Kumbukumbu 34 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 34:1-12

Kifo Cha Mose

134:1 Hes 32:3; 21:10; Kum 32:49, 52; Yos 19:40-48; Amu 18:28Kisha Mose akaupanda mlima Nebo kutoka tambarare za Moabu mpaka kilele cha Pisga, ngʼambo ya Yeriko. Huko Bwana akamwonyesha nchi yote: kutoka Gileadi mpaka Dani, 234:2 Kut 23:31; Kum 11:24; Hes 34:6; Yos 15:12Naftali yote, nchi ya Efraimu na Manase, nchi yote ya Yuda mpaka bahari ya magharibi,34:2 Yaani Bahari ya Mediterania. 334:3 Mwa 12:9; 13:10; Amu 1:16; 3:13; 2Nya 28:15Negebu na nchi yote kuanzia Bonde la Yeriko, Mji wa Mitende, hadi Soari. 434:4 Mwa 28:13; 12:7; Yos 21:43; Kum 3:23, 27Kisha Bwana akamwambia, “Hii ndiyo nchi niliyomwahidi Abrahamu na Isaki na Yakobo kwa kiapo niliposema, ‘Nitawapa wazao wako.’ Nimekuruhusu uione kwa macho yako, lakini hutavuka kuingia.”

534:5 Hos 12:7; Yos 1:1-2; Mwa 25:8Naye Mose mtumishi wa Bwana akafa huko Moabu, kama Bwana alivyokuwa amesema. 634:6 Kum 3:29; Yud 9Mungu akamzika huko Moabu, katika bonde mkabala na Beth-Peori, lakini hakuna ajuaye kaburi lake lilipo mpaka leo. 734:7 Kut 7:7; Yos 14:10; Mwa 27:1; 15:15; Kum 31:2Mose alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipofariki; hata hivyo nguvu ya macho yake haikufifia wala mwili wake haukudhoofika. 834:8 Hes 21:11; 20:29; Mwa 37:34; 50:3; 10; 50:3; 2Sam 11:27; 1Sam 25:1; Isa 57:1; Mdo 8:2Waisraeli wakaomboleza kwa ajili ya Mose kwenye tambarare za Moabu kwa siku thelathini, mpaka wakati wa kulia na kuomboleza ulipopita.

934:9 Mwa 41:38; Kut 28:3; 31:3; Isa 11:2; 1Fal 9:12; Kum 31:14; Mdo 6:6; Dan 6:3; Kum 27:18; Hes 11:17; 27:18Basi Yoshua mwana wa Nuni alijazwa roho ya hekima kwa sababu Mose alikuwa ameweka mikono yake juu yake. Kwa hiyo Waisraeli wakamsikiliza na wakafanya yale ambayo Bwana alikuwa amemwagiza Mose.

1034:10 Mwa 20:7; Kum 18:15-18; 5:4; Kut 33:11; Hes 12:6-8Tangu wakati huo, katika Israeli hajainuka nabii mwingine kama Mose, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso, 1134:11 Kum 4:34; 7:19; Kut 11:3aliyetenda ishara zote zile za miujiza na maajabu ambayo Bwana alimtuma kuyatenda huko Misri, yaani kwa Farao na maafisa wake wote na nchi yake yote. 1234:12 Ebr 3:1-6; Kum 4:34Kwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyewahi kuonyesha nguvu nyingi ama kutenda matendo ya kutisha ambayo Mose aliwahi kuyafanya mbele ya Israeli yote.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

申命记 34:1-12

摩西去世

1摩西摩押平原登上尼波山,上到耶利哥对面的毗斯迦山顶。耶和华把整片土地指给他看,从基列一直到2拿弗他利全境,以法莲玛拿西地区,远至地中海的犹大全境, 3南地和棕榈城耶利哥的谷地,远至琐珥4耶和华对摩西说:“这便是我向亚伯拉罕以撒雅各起誓要赐给他们子孙的土地。现在我让你亲眼看到了,但你不能进入。”

5于是,耶和华的仆人摩西死在摩押,正如耶和华所言。 6耶和华把他安葬在摩押境内伯·毗珥对面的山谷,至今无人知道摩西的坟墓在哪里。 7摩西去世时一百二十岁,眼睛没有昏花,精力没有衰败。 8以色列人在摩押平原为摩西致哀三十天,服丧的日子才结束。

9的儿子约书亚充满了智慧之灵,因为摩西曾把手按在他身上。以色列人都听从他,遵守耶和华对摩西的吩咐。

10此后,以色列再也没有出现像摩西那样的先知,他曾面见耶和华, 11奉耶和华的命令在埃及行神迹奇事,惩罚法老及其臣仆和国民, 12以色列人面前行伟大而可畏的事。