shingo yake. Kila mzaliwa wa kwanza mwanaume miongoni mwa wana wenu utamkomboa.

1413:14 Kut 10:2; 20:2; Kum 7:8; 6:20; 28:68“Katika siku zijazo, mwanao akikuuliza, ‘Hii ina maana gani?’ Mwambie, ‘Kwa mkono wenye nguvu Bwana alitutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. 15Farao alipokataa kwa ukaidi kuturuhusu kuondoka, Bwana aliua kila mzaliwa wa kwanza wa Wamisri, mwanadamu na wa mnyama. Hii ndiyo sababu ninatoa dhabihu kwa Bwana mzaliwa wa kwanza wa kiume, wa kila tumbo na kumkomboa kila mzaliwa wa kwanza wa wana wangu.’ 16Jambo hili litakuwa kama ishara kwenye mkono wako na kama alama kwenye paji la uso wako, kwamba Bwana alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu.”

Nguzo Ya Wingu Na Moto

1713:17 Kut 14:11; Hes 14:1-4; Kum 17:16; Hos 11:5Farao alipowaachia watu waende, Mungu hakuwaongoza kufuata njia ipitiayo katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa fupi zaidi. Kwa maana Mungu alisema, “Wakikabiliana na vita, wanaweza kubadili mawazo yao na kurudi Misri.” 1813:18 Kut 15:22; Za 136:16; Eze 20:10; Yos 4:13Kwa hiyo Mungu akawaongoza watu kupitia njia ya kuzunguka kupitia jangwani, kuelekea Bahari ya Shamu. Waisraeli walipanda kutoka nchi ya Misri wakiwa wamejiandaa kwa vita.

1913:19 Yos 24:32; Mdo 7:16; Ebr 11:22; Mwa 47:29-30Mose akachukua mifupa ya Yosefu kwa sababu Yosefu alikuwa amewaapisha wana wa Israeli. Alikuwa amewaambia, “Hakika Mungu atakuja kuwasaidia, nanyi ni lazima mwiichukue mifupa yangu mwende nayo kutoka mahali hapa.”

2013:20 Kut 12:37; Hes 33:6Baada ya Waisraeli kuondoka Sukothi wakapiga kambi huko Ethamu pembeni mwa jangwa. 2113:21 Kut 32:1; 33:14; Kum 2:7; 31:8; Amu 4:14; 5:4; Za 68:7; 72:20; Yer 2:2; Hab 3:13; Kut 14:19, 24; 24:16; 33:9-10; 34:5; 40:38; Hes 9:16; 12:5; 14:14; Kum 1:33; Neh 9:12, 19; Za 78:14; 99:7; 105:39; Isa 4:5; 1Kor 10:1Wakati wa mchana Bwana aliwatangulia kwa nguzo ya wingu kuwaongoza katika njia yao, na wakati wa usiku aliwatangulia kwa nguzo ya moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana au usiku. 2213:22 Neh 9:19; Hes 33:7; Yer 44:1; Eze 29:10Ile nguzo ya wingu wakati wa mchana au ile nguzo ya moto wakati wa usiku haikuondoka mahali pake mbele ya watu.