Kumbukumbu 33 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 33:1-29

Mose Anayabariki Makabila

133:1 Mwa 27:4; Yos 14:6; 1Sam 2:27; 9:6; 1Fal 12:22; 13:1; 2Fal 1:9-13; 5:2; Yer 35:4Hii ndiyo baraka Mose mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake. 233:2 Kut 19:18; Za 68:8; Yos 11:17; Amu 5:4; Za 50:2; 80:1; 94:1; Hes 10:12; Za 89:7; Dan 4:13; 7:10; 8:13; Zek 14:5; Mdo 7:53; Gal 3:19; Ebr 2:2; Ufu 5:11Alisema:

Bwana alikuja kutoka Mlima Sinai,

akachomoza kama jua juu yao

kutoka Mlima Seiri,

akaangaza kutoka Mlima Parani.

Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu

kutoka kusini,

kutoka materemko ya mlima wake.

333:3 Kum 4:37; 7:6; Lk 10:39; Ufu 4:10; Hos 11:1; Kum 14:2Hakika ni wewe ambaye huwapenda watu,

watakatifu wako wote wamo mkononi mwako.

Miguuni pako wote wanasujudu

na kutoka kwako wanapokea mafundisho,

433:4 Kum 4:2; Yn 1:7; 7:19; Za 19:11sheria ile Mose aliyotupa sisi,

tulio milki ya kusanyiko la Yakobo.

533:5 Kut 16:8; 1Sam 10:19; Za 10:16; 149:2; Hes 23:21; Kum 32:15; Ay 29:25Alikuwa mfalme juu ya Yeshuruni33:5 Yeshuruni maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli.

wakati viongozi wa watu walipokusanyika,

pamoja na makabila ya Israeli.

633:6 Mwa 34:5“Reubeni na aishi, asife,

wala watu wake wasiwe wachache.”

7Akasema hili kuhusu Yuda:

“Ee Bwana, sikia kilio cha Yuda,

mlete kwa watu wake.

Kwa mikono yake mwenyewe hujitetea.

Naam, uwe msaada wake

dhidi ya adui zake!”

833:8 Mwa 29:34; Kut 28:30; Za 106:16; Hes 14:22; 27:21; Kut 17:7Kuhusu Lawi alisema:

“Thumimu yako na Urimu33:8 Thumimu na Urimu maana yake Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. yako ulimpa,

mtu yule uliyemfadhili.

Ulimjaribu huko Masa

na kushindana naye

kwenye maji ya Meriba.

933:9 Kut 32:26-29; Za 61:5; Mal 2:5Alinena hivi kuhusu baba yake na mama yake,

‘Mimi siwahitaji kamwe.’

Akawasahau jamaa zake,

asiwatambue hata watoto wake,

lakini akaliangalia neno lako

na kulilinda Agano lako.

1033:10 Ezr 7:10; Neh 8:18; Za 119:151; Yer 23:22; Mal 2:6; Law 10:11; Kum 17:8-11; 13:9-13; Kut 30:7; Law 16:12-13; Za 51:19Humfundisha Yakobo mausia yako

na Israeli sheria yako.

Hufukiza uvumba mbele zako

na sadaka nzima za kuteketezwa

juu ya madhabahu yako.

1133:11 2Sam 24:23; Za 20:3; 51:19Ee Bwana, bariki ustadi wake wote,

nawe upendezwe na kazi ya mikono yake.

Vipige viuno vya wale wainukao dhidi yake;

wapige adui zake hata wasiinuke tena.”

1233:12 Mwa 35:18; Kum 4:37-38; 12:10; 32:8; Kut 19:4; Za 60:5; 127:2; Kut 28:12Kuhusu Benyamini akasema:

“Mwache mpenzi wa Bwana

apumzike salama kwake,

kwa maana humkinga mchana kutwa,

na yule Bwana ampendaye

hupumzika kati ya mabega yake.”

1333:13 Mwa 30:24; 27:28; Za 148:7; Mwa 49:25Kuhusu Yosefu akasema:

Bwana na aibariki nchi yake

kwa umande wa thamani

kutoka mbinguni juu,

na vilindi vya maji

vilivyotulia chini;

14pamoja na vitu vilivyo bora sana

viletwavyo na jua,

na vitu vizuri sana vinavyoweza

kutolewa na mwezi;

1533:15 Hab 3:6pamoja na zawadi bora sana

za milima ya zamani

na kwa wingi wa baraka

za vilima vya milele;

1633:16 Kut 3:2; Mwa 37:8pamoja na baraka nzuri mno

za ardhi na ukamilifu wake,

na upendeleo wake yeye

aliyeishi kwenye kichaka

kilichokuwa kinawaka moto.

