Kumbukumbu 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 4:1-49

Waamriwa Utii

14:1 Law 18:4-5; Kum 1:3; 30:15-20; Rum 10:5; Eze 20:11; Rum 10:5Sikia sasa, ee Israeli, amri na sheria nitakazokufundisha wewe. Zifuate ili upate kuishi na uingie kuimiliki nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zako anawapa. 24:2 Kum 12:32; Yos 1:7; Mit 30:6; Ufu 22:18-19; Yer 26:2; Law 22:31; Kum 10:12-13; Mhu 12:13Usiongeze wala usipunguze chochote ninachowaamuru ninyi, ila myashike maagizo ya Bwana Mungu wenu ambayo nawapa.

34:3 Hes 25:1-9; Za 106:28Mliona kwa macho yenu wenyewe kile Bwana alichokifanya kule Baal-Peori. Bwana Mungu wenu aliwaangamiza kutoka miongoni mwenu kila mmoja aliyemfuata Baali wa Peori, 4lakini ninyi nyote mlioshikamana na Bwana kwa uthabiti, Mungu wenu, mko hai mpaka leo.

54:5 Za 71:17; 119:102; Yer 32:33; Kut 18:20; Law 27:34; Ezr 9:11Tazama, nimewafundisha amri na sheria kama Bwana Mungu wangu alivyoniamuru mimi, ili mzifuate katika nchi mnayoiingia kuimiliki. 64:6 Kum 29:9; 1Fal 2:3; Kum 30:19-20; 32:46-47; Za 19:7; 119:98; Mit 1:7; 2:5; 2Tim 3:15; Ay 28:28; Za 111:10; Mit 3:7; 9:10; Mhu 12:13; Eze 5:5Zishikeni kwa uangalifu, kwa kuwa hii itaonyesha hekima na ufahamu wenu kwa mataifa, ambayo yatasikia kuhusu amri zote hizi, nao watasema, “Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na ufahamu.” 74:7 2Sam 7:23; Hes 23:21; Za 46:1; Mdo 17:27; Kut 25:8; 29:45; Law 26:12; 1Fal 6:13; Isa 55:6; Zek 2:10; Efe 2:17; Yak 4:8Ni taifa gani jingine lililo kubwa kiasi cha kuwa na miungu yao iliyo karibu nao kama Bwana Mungu wetu alivyo karibu nasi wakati wowote tunapomwomba? 84:8 Za 89:14; 97:2; 119:7, 62, 144, 160, 172; Rum 3:2Nalo ni taifa gani jingine lililo kubwa hivi lenye kuwa na amri na sheria za haki kama hizi ninazoweka mbele yenu leo?

94:9 Kut 23:13; Mwa 14:14; 18:19; Kum 6:20-25; Efe 6:4; Kut 10:2; Mit 4:23; Za 78:5-6; Mit 4:23; 23:19; 3:1, 3; 4:21; Mwa 18:19; Mit 22:6; Efe 6:4Mwe waangalifu, na makini ili msije mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa macho yenu, wala kuyaacha yaondoke moyoni mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.

104:10 Kut 3:1; 19:9, 16; Kum 14:23; 17:19; 31:12-13; Za 2:11; 111:10; 147:11; Isa 8:13; Yer 32:40; Kut 20:20; Kum 12:1Kumbuka siku uliyosimama mbele za Bwana Mungu wako kule Horebu, wakati aliponiambia, “Wakutanishe watu mbele yangu wasikie maneno yangu ili kwamba waweze kujifunza kuniheshimu kwa muda wote watakaoishi katika nchi, nao waweze kuwafundisha watoto wao maneno hayo.” 114:11 Kut 3:1; 19:17-18; 19:9; Za 18:11; 97:2; Ebr 12:18-19Mlisogea karibu na mkasimama chini ya mlima wakati ulipowaka moto mpaka mbinguni juu, pamoja na mawingu meusi na giza nene. 124:12 Kut 20:22; Mt 3:17; Kum 5:4-20; Ebr 12:19; Yn 5:37; Kut 19:9Ndipo Bwana alipozungumza nanyi kutoka moto. Mkasikia sauti ya maneno lakini hamkuona umbo, kulikuwa na sauti tu. 134:13 Kum 9:9-11; Rum 9:4; Kut 24:12; 31:18; 4:14; 21:1Aliwatangazia Agano lake na Amri Kumi, ambazo aliwaamuru mzifuate, kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe. 14Naye Bwana alinielekeza wakati huo kuwafundisha ninyi sheria na amri ambazo mnapaswa kuzifuata katika nchi ambayo mnavuka Yordani kuimiliki.

Kuabudu Sanamu Kwakatazwa

154:15 Isa 40:18; 41:22-24; Kut 3:1; Yos 23:11; Mal 2:15; Mit 4:23, 27; Yer 17:21; Mdo 17:24-29Hamkuona umbo la aina yoyote siku ambayo Bwana alizungumza nanyi kule Horebu kutoka kwenye moto. Kwa hiyo mjihadhari kwa uangalifu sana, 164:16 Mwa 6:11-12; Kum 9:12; 31:29; 32:5; Amu 2:19; Kut 20:4-5; 32:7; Rum 1:23ili msije mkajichafua na kujitengenezea sanamu au kinyago chenye umbo lolote kama la mwanaume au mwanamke, 174:17 Rum 1:23au kama mnyama aliye juu ya nchi au ndege yeyote arukaye angani, 18au kama kiumbe kitambaacho juu ya ardhi au samaki yeyote aliye ndani ya maji. 194:19 2Fal 23:11; Kum 17:3; Ay 31:26; Yer 8:2; 43:13; Eze 8:16; Mwa 1:16; 2:1; 37:9; Rum 1:25; Kum 13:5; Hes 25:3Na utazamapo juu angani na ukaliona jua, mwezi na nyota na vyote vinavyoipamba mbingu, usije ukashawishiwa kuviinamia na kuviabudu vile ambavyo Bwana Mungu wenu alivyogawia mataifa yote chini ya mbingu. 204:20 Kut 1:13; 3:10; Mwa 17:7; Kut 8:22; 34:9; Tit 2:14; Kut 19:5Lakini kwenu ninyi, Bwana amewatoa kutoka kwenye tanuru ya kuyeyushia chuma, katika Misri kuwa watu wa urithi wake kama mlivyo sasa.

214:21 Hes 20:12; Kum 1:37Bwana alinikasirikia kwa sababu yenu na akaapa kwamba sitavuka Yordani kuingia katika nchi nzuri Bwana Mungu wenu anayowapa kuwa urithi wenu. 224:22 Hes 27:13-14; Kum 3:25Nitakufa katika nchi hii; sitavuka Yordani, lakini ninyi ni karibu mvuke mkaimiliki ile nchi nzuri. 234:23 Kut 20:4Jihadharini msilisahau Agano la Bwana Mungu wenu lile alilofanya nanyi; msijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote ambacho Bwana Mungu wenu amewakataza. 244:24 Kut 15:7; 19:18; Ebr 12:29; Kut 20:5Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.

254:25 1Fal 11:6; 15:26; 16:25-30; 2Fal 17:2; 17:21Baada ya kuwa na watoto na wajukuu na kuishi katika nchi hiyo siku nyingi, tena kama mkijichafua na kutengeneza sanamu ya aina yoyote, mkifanya maovu machoni pa Bwana Mungu wenu na kumfanya awe na hasira, 264:26 Mwa 31:50; Mit 14:5; Kum 30:18-19; 31:28; 32:1; Za 50:4; Isa 1:2; 34:1; Yer 6:19; Mik 6:2; Kum 6:15; 7:4ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yenu siku hii kwamba mtaangamia mara moja kutoka nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki. Hamtaishi kule kwa muda mrefu bali kwa hakika mtaangamizwa. 274:27 Law 26:23; Kum 28:36-64; 29:28; 1Fal 8:46; 2Fal 17:16; Za 44:11; 106:27; Yer 3:8; Mik 1:16; Isa 17:6; 21:17; Oba 1:5; Neh 1:8Bwana atawatawanya miongoni mwa mataifa, na ni wachache wenu tu watakaosalia miongoni mwa mataifa hayo ambayo Bwana atawafukuzia. 284:28 Kum 13:2; 28:36-64; 1Sam 26:19; Yer 5:19; 16:13; Mdo 19:26; Kum 29:17; Za 115:4-8; 135:15-18; Isa 8:19; 26:14; 44:17-20; Ufu 9:20Huko mtaabudu miungu ya miti na mawe iliyotengenezwa na watu, ambayo haiwezi kuona au kusikia wala kula au kunusa. 294:29 1Sam 13:12; 2Fal 13:4; 2Nya 7:14; 15:4; 33:12; Za 78:34; 119:58; Isa 45:19, 22; 55:6; Yer 26:19; Dan 9:13; Hos 3:5; Amo 5:4; 1Sam 7:3; 1Fal 8:48; Yer 29:13; Kum 6:5; 30:1-3, 10Lakini kama mtamtafuta Bwana Mungu wenu, mtampata; kama mtamtafuta kwa moyo wenu wote na kwa roho yote. 304:30 Hos 3:5; Law 26:41; Kum 31:17-21; Za 4:1; 18:6; 48:1; 59:16; 107:6; Kum 31:29; Yer 23:20; 3:1-12, 22; 4:1; 18:11; Ebr 1:2; Kum 30:2; 1Fal 8:48; Neh 1:9; Yoe 2:12Wakati mnapokuwa katika dhiki, nayo mambo haya yote yamewatokea siku hizo, ndipo mtamrudia Bwana Mungu wenu na kumtii. 314:31 Kut 34:6; Neh 9:31; Za 111:9; Kum 31:6-8; Yoe 1:5; 1Fal 8:57; 1Nya 28:9-20; Za 9:10; 27:9; 71:9; Isa 42:16; Ebr 13:5; Law 26:44-45; Yon 4:2Kwa maana Bwana Mungu wenu ni Mungu mwenye huruma, hatawaacha au kuwaangamiza wala kusahau Agano alilofanya na baba zenu, alilowathibitishia kwa kiapo.

Bwana Ndiye Mungu

324:32 Kum 32:7; Mwa 1:27; Isa 45:12; Kum 28:64; 30:1; Yer 9:16; Mt 24:31; 2Sam 7:23; Ay 8:8Sasa uliza kuhusu siku za zamani, zamani kabla ya wakati wako, tangu siku ile Mungu alipomuumba mtu juu ya nchi, uliza kutoka mwisho mmoja wa mbingu mpaka mwisho mwingine wa mbingu. Je, kumepata kutokea jambo jingine lililo kubwa kama hili, au kuna jambo jingine kama hilo limepata kusikiwa? 334:33 Kut 20:22; Kum 5:24-26Je, kuna watu wengine wowote waliosikia sauti ya Mungu ikizungumza kwenye moto, kama mlivyosikia, nao wakaishi? 344:34 Kut 14:30; Isa 7:12; Kut 4:17; Kum 7:19; 26:8; 29:3; 1Nya 16:12; Za 9:1; 40:5; Yer 32:20; Kut 32:20; 3:20; Kum 5:15; 6:21; 15:15; Kut 15:1; Kum 34:12; Za 45:4; 65:5Je, kuna mungu yeyote amepata kujaribu mwenyewe kuchukua taifa moja kutoka taifa lingine, kwa mapigo, kwa ishara za miujiza na maajabu, kwa vita, kwa mkono wenye nguvu na mkono ulionyooshwa au kwa matendo makuu ya kutisha, kama yale ambayo Bwana Mungu wenu aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu?

354:35 Kum 4:39; 7:9; 32:4-12; Kut 8:10; 1Sam 2:2; 1Fal 8:60; 2Fal 19:19; Isa 3:10; Mk 12:32Mlionyeshwa mambo haya ili mpate kujua kuwa Bwana ndiye Mungu; hakuna mwingine ila yeye. 364:36 Kut 19:19; Kum 8:5; Kut 19:20; 18:22; 24:16; 1Nya 29:1; 2Nya 20:6; Ebr 12:18, 25Kutoka mbinguni amewasikizisha sauti yake ili kuwaadilisha. Hapa duniani aliwaonyesha moto wake mkubwa, nanyi mlisikia maneno yake kutoka kwenye ule moto. 374:37 Kum 7:8; 10:15; 23:5; 33:3; Za 44:3; Yer 31:3; Hos 11:1; Mal 1:2; 2:11; Kut 3:20; 13:3, 9-14Kwa sababu aliwapenda baba zenu na alichagua wazao wao baada yao, aliwatoa katika nchi ya Misri kwa Uwepo wake na kwa uwezo wake mkuu, 384:38 Hes 34:14-15; Kum 7:1; 9:5aliwafukuza mbele yenu mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi na kuwaleta ninyi katika nchi yao na akawapa ninyi kuwa urithi wenu, kama ilivyo leo.

394:39 Kum 8:10; Kut 15:11; Yos 2:11; Isa 42:8; Dan 4:35Kubalini na mweke moyoni leo kuwa Bwana ndiye Mungu mbinguni juu na duniani chini. Hakuna mwingine. 404:40 Law 22:31; Mwa 26:5; Kum 5:29; 11:1; Za 105:45; Isa 48:18; Kum 5:16; 12:25; Isa 3:10; Kut 23:26; Efe 6:2-3Mshike amri na maagizo yake ninayowapa leo, ili mpate kufanikiwa ninyi na watoto wenu baada yenu, na mpate kuishi maisha marefu katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu siku zote.

Miji Ya Makimbilio

414:41 Hes 35:6Kisha Mose akatenga miji mitatu mashariki ya Yordani, 424:42 Kut 21:13ambayo mtu yeyote aliyemuua mtu angeweza kukimbilia ikiwa amemuua jirani yake bila kukusudia na bila kuwa na chuki naye siku zilizopita. Angeweza kukimbilia katika mmojawapo ya miji hii na kuokoa maisha yake. 434:43 Yos 21:38; 1Fal 22:3; 2Fal 8:28; 9:14Miji hiyo ilikuwa: Bezeri katika tambarare ya jangwa kwa ajili ya Wareubeni; Ramothi katika nchi ya Gileadi kwa ajili ya Wagadi; nao mji wa Golani katika nchi ya Bashani kwa ajili ya Wamanase.

Utangulizi Wa Sheria

44Hii ndiyo sheria Mose aliyoweka mbele ya Waisraeli. 45Haya ndiyo masharti, amri na sheria Mose aliyowapa wana wa Israeli wakati walitoka Misri, 464:46 Hes 21:26; Kum 3:29nao walikuwa katika bonde karibu na Beth-Peori mashariki ya Yordani, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala Heshboni, naye alishindwa na Mose na Waisraeli walipokuja toka Misri. 474:47 Hes 21:25; Kum 3:3, 4Waliimiliki nchi yake na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, wafalme wawili Waamori waliotawala mashariki ya Yordani. 484:48 Kum 2:36; 3:8-9; Za 133:3Nchi hii ilienea kutoka Aroeri ukingoni mwa Bonde la Arnoni mpaka Mlima Sioni (yaani Hermoni), 49pamoja na eneo lote la Araba mashariki ya Yordani, na kuenea mpaka Bahari ya Araba kwenye miteremko ya Pisga.