Hivi vyote na vikae juu ya kichwa cha Yosefu,

juu ya paji la uso la aliye mkuu

miongoni mwa ndugu zake.

1733:17 1Sam 2:10; 2Sam 22:3; Eze 34:21; Hes 23:22; 1Fal 22:11; Za 44:5; Mwa 41:51-52Katika fahari yeye ni kama fahali mzaliwa wa kwanza;

pembe zake ni pembe za nyati,

na kwa pembe hizo atapiga mataifa,

hata yaliyo miisho ya dunia.

Hivyo ndivyo yalivyo makumi elfu ya Efraimu;

hivyo ndivyo yalivyo maelfu ya Manase.”

1833:18 Mwa 30:18-20; 49:13-15Kuhusu Zabuloni akasema:

“Shangilia, Zabuloni, wakati wa kutoka nje,

nawe Isakari, katika mahema yako.

1933:19 Kut 15:17; Za 48:1; Isa 2:3; 65:11; 66:20; Yer 31:6; Za 4:5; 51:19; Isa 18:7; 23:18; 45:14; 60:5; 11; 61:6; Hag 2:7; Zek 14:14Watawaita mataifa kwenye mlima,

na huko mtatoa dhabihu za haki;

watajifurahisha kwa wingi uliojaza bahari,

kwa hazina zilizofichwa mchangani.”

2033:20 Mwa 30:11; Kum 3:12-17; Mwa 49:19Kuhusu Gadi akasema:

“Atabarikiwa yeye aongezaye milki ya Gadi!

Gadi huishi huko kama simba,

akirarua kwenye mkono au kichwa.

2133:21 Hes 32:1-5, 31-32; 34:14; Yos 22:1-3; 4:14Alijichagulia nchi nzuri kuliko zote

kwa ajili yake mwenyewe;

fungu la kiongozi lilikuwa limehifadhiwa

kwa ajili yake.

Viongozi wa watu walipokusanyika,

alitimiza haki ya mapenzi ya Bwana,

na hukumu zake kuhusu Israeli.”

2233:22 Yos 19:47; Amu 18:27Kuhusu Dani akasema:

“Dani ni mwana simba,

akiruka kutoka Bashani.”

2333:23 Mwa 30:8; Yos 19:32Kuhusu Naftali akasema:

“Naftali amejaa tele upendeleo wa Bwana,

naye amejaa baraka yake;

atarithi magharibi na kusini.”

2433:24 Mwa 30:13; 49:20; Kum 32:13; Ay 29:6Kuhusu Asheri akasema:

“Aliyebarikiwa zaidi sana katika wana ni Asheri;

yeye na apate upendeleo kwa ndugu zake,

yeye na anawe miguu yake kwenye mafuta.

2533:25 Neh 3:3; 7:3; Za 147:13; Kum 32:47Makomeo ya malango yako yawe chuma na shaba,

nazo nguvu zako zitakuwa sawa na siku zako.

2633:26 Kum 32:15; Za 18:10; 68:33; Kum 10:14; Za 104:3; 2Sam 22:10; Za 18:9; 68:4; Dan 7:13; Kut 15:7“Hakuna mwingine kama Mungu wa Yeshuruni,

ambaye hupanda juu ya mbingu ili akusaidie,

na juu ya mawingu katika utukufu wake.

2733:27 Kut 15:18; Isa 40:28; 57:15; Za 9:9; 84:1; 90:1; 91:9; Mwa 21:33; Kut 34:11; Yos 24:18; Kum 7:2Mungu wa milele ni kimbilio lako,

na chini kuna mikono ya milele.

Atamfukuza adui yako mbele yako,

akisema, ‘Mwangamize yeye!’

2833:28 Kut 33:16; Law 25:18; Kum 32:8; Za 16:9; Mit 1:33; Isa 14:30; Mwa 27:28Hivyo Israeli ataishi salama peke yake.

Mzao wa Yakobo ni salama

katika nchi ya nafaka na divai mpya,

mahali ambapo mbingu

hudondosha umande.

2933:29 Za 1:1; 132:1-2; 144:15; 118:7; 18:44; 66:3; 54:4; 81:15; 10:14; 18:1; 27:1; 9; 30:10; 70:5; 115:9-11; 2Sam 22:45; Kum 4:7; 32:13; Mwa 15:1; Kut 18:4; Hab 3:19; Hos 13:9; Isa 45:24; 2Sam 7:23; Hes 33:52Ee Israeli, wewe umebarikiwa!

Ni nani kama wewe,

taifa lililookolewa na Bwana?

Yeye ni ngao yako na msaada wako,

na upanga wako uliotukuka.

Adui zako watatetemeka mbele yako,

nawe utapakanyaga

mahali pao pa juu.”33:29 Utapakanyaga mahali pao pa juu maana yake mtakanyaga juu ya miili yao.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

申命記 33:1-29

摩西最後的祝福

1以下是上帝的僕人摩西臨終時給以色列人的祝福:

2「耶和華從西奈山來,

西珥山向我們顯現,

祂從巴蘭山發出光輝;

祂帶著千萬聖者來臨,

祂右邊有閃耀的光芒。

3祂深愛自己的子民,

眾聖者都聽命於祂,

伏在祂的腳前,

領受祂的訓誨。

4摩西將律法頒佈給我們,

作為雅各子孫的產業。

5百姓的眾首領齊聚,

以色列各支派集合之時,

耶和華在耶書崙做王。」

6摩西祝福呂便支派說:

「儘管呂便人數稀少,

願他存活,不致滅沒。」

7摩西祝福猶大支派說:

「耶和華啊,

求你聽猶大人的呼求,

帶他們回歸本族,

出手為他們爭戰,

幫他們對抗仇敵。」

8摩西祝福利未支派說:

「耶和華啊,

求你把土明和烏陵賜給虔誠的利未人,

你曾經在瑪撒試驗他們,

米利巴泉邊與他們爭論。

9為了聽從你的話,遵守你的約,

他們不顧父母,

捨棄弟兄,拋下兒女。

10他們把你的典章傳授給雅各

把你的律法傳授給以色列

他們要把香獻在你面前,

把全牲燔祭獻在你的壇上。

11耶和華啊,

求你賜他們力量,

悅納他們的工作,

擊碎仇敵的腰桿,

使敵人一蹶不振。」

12摩西祝福便雅憫支派說:

「耶和華所愛的人,

安居在祂身邊,

安居在祂懷中,

終日蒙祂庇護。」

13摩西祝福約瑟家族說:

「願他們的土地蒙耶和華賜福,

得天上的甘霖,

及地下的泉源;

14得日月之輝,物產豐美;

15得古老群山之精華,

永存丘陵之富饒;

16得大地的豐肥,

蒙荊棘火中之上帝的恩寵。

願這些福氣落在約瑟頭上,

臨到弟兄中的王者身上。

17約瑟威武如頭生的公牛,

有野牛的角,

他用角牴萬邦,

直到地極。

他的兩角是數以萬計的以法蓮人和數以千計的瑪拿西人。」

18摩西祝福西布倫以薩迦支派說:

「願西布倫人欣然外出,

以薩迦人在帳篷中歡喜。

19他們要招聚眾人上山,

一同獻上公義的祭;

他們汲取海裡的財富和沙中的寶藏。」

20摩西祝福迦得支派說:

「擴張迦得疆界的那位當受稱頌!

迦得蹲伏如母獅,

撕碎頭顱和臂膀。

21他為自己選了最好的土地,

是留給首領的那份。

他與眾首領同行,

施行耶和華的公義和祂給以色列的典章。」

22摩西祝福支派說:

像一隻從巴珊躍出的幼獅。」

23摩西祝福拿弗他利支派說:

拿弗他利人啊,

你們飽嘗耶和華的恩寵,

滿得祂的賜福,

擁有西方和南方的土地。」

24摩西祝福亞設支派說:

「願亞設在眾子中最蒙福,

受眾弟兄的恩待,

雙腳沐浴橄欖油,

25城門有銅鎖鐵閂,

一生都充滿力量。

26耶書崙啊,

上帝獨一無二,

祂馳騁諸天,前來助你,

穿越長空,充滿威嚴。

27亙古的上帝是你的庇護,

祂永恆的臂膀是你的依託。

祂趕走你面前的仇敵,

下令毀滅他們。

28以色列安然居住,

雅各獨居一處,

那裡盛產五穀新酒,

有天上的雨露滋潤。

29以色列啊,你多麼有福!

蒙耶和華拯救之人啊,誰能像你?

祂是你的盾牌,你得勝的寶劍。

敵人要向你屈服,被你踐踏。